bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 10
Acts 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 11 →
1
Kesaria kulikuwa na mtu, jina lake Kornelio, mkubwa wa kikosi cha askari kilichoitwa cha Italia.
2
Naye alimtii Mungu na kumcha pamoja nao wote wa nyumbani mwake: wengi wa kwao aliwagawia vipaji vingi, tena alikuwa akimwomba Mungu po pote.
3
Siku moja, alipokuwa kama saa tisa ya mchana, akaona njozi, yuko macho, akaona, malaika wa Mungu akiingia nyumbani mwake na kumwambia: Kornelio!
4
Naye akamkazia macho, akashikwa na woga, akasema: Nini, Bwana? Akamwambia: Maombo yako na magawio yako yamefika juu machoni pa Mungu, anayakumbuka.
5
Sasa hivi tuma watu, waende Yope, wamlete Simoni anayeitwa Petero!
6
amefikia kwa mtengenezaji wa ngozi, jina lake Simoni, nyumba yake iko pwani.
7
Malaika aliyesema naye alipokwenda zake, akaita watumishi wawili na askari mwenye kumcha Mungu miongoni mwao walioshikana naye siku zote,
8
akawasimulia yote, akawatuma, waende Yope.
9
Kesho yake wale walipokuwa njiani na kuufikia mji karibu, Petero alikuwa amepanda kwenda katika chumba cha juu, aombe, saa sita ilipofika.
10
Akaumwa na njaa, akataka kula. Walipomwandalia, akaingiwa na kituko,
11
kwani anaona: mbingu imefunuka, kutoka mle panashuka chombo kinachofanana na guo kubwa, linatelemshwa chini, likishikwa kwa pembe zake nne.
12
Mle ndani wamo nyama wote wenye miguu minne nao watambaao chini nao ndege wa angani.
13
Kisha akasikia sauti ya kumwambia: Inuka, Petero, uchinje, ule!
14
Ndipo, Petero aliposema: Hapana, Bwana! Kwani zamani zote sijala bado kilicho chenye mwiko au kisichotakata.
15
Lakini sauti ikamwambia mara ya pili: Mungu alivyovitakasa, wewe usivizie!
16
Vikafanyika hivyo mara tatu; kisha chombo kikapazwa mbinguni papo hapo.
17
Petero alipopotelewa moyoni mwake, asijue maana ya hayo, aliyoyaona, papo hapo wale watu waliotumwa na Kornelio wakasimama mlangoni wakiiuliza nyumba ya Simoni.
18
Wakapaza sauti na kuuliza, kama ndimo, Simoni anayeitwa Petero alimofikia.
19
Naye Petero alipoyafikiri moyoni, aliyoyaona, Roho akamwambia: Tazama, pana watu watatu wanaokutafuta!
20
Lakini inuka, ushuke, ufuatane nao pasipo mashaka! Kwani aliyewatuma ni mimi.
21
Ndipo, Petero aliposhuka, akawajia wale watu, akawaambia: Tazameni, mnayemtafuta ni mimi. Mmekuja kwa sababu gani?
22
Nao wakasema: Kornelio aliye mkubwa wa askari ni mtu mwongofu, mwenye kumcha Mungu, hata wote wa taifa la Wayuda wanamsemea vizuri; huyo ameagizwa na malaika mtakatifu, atume kwako, uje nyumbani mwake, ayasikie, utakayomwambia.
23
Ndipo, alipowakaribisha na kuwafikiza. Kesho yake akainuka, akatoka pamoja nao, hata wengine wa Yope waliokuwa ndugu wakaenda pamoja naye.
24
Siku ya kesho akaingia Kesaria. Naye Kornelio alikuwa akiwangoja; kwa hiyo alikuwa amewakusanya ndugu zake nao walio wapenzi wake wa kweli.
25
Petero alipoingia, Kornelio akamwendea, akamwamkia na kumwangukia miguuni.
26
Lakini Petero akamwinua akisema: Simama! kwani mimi nami ni mtu tu.
27
Akaongea naye akiingia ndani; akawakuta wengi waliokusanyika,
28
akawaambia: Ninyi mmejua, ya kuwa mtu wa Kiyuda ana mwiko wa kugandamiana na mtu wa kabila jingine au kumfikia. Lakini Mungu amenionyesha, nisimwazie mtu wo wote, kwamba ni wa mwiko au wa mzio.
29
Kwa sababu hiyo nimekuja pasipo kubisha, ulipotuma kwangu. Sasa nawauliza: Ni neno gani, mlilonitumia?
30
Kornelio akasema: Leo ni siku ya nne, tangu nilipokuwa nikifunga mpaka saa hii, tena nikimwomba Mungu nyumbani mwangu, saa tisa ilipofika. Papo hapo mtu alisimama mbele yangu aliyevaa nguo zilizomerimeta.
31
Naye akasema: Kornelio, maombo yako yamesikiwa, nayo magawio yako yamekumbukwa mbele ya Mungu.
32
Tume watu, waende Yope, wamwite Simoni anayeitwa Petero! Huyu amefikia nyumbani mwa Simoni aliye mtengenezaji wa ngozi, anakaa pwani.
33
Papo hapo nikatuma kwako, nawe umefanya vema ukija. Sasa sisi sote tupo hapa mbele ya Mungu, tuyasikilize yote, uliyoagizwa na Bwana.
34
*Petero akakifumbua kinywa chake, akasema: Naitambua kabisa iliyo kweli, ya kuwa Mungu hautazami uso wa mtu,
35
lakini katika mataifa yote anayemcha yeye na kufanya yaongokayo humpendeza.
36
Neno lake alilituma, liwafikie wana wa Isiraeli, akiwapigia ile mbiu njema ya utengemano uliopatikana kwa Yesu Kristo. Huyu ndiye Bwana wao wote.
37
Ninyi mnayajua mambo yale yaliyofanyika katika nchi yote ya Yudea, yaliyoanza huko Galilea, Yohana alipokwisha kuutangaza ubatizo wake.
38
Yesu wa Nasareti, Mungu alipomchagua kuwa mfalme na kumpa Roho takatifu na uwezo, alipita huko na huko akifanya mema na kuwaponya wote waliopagawa na yule Msengenyaji, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.
39
Nasi tumeyaona yote, aliyoyafanyiza katika nchi ya Wayuda namo Yerusalemu. Huyo walimwangamiza na kumtundika mtini,
40
lakini Mungu akamfufua siku ya tatu, akamtuma, atokee;
41
lakini sio watu wote waliotokewa naye, ni sisi tu tuliochaguliwa na Mungu kale, tuwe mashahidi; ni sisi tuliokula, tena tuliokunywa pamoja naye, alipokwisha kufufuka katika wafu.*
42
*Akatuagiza kutangazia watu na kuyashuhudia po pote, ya kuwa ndiye aliyewekwa na Mungu, awahukumu wanaoishi nao waliokufa.
43
Kwa kumwelekea huyu Wafumbuaji wote hushuhudia, ya kuwa kila atakayemtegemea atapata kuondolewa makosa kwa Jina lake.
44
Petero akingali akiyasema maneno haya, Roho Mtakatifu akawaguia wote waliolisikia lile neno.
45
Ndipo, wenye kumtegemea Bwana waliotahiriwa, waliokuja pamoja na Petero, waliposhangaa sana, ya kuwa hata wamaizimu humiminiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.
46
Kwani waliwasikia, wakisema misemo migeni na kumkuza Mungu. Ndipo, Petero alipojibu:
47
Yuko nani anayeweza kukataza maji, hawa wasibatizwe waliompokea Roho Mtakatifu sawasawa kama sisi?
48
Akaagiza, wabatizwe katika Jina la Yesu Kristo.* Kisha wakamwomba, akae kwao siku kidogo.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28