bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 12
Acts 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 13 →
1
Siku zile mfalme Herode alikuwa amekamata wengine miongoni mwao wateule, awafanyizie maovu.
2
Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.
3
Alipoona, ya kuwa Wayuda wamependezwa, akaendelea, akamkamata naye Petero, siku za mikate isiyochachwa zilipotimia.
4
Alipokwisha kumkamata akamtia kifungoni, akaagiza vikosi vinne, kila kikosi cha askari wanne, wamlinde kwa zamu, akataka kumtia mikononi mwa watu, siku za Pasaka zitakapokuwa zimepita.
5
Petero alipolindwa hivyo kifungoni, wateule wakamwombea kwa Mungu pasipo kuchoka.
6
Lakini hapo, Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule Petero alikuwa amelala katikati ya askari wawili akiwa amefungwa na mapingu mawili; nao walinzi walikilinda kifungo mlangoni.
7
Mara malaika wa Bwana akasimama hapo karibu, nao mwanga ukamulika chumbani. Akamwamsha Petero kwa kumpiga ubavu akisema: Inuka upesi! Ndipo, mapingu yalipomwanguka mikononi.
8
Kisha malaika akamwambia: Jifunge nguo zako, uvae navyo viatu vyako! Alipokwisha kufanya hivyo, akamwambia tena: Jivike kanzu yako, unifuate!
9
Kisha akatoka akimfuata, asijue, kama ni kweli yaliyofanyika na malaika; maana aliwaza, ameona njozi.
10
Wakapita zamu ya kwanza ya walinzi na ya pili, wakalifikia lango la chuma linaloelekea mjini, nalo likawafungukia lenyewe, wakatoka; walipoendelea njia tu, papo hapo ndipo, malaika alipoondoka na kumwacha.
11
Naye Petero, moyo wake ulipomrudia, akasema: Sasa nimejua kweli ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake, akaniokoa katika mkono wa Herode na katika mangojeo yote ya watu wa kwao Wayuda.
12
Alipokuwa akiyawaza hayo akaifikia nyumba ya Maria, mama yake Yohana anayitwa Marko; ndimo, wengi walimokuwa wamekusanyikia kuomba.
13
Alipogonga kilango kilichomo langoni, akaja kijakazi kusikiliza, jina lake Rode.
14
Naye alipoutambua mtamko wa Petero hakulingua lango kwa furaha, ila akaingia mbio, akawaambia, ya kuwa Petero amesimama langoni.
15
Nao wakamwambia: Una wazimu. Lakini alipokaza kusema, ya kuwa ndivyo, wakasema: Ni malaika wake.
16
Petero alipofuliza kugonga, wakamfungulia, wakamwona, wakashangaa sana.
17
Akawapungia mkono, wanyamaze; kisha akawasimulia, jinsi Bwana alivyomtoa kifungoni, akasema: Habari wapasheni nao akina Yakobo nao walio ndugu! Kisha akatoka, akaenda mahali pengine.
18
Palipokucha, pakapatikana mahangaiko mengi kwa askari, wasijue, jinsi ya Petero yalivyowezekana.
19
Naye Herode asipompata hapo, alipomtaka, akawaulizauliza walinzi, akaagiza, wafungwe. Kisha akaondoka Yudea, akatelemka kwenda Kesaria, akatua huko.
20
Lakini moyoni alifikiri kuwashambulia watu wa Tiro na Sidoni; ndipo, walipomwendea wote pamoja, wakamhonga Bulasto aliyekuwa mshika funguo wa mfalme, wakamwomba, awaamue, kwa sababu walichuma vyakula vyao katika nchi ya mfalme.
21
Siku, waliyopatania, Herode akavaa nguo ya kifalme, akakaa katika kiti cha uamuzi, akatoa maneno.
22
Watu walipoitikia kwamba: Ni Mungu, tunayemsikia, si mtumtu tu,
23
papo hapo malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. Akawa akiliwa na vidudu, akakata roho.
24
Lakini Neno la Bwana likakua na kuenea pengi.
25
Barnaba na Sauli walipoimaliza kazi yao wakarudi toka Yerusalemu wakimchukua naye Yohana aliyeitwa Marko
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28