bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 5
Acts 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 6 →
1
Kulikuwa na mtu jina lake Anania, na mkewe Safira; huyu alipouza kiunga
2
akaficha fungu la fedha, alizozipata, naye mkewe alivijua. Kisha akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume.
3
Lakini Petero akasema: Anania, mbona Satani ameenea moyoni mwako, ukamdanganya Roho Mtakatifu na kuficha fungu la fedha za kiunga?
4
Hakikuwa mali yako, uliyoweza kukaa nayo? Hata kilipokwisha kuuzwa, je? Hukuweza kufanya, kama ulivyopenda? Mbona umelitia jambo hilo moyoni mwako? Hukudanganya watu, ila umemdanganya Mungu.
5
Anania alipoyasikia maneno haya akaanguka chini, akakata roho. Ndipo, woga mwingi ulipowaingia wote walioyasikia.
6
Kisha vijana wakainuka, wakamfunga nguo, wakampeleka nje, wakamzika.
7
Zilipopita kama saa tatu, mkewe akaingia, asiyajue yaliyofanyika.
8
Petero akamwuliza: Niambie: Fedha, mlizozipata kwa kukiuza kiunga, ndizo hizi? Naye aliposema: Ndio, ni zizi hizi,
9
Petero akamwambia: Mbona ninyi mmepatana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama, miguu yao waliomzika mumeo iko nje mlangoni, watakupeleka wewe nawe!
10
Papo hapo akaanguka chini miguuni pake, akakata roho. Wale vijana walipoingia na kumkuta, amekufa, wakampeleka nje, wakamzika hapo pa mumewe.
11
Ndipo, woga mwingi ulipowaingia wateule wote nao wote walioyasikia haya.
12
Vikafanyika vielekezo na vioja vingi kwa mikono ya mitume kwa watu wa kwao, wale wote wakiwa pamoja katika ukumbi wa Salomo, kwa sababu mioyo yao ilikuwa ilikuwa mmoja.
13
Lakini wengine hakuna hata mmoja aliyejipa moyo na kugandamiana nao, maana watu waliwakuza.
14
Nao waliomtegemea Bwana wakaongezeka sana, ni vikundi vizima vya wanaume na vya wanawake.
15
Kwa hiyo watu wakawatoa hata wagonjwa, wakawaweka njiani, wakilala vitandani au majamvini, kwamba Petero akipita, kivuli chake tu kiwafikie mmojammoja.
16
Wakakusanyika hata watu wengi wa vijiji vilivyouzunguka Yerusalemu, wakaleta wagonjwa nao wenye kupagawa na pepo wachafu, wakaponywa wote.
17
Pakainuka mtambikaji mkuu nao wote waliokuwa naye, ndio wa chama kile cha Masadukeo; kwa kujaa wivu
18
wakawakamata mitume, wakawafunga na kuwapeleka kifungoni.
19
Lakini usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya kifungoni, akawatoa, akasema:
20
Nendeni, msimame Patakatifu kuwaambia watu wa kwenu maneno yote ya uzima huo!
21
Walipoyasikia haya wakapaingia Patakatifu, kulipokucha, wakafundisha. Lakini mtambikaji mkuu nao waliokuwa pamoja naye wakaja, wakawakusanya wenzao wakuu na wazee wote wa wana wa Isiraeli, wakatuma watu bomani, wawalete.
22
Hao watumishi walipofika hawakuwaona kifungoni, wakarudi, wakaleta habari
23
wakisema: Kifungo tumekikuta, kimefungwa vizuri na kukazwa sana, hata walinzi tuliwaona, wamesimama milangoni; lakini tulipofungua hatukuona mtu ndani.
24
Mlinda Patakafitu nao watambikaji wakuu walipoyasikia maneno haya wakahangaika sana, wasijue, jambo hilo litakavyokuwa.
25
Pakaja mtu, akawasimulia: Tazameni, watu hao, mliowatia kifungoni, wamo nyumbani mwa Patakatifu, wamesimama na kufundisha watu!
26
Ndipo, mlinda Patakatifu alipokwenda na watumishi, akawaleta, lakini si kwa nguvu, kwani waliwaogopa watu, wasije, wakawapiga mawe.
27
Walipowaleta, wakawasimamisha mbele yao wakuu. Mtambikaji mkuu akawauliza:
28
Hatukuwakemea kwa nguvu ya kwamba: Msifundishe mambo ya Jina hilo? Lakini tazameni, mafundisho yenu mmeyaeneza Yerusalemu, tena mwataka kutusingizia damu ya mtu yule.
29
Ndipo, Petero na mitume walipojibu wakisema: Sharti tumtii Mungu kuliko watu!
30
Mungu wa baba zetu amemfufua Yesu, mliyemwua ninyi na kumtundika mtini;
31
huyo ndiye, Mungu aliyempaza na kumketisha kuumeni kwake, awe kiongozi na mponya, ajutishe Waisiraeli, wapate kuondolewa makosa.
32
Nasi ndio mashahidi wa mambo hayo pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu aliyewapa wale waliomtii.
33
Walipoyasikia haya wakakereza meno, wakataka kuwaua.
34
*Kisha pakainuka hapo penye wakuu Fariseo, jina lake Gamalieli; ni mfunzi wa Maonyo mwenye cheo kwa watu wote, akaagiza, wale watu wapelekwe nje kidogo.
35
Kisha akawaambia: Waume Waisiraeli, jilindeni kwa ajili ya hayo, mtakayowatendea watu hawa!
36
Kwani mbele ya siku hizi aliondokea Teuda, akajiwazia, kwamba yeye ndiye mtu, nao watu waliomfuata wakapata kama 400. Alipouawa, wote waliomtii wakatawanyika, wakapoteapotea, tena hakuna kitu.
37
Kisha katika siku za kuandikiwa kodi aliondokea Yuda Mgalilea, akatenga kikundi cha watu, wamfuate yeye. Naye alipoangamia, wote waliomtii wakatawanyika nao.
38
Kwa hiyo sasa nawaambiani: Mtengamane na watu hawa, mwaache! Kwani mawazo hayo au kazi hizo zikiwa zimetoka kwa watu zitakoma;
39
lakini zikiwa zimetoka kwake Mungu, hamwezi kuwakomesha, msije mkaonekana, ya kuwa mnagombana na Mungu.
40
Ndipo, walipomwitikia, wakawaita wale mitume, wakawapiga, wakawakemea, wasiseme tena mambo ya Jina la Yesu, kisha wakawafungua.
41
Wao wakatoka machoni pa wakuu wakichangamka, kwa sababu Mungu amewapa kutwezwa kwa ajili ya Jina lake.
42
Siku zote hawakuacha kufundisha na kuutangaza Utume mwema wa Yesu Kristo hapo Patakatifu na nyumbani mo mote.*
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28