bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 19
Acts 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 20 →
1
Ikawa, Apolo alipokuwako Korinto, Paulo akazunguka hapo penye milima, kisha akafika Efeso, akaona wanafunzi wengine,
2
akawauliza: Mmepewa Roho takatifu mlipoanza kumtegemea Bwana? Nao wakamjibu: Hapana, hatujasikia, kama iko Roho takatifu.
3
Alipowauliza: Mmebatizwa ubatizo gani? wakasema: Tumebatizwa ubatizo wa Yohana.
4
Ndipo, Paulo aliposema: Yohana alibatiza ubatizo wa kujutisha akiwaambia watu, wamtegemee atakayekuja nyuma yake, naye ndiye Yesu.
5
Walipoyasikia wakabatiziwa Jina la Bwana Yesu.
6
Paulo alipowabandikia mikono, Roho Mtakatifu akawajia, akasema misemo migeni na kufumbua.
7
Nao wote walikuwa waume kama kumi na wawili.
8
Alipoingia nyumbani mwa kuombea, akapiga mbiu waziwazi yapata miezi mitatu, akaongeana nao mambo ya ufalme wa Mungu na kuwashinda.
9
Lakini palipopatikana wenye mioyo migumu waliokataa kutii, walipoifyoza ile njia mbele ya watu waliokusanyika hapo, akawaacha, akawatenga nao wanafunzi, akaongea na watu kila siku katika shule ya Tirano.
10
Vikawa hivyo kama miaka miwili; nao wote waliokaa Asia, Wayuda na Wagriki, wakapata kulisikia Neno la Bwana.
11
Mungu akaifanyisha mikono ya Paulo matendo ya nguvu yasiyokuwapo hata kale.
12
Kwa hiyo watu waliitwa hata miharuma na mishipi ya mwilini pake, wakawapelekea wagonjwa; ndipo, magonjwa yao yalipowaacha nao pepo wabaya wakawatoka.
13
Kulikuwa na wapunga pepo wa Kiyuda waliozunguka hapo, wakajaribu kuwatajia waliopagawa na pepo wabaya Jina la Bwana Yesu, wakisema: Nawaapiza kwa nguvu ya Yesu, Paulo anayemtangaza.
14
Nao waliovifanya hivyo walikuwa wana saba wa Sikewa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa Kiyuda.
15
Lakini pepo mbaya akawajibu: Yesu ninamtambua, naye Paulo ninamjua. Lakini ninyi, m wa nani?
16
Kisha yule mtu mwenye pepo mbaya akawarukia, akawakamata wawili, akawafanyizia vibaya kwa nguvu zake, mpaka wakakimbia mle nyumbani wenye uchi na wenye madonda.
17
Haya yakatambulikana kwa Wayuda na kwa Wagriki wote waliokaa Efeso, nao wote wakashikwa na woga, lakini Jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
18
Ndipo, wengi wao walioanza kumtegemea walipokuja kuyaungama matendo yao wakiyajutia.
19
Nao wengi wao waliofanya kazi za uganga wakavikusanya vyuo vyao, wakaviteketeza mbele yao wote. Wakazihesabu fedha zilizotumiwa, walipovinunua, wakaona, zilikuwa fedha 50000.
20
Hivyo Neno likakua, likapata nguvu kwa uwezo wa Bwana.
21
Hayo yalipomalizika, Paulo aliwaza moyoni kuzunguka katika Makedonia na Akea, apate kwenda Yerusalemu, akasema: Nikiisha kwenda huko, sharti niuone hata Roma!
22
Akatuma wawili waliomtumikia, Timoteo na Erasto, watangulie kwenda Makedonia, mwenyewe akakawia kidogo Asia.
23
Lakini siku zile ikawako kondo isiyokuwa ndogo kwa ajili ya hiyo njia.
24
Kwani kulikuwa na mfua fedha, jina lake Demetirio, aliyekuwa akitengeneza vijumba vya fedha kwa mfano wa nyumba ya kumwombea Artemi; ndivyo, alivyowapatia mafundi wengi mali nyingi.
25
Hao akawakusanya na wengine waliowafanyia kazi, akasema: Waume, mmejua: kazi hii ni chumo letu.
26
Tena mnaona, pengine mnasikia, ya kuwa si kwenu Efeso tu, ila hata katika nchi zote za Asia ndiko, huyu Paulo anakohimiza watu na kugeuza mioyo ya makundi mazima ya watu akisema: Miungu iliyofanyika kwa mikono siyo.
27
Lakini linalotuogopesha si hilo tu la kwamba: Uchumi wetu utatoweka, ila hata patakatifu pa Artemi aliye mungu wetu wa kike mkuu patabezwa kuwa si kitu. Tena pataangamia ujumbe wake mkuu unaotambikiwa na watu wote wa Asia na wa ulimwengu.
28
Walipoyasikia, makali yakawajaa, wakapiga kelele wakisema; Mkuu ni Artemi wa Waefeso!
29
Mji ukajaa machafuko, wakapiga mbio wote pamoja kwenda penye machezo, wakawakamata hapo na kuwaburura akina Gayo na Aristarko waliokuwa Wamakedonia, kwani waliandamana na Paulo.
30
Paulo alipotaka kuwatokea watu, wanafunzi wakamzuia;
31
nao wakubwa wa nchi za Asia wengine waliokuwa rafiki zake wakatuma mtu kwake, wakamtisha, asijitoe kwenda penye machezo.
32
Hapo walikuwa wanapiga kelele, wengine hivi, wengine hivi. Watu waliokusanyika hapo walikuwa wamevurugika, wengi hawakujua kilichowakusanya.
33
Watu wengine wakamshika Alekisandro, Wayuda waliyemsogeza, aje mbele. Naye Alekisandro akawapungia mkono, akataka kujikania mbele ya makutano;
34
lakini walipomtambua, ya kuwa ni Myuda, wakapiga kelele wote pamoja kwa sauti moja kama saa mbili kwamba: Mkuu ni Artemi wa Waefeso!
35
Mwandishi wa mji alipowanyamazisha wao wa makundi, akasema: Waume wa Efeso, yuko mtu asiyetambua kwamba: Mji wa Efeso ndio unaoilinda nyumba ya kumwombea Artemi aliye mkuu nao mfano wake uliotoka mbinguni?
36
Basi, kwa kuwa haya hayabishiki, imewapasa ninyi kutulia, msifanye neno kwa kikaka.
37
Kwani mmewaleta watu hawa wasionyang'anya vilivyomo nyumbani mwa kuombea, wala hawakumbeza mungu wetu.
38
Kama Demetirio na mafundi wenziwe wako na neno la kusuta mtu, siku za uamuzi ziko, hata waamuzi wako, basi, na wasutane!
39
Lakini mkiwa na neno jingine-jingine, litatimizwa mbele ya wale waliochaguliwa wa kazi hiyo.
40
Kwani tunajiponza kusutiwa ugomvi kwa ajili ya matata haya ya leo; tena hatutakuwa na neno la kujikania sisi kwa ajili ya kondo hii.
41
Alipokwisha kusema hivyo akauvunja mkutano.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28