bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 20
Acts 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 21 →
1
Lile fujo lilipotulia, Paulo akatuma watu kuwaita wanafunzi, akawatuliza mioyo, akaagana nao, akaondoka kwenda Makedonia.
2
Akapita pande zile akiwatuliza mioyo na kuwaambia maneno mengi, kisha akafidka Ugriki.
3
Akakaa huko miezi mitatu. Alipotaka kuingia chomboni, aende Ushami, Wayuda walimlia njama. Kwa hiyo akapendezwa kurudi na kupita Makedonia.
4
Waliofuatana naye mpaka Asia ni Sopatiro, mwana wa Puro wa Beroya, na Aristarko na Sekundo wa Tesalonike na Gayo wa Derbe na Timoteo; tena Tikiko na Tirofimo wa Asia.
5
Hao walitangulia, wakatungoja Tiroa.
6
Siku za mikate isiyotiwa chachu zilipopita, nasi tukatweka, tukaondoka Filipi, tukawafikia huko Tiroa siku ya tano, tukaa huko siku saba.
7
Siku ya kwanza ya juma tulipokuwa tumekusanyikia kumegeana mkate, Paulo akasema nao; kwa sababu alitaka kuondoka kesho yake, akaendelea kusema mpaka usiku wa manane.
8
Mkawa na taa nyingi katika chumba cha juu, tulimokuwa tumekusanyika.
9
Mlikuwa na kijana, jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, akasinzia mno. Paulo alipofuliza kusema, akashindwa na usingizi, akaanguka toka dari ya tatu mpaka chini, akainuliwa amekufa.
10
Lakini Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema: Msipige makelele! Kwani roho yake ingalimo mwake.
11
Akapanda tena, akamega mkate, akala, akaongea mengi nao, mpaka kulipopambazuka. ndivyo, alivyotoka huko.
12
Lakini yule kijana walimleta, yuko mzima, kwa hiyo mioyo yao ikawatulia kabisa.
13
Lakini sisi tulitangulia kuingia chomboni, tukatweka kwenda Aso; ndiko, tulikotaka kumpakia Paulo. Kwani alikuwa ametuagiza hivyo; mwenyewe alitaka kufika huko kwa miguu.
14
Naye alipokutana nasi huko Aso, tukampakia, tukafika Mitilene.
15
Tukatweka huko, kesho yake tukaelekea Kio; kesho kutwa tukatia nanga Samo, tukakaa Tirogilio, mtondogoo tukafika Mileto.
16
Kwani Paulo alitaka kupita Efeso kwa chombo, asipate kukawia katika Asia, maana alikwenda mbiombio, kwa sababu alitaka ikiwezekana, kuila sikukuu ya Pentekote huko Yerusalemu.
17
*Lakini toka Mileto alituma mtu Efeso kuwaita wazee wa wateule.
18
Hao walipofika kwake, akawaambia: Ninyi mnajua, nilivyokaa nanyi siku zote tangu siku ya kwanza, nilipofika Asia:
19
nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, hata nilipoulizwa, hata nilipojaribiwa na Wayuda mara kwa mara, wakininyatia.
20
Hakuna neno lenye kufaa, nililowanyika nikiacha kulitangaza, tena sikuacha kuwafundisha mkikusanyika au nikienda nyumba kwa nyumba.
21
Kwa ushahidi wangu nimewahimiza Wayuda na Wagriki, wajute na kurudi kwake Mungu, tena wamtegemee Bwana wetu Yesu.
22
Sasa tazameni, kwa hivyo, nilivyofungwa na Roho, ninakwenda Yerusalemu, nisijue yatakayonipata huko.
23
Naijua hii tu, ya kuwa Roho Mtakatifu hunishuhudia mijini mote, nifikamo, kwamba: Mapingu na maumivu yananingoja.
24
Lakini ninajiwazia kwamba: Si kitu, mwenyewe nikiangamia; lakini kilicho kitu, ni kuumaliza mwendo wangu na utumishi wangu, niliopewa na Bwana Yesu, niushuhudie Utume mwema wa gawio lake Mungu.
25
Sasa tazameni, mimi ninajua, ya kuwa hamtauona tena uso wangu ninyi nyote, ambao nilipita kwao na kuutangaza ufalme.
26
Kwa hiyo ninawaambia waziwazi siku hii ya leo kwamba: Ninyi nyote hakuna, ambaye ninawiwa naye damu ya mtu.
27
Kwani sikuacha kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.
28
Jilindeni wenyewe na kikundi chote! Kwani Roho Mtakatifu amewaweka, mwe wakaguzi wao, mwachunge wateule wake Mungu, aliojichumia kwa kuitoa damu yake mwenyewe.
29
Mimi najua: Nitakapokwisha kuondoka, wataingia chui wakali kwenu wasiowaonea huruma wao wa kikundi hiki.
30
Tena miongoni mwenu wenyewe watainuka watu wakaofundisha mapotovu, wapate kuwavuta nao walio wanafunzi, wawaandamie.
31
Kwa hiyo kesheni na kukumbuka, ya kuwa miaka mitatu sikuacha usiku na mchana kumwonya kila mmoja kwa kutoa machozi!
32
Sasa hivi ninawaweka mikononi mwake Mungu, awagawie Neno lake linaloweza kuwajenga na kuwapa fungu kwao wote waliotakaswa.
33
Sikutaka fedha au dhahabu au mavazi ya mtu.
34
Mnatambua wenyewe: hii mikono yangu imetumika kunichumia yaliyotulisha mimi na wenzangu waliokuwa pamoja nami.
35
Kwangu mimi nimewaonyesha yote, ya kuwa imetupasa kusumbukia kazi vivyo hivyo, tupate kuwasaidia wanyonge, tukiyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, aliyoyasema mwenyewe: Kumpa mtu huna upato kuliko kupewa.
36
Alipokwisha kusema hivyo akapiga magoti pamoja nao wote, akaomba.
37
Wote wakalia sana, wakamkumbatia Paulo lshingoni, wakamnonea.
38
Lililowasikitisha zaidi ni neno lile, alilolisema, ya kuwa hawatamwona tena uso kwa uso. Kisha wakamsindikiza hata chomboni.*
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28