bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 7
Acts 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 8 →
1
Mtambikaji mkuu alipomwuliza: Ndivyo, yalivyo mambo haya?
2
akasema: Waume ndugu na baba, sikilizeni! Mungu mwenye utukufu alimtokea baba yetu Aburahamu, alipokaa Mesopotamia, alipokuwa hajahamia Harani,
3
akamwambia: Toka katika nchi yako kwenye ndugu zako, uende katika nchi, nitakayokuonyesha!
4
Ndipo, alipotoka katika nchi ya Wakasidi, akahamia Harani. Tena, baba yake alipokwisha kufa, akamhamisha toka huko, akamweka katika nchi hii, mnayoikaa ninyi sasa.
5
Lakini hakumpa fungu humu, ingawa liwe limelingana na wayo; ila alipokuwa hana mtoto, aliagana naye, ya kuwa atampa, aitwae nchi hii yeye nao wa uzao wake wajao nyuma yake.
6
Kisha Mungu akavisema: Wao wa uzao wake watakaa ugenini katika nchi ngeni, wale wawafanyishe kazi za watumwa na kuwasumbua vibaya miaka 400.
7
Nalo taifa lile, ambalo watalifanyika kazi za watumwa, nitawahukumu mimi, wale wapate kuhama huko, wanitumikie mahali hapa; ndivyo, alivyosema Mungu.
8
Kisha akampa agano la tohara; kwa hiyo alipomzaa Isaka akamtahiri siku ya nane; naye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa babu zetu wakuu kumi na wawili.
9
Wale babu zetu wakuu wakamwonea Yosefu wivu, wakamwuza kwenda Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,
10
akamwokoa katika maumivu yake yote, akamgawia kipaji cha werevu wa kweli, apate kusema mbele ya Farao, mfalme wa Misri; ndiye aliyemweka kuwa mkubwa, aitawale Misri na nyumba yake yote.
11
Njaa ilipokuja kuiingia Misri yote na Kanaani, yakawa maumivu makubwa, baba zetu nao wasione vya kujishibisha.
12
Lakini Yakobo aliposikia, ya kuwa Misri ziko ngano, akawatuma baba zetu mara ya kwanza.
13
Katika safari ya pili Yosefu akajitambilisha kwa ndugu zake, nako kwa Farao ukoo wa Yosefu ukajulika.
14
Kisha Yosefu akatuma watu, akamwita baba yake Yakobo na ndugu zake wote, wakawa kama 75.
15
Ndipo, Yakobo alipotelemka kwenda Misri. Huko akafa yeye mwenyewe nao baba zetu,
16
wakapelekwa Sikemu, wakazikwa katika kaburi, alilolinunua Aburahamu na fedha kwa wana wa Hamori kule Sikemu.
17
Siku zilipokaribia, Mungu alizoziagana na Aburahamu na kujiapisha, watu wa kwetu wakazidi kuwa wengi sana huko Misri,
18
mpaka alipoondokea mfalme mwingine wa Misri asiyemjua Yosefu.
19
Huyo akawaendea wao wa kizazi chetu kwa udanganyi, akawatendea baba zetu maovu akiagiza, vitoto vyao vichanga watupwe, wasikae kuwa wazima.
20
Siku zile Mose akazaliwa, Mungu akapendezwa naye. Kwa hiyo akalelewa miezi mitatu nyumbani mwa baba yake;
21
kisha alipotupwa, binti Farao akamwokota, akamlea, awe mwanawe yeye.
22
Naye Mose akafundishwa ujuzi wote wa Wamisri, akawa mwenye nguvu kwa maneno na kwa matendo yake.
23
Tena miaka yake ilipopata 40, moyo wake ukamtuma kuwakagua ndugu zake, wale wana wa Isiraeli.
24
Alipoona, mmoja anavyoumizwa bure tu, akamsaidia yule aliyepigwa, akamlipiza yule Mmisri akimwua.
25
Akadhani, ndugu zake watajua, ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake yeye; lakini hawakujua.
26
Kulipokucha, akawajia tena, akawaona, wakipigana; akawaamua, wapatane, akisema: Waume, ninyi m ndugu, mbona mnakorofishana?
27
Lakini yule aliyemkorofisha mwenziwe akamsukuma akisema: Yuko nani aliyekuweka kuwa mkuu mwamuzi kwetu?
28
Je? Wewe unataka kuniua nami, kama ulivyomwua jana yule Mmisri?
29
Kwa ajili ya neno hilo Mose akakimbia, akawa mgeni katika nchi ya Midiani. Ndiko, alikozaa wana wawili.
30
Ilipokwisha pita tena miaka 40, malaika akamtokea porini mlimani kwa Sinai katika kichaka kilichowaka moto.
31
Mose alipoyaona hayo akastaajabu; lakini alipopakaribia kuyatazama akasikia, Bwana akisema:
32
Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Yakobo. Ndipo, Mose alipotetemeka, hakupata moyo wa kupatazama.
33
Naye Bwana akamwambia: Vivue viatu miguuni pako! Kwani hapa, unaposimama, ni nchi takatifu.
34
Nimeyaona mateso yao walio ukoo wangu walioko Misri; nikasikia, wanavyopiga kite, nikashuka, niwaokoe. Sasa njoo! Nitakutuma, uende Misri.
35
Huyo Mose, waliomkataa na kusema: Yuko nani aliyekuweka kuwa mkubwa na mwamuzi? huyo ndiye, Mungu aliyemtuma kuwa mkubwa na mwokozi, awaokoe kwa mkono wa malaika aliyemtokea kichakani.
36
Kisha huyo akawatoa na kufanya vioja na vielekezo katika nchi ya Misri na katika Bahari Nyekundu, kisha nako jangwani miaka 40.
37
Huyo ndiye yule Mose aliyewaambia wana wa isiraeli: Miongoni mwa ndugu zenu Mungu atawainulia mfumbuaji atakayelingana na mimi.
38
huyo ndiye aliyekuwa penye wateule jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye mlimani kwa Sinai, tena pamoja na baba zetu. Ndiye aliyepokea maneno ya uzima, atupe sisi;
39
tena ndiye, ambaye baba zetu hawakutaka kumtii, wakamsukuma, wakageuka mioyoni mwao, kwamba warudi Misri,
40
wakamwambia Haroni: Tufanyie miungu itakayotuongoza! Kwani huyo Mose aliyetutoa katika nchi ya Misri hatuyajui yaliyompata.
41
Siku zile wakatengeneza ndama, nacho kinyago hicho wakakitolea ng'ombe za tambiko, nacho kilichokuwa kazi ya mikono yao wakakishangilia.
42
Kisha Mungu akageuka, akawatupa, wavitumikie vikosi vya mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Wafumbuaji: Je? Ng'ombe na vipaji, mlivyovitoa nyikani miaka 40, vilikuwa vya kunitambikia mimi, ninyi mlio mlango wa Isiraeli?
43
Hapana, ila mlikuwa mmejitwika hema la Moloko na nyota za mungu wa Romfa; hivyo vinyago, mlivyovitengeneza, ndivyo, mlivyovitumia vya kuviangukia. Kwa hiyo nitawahamisha ninyi, mwende mbali kupita Babeli.
44
Baba zetu walipokuwa jangwani walikuwa nalo lile Hema la Ushahidi, kama mwenye kusema na Mose alivyoagiza na kumwambia, alitengeneze kwa mfano, aliouona.
45
Nao baba zetu wakalipokea tena wakiongozwa na Yosua, wakaliingiza katika nchi ya wamizimu, Mungu aliowafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Dawidi.
46
Huyo akaonea mapendeleo machoni pa Mungu, akaomba ruhusa ya kumpatia Mungu wa Yakobo makazi,
47
lakini Salomo ndiye aliyemjengea Nyumba.
48
Lakini yeye Alioko huko juu hakai katika nyumba zilizojengwa na mikono ya watu. Ndivyo, anavyosema mfumbuaji:
49
Mbingu ni kiti changu cha kifalme, nayo nchi ni pa kuiwekea miguu yangu. kwa hiyo Bwana anasema: Ni nyumba gani, mtakayonijengea? Au mahali pa kupumzikia mimi ni mahali gani?
50
Sio mkono wangu ulioyafanya hayo yote?
51
Ninyi wenye kosi ngumu, ninyi wenye mioyo na masikio yaliyo kama ya watu wasiotahiriwa, ninyi kila mara humpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zenu, vivi hivi ninyi nanyi.
52
Ni mfumbuaji gani, ambaye baba zenu hawakumfukuza? Nao walianza kupiga mbiu za kuja kwake huyo Mwongofu waliwaua, tena ni yuleyule, mliyemchongea, kisha mkamwua;
53
Maonyo mliyapokea kwa kuagizwa na malaika, lakini hamkuyalinda.
54
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyoni mwao, wakamkerezea meno.
55
Lakini yeye akajaa Roho takatifu, akayaelekeza macho mbinguni akaona utukufu wa Mungu, akamwona naye Yesu, akiwa amesimama kuumeni kwa Mungu,
56
akasema: Tazameni, naziona mbingu, zimefunuka, naye Mwana wa mtu amesimama kuumeni kwa Mungu.
57
Ndipo, walipopiga kelele na kupaza sauti na kujiziba masikio, wakamrukia wote pamoja,
58
wakamkumba, atoke mjini, wakampiga mawe. Kulikuwako mashahidi, nao wakazivua nguo zao, wakaziweka miguuni pa kijana, jina lake Sauli,
59
kisha nao wakampiga Stefano mawe, yeye akiomba na kusema: Bwana Yesu, ipokee roho yangu!
60
Kisha akapiga magoti, akaita kwa sauti kuu: Bwana, usiwawekee kosa hili! Alipokwisha kuyasema haya akalala.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28