bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 2
Acts 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 3 →
1
Siku ya Pentekote (Hamsini) ilipotimia, wote walikuwa pamoja mahali palepale pamoja.
2
Mara kukatoka uvumi mbinguni kama wa upepo unaovuma na nguvu, ukaijaza nyumba yote, walimokuwa wakikaa.
3
Tena zikaonekana ndimi zilizogawanyika kama za moto, zikawakalia kila mmoja wao.
4
Wote wakajazwa Roho takatifu, wakaanza kusema kwa misemo mingine, kama Roho alivyowapa, watamke.
5
Mle Yerusalemu walikuwamo wakikaa Wayuda wenye kumcha Mungu wa kila taifa lililoko chini ya mbingu.
6
Ule mvumo uliposikilika, watu wengi wakakusanyika, wakashangaa, kwani kila mtu aliwasikia, wakisema msemo wake yeye.
7
Wakastuka na kustaajabu wakisema: Kumbe hawa wote wanaosema sio Wagalilea!
8
Tena inakuwaje, sisi kila mtu tukiisikia misemo ya kwetu sisi, tuliyozaliwa nayo?
9
Sisi Waparti na Wamedi na Waelamu, nasi tunaokaa Mesopotamia na Yudea na Kapadokia, Ponto na Asia,
10
Furigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia zinazoelekea Kirene, sisi Waroma tunaokaa ugenini huku,
11
sisi tulio Wayuda nasi tulio wafuasi, Wakreta na Waarabu, twawasikia hawa, wakiyatangaza makuu yake Mungu kwa ndimi zetu!
12
Wakastaajabu wote wakipotelewa nayo, wakaulizana wao kwa wao: Jambo hili litakwenda kuwaje?
13
Lakini wengine wakafyoza wakisema: Wamelewa mvinyo mbichi!*
14
Ndipo, Petero alipoinuka pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake akawaambia: Nyie waume Wayuda nanyi nyote mnaokaa Yerusalemu, jambo hili sharti litambulike kwenu, mpate kuyasikiliza maneno yangu!
15
Kwani hawa hawakulewa, kama ninyi mnavyowawazia, maana sasa ni saa tatu ya mchana.
16
Lakini hili ndilo lililosemwa na mfumbuaji Yoeli, ya kuwa
17
Mungu anasema: Siku za mwisho ndipo, itakapokuwa, niwamiminie Roho yangu wote wenye miili ya kimtu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike watasema na kufumbua, nao vijana wenu wataona maono; nao wazee wenu wataoteshwa ndoto.
18
Nao walio watumwa wangu waume na wake nitawamiminia Roho yangu siku zilezile, nao watasema na kufumbua.
19
Nami nitafanya vioja juu mbinguni na vielekezo chini katika nchi, vyenye damu na moto na moshimoshi.
20
Jua litageuka, liwe giza, nao mwezi utageuka, uwe damu, mbele ya kutimia kwake ile siku ya Bwana iliyo kubwa, wanayoingoja wote.
21
Tena itakuwa, kila atakayelitambikia Jina la Bwana, ataokoka.
22
Enyi waume wa Kiisiraeli, yasikilizeni maneno haya! Yesu wa Nasareti alikuwa amejulikana, kwamba ametoka kwa Mungu hapo alipokuja kwenu na kufanya vya nguvu na vioja na vielekezo, tena ni Mungu aliyempa kuvifanya machoni penu, kama mnavyojua wenyewe.
23
Kwa kuwa Mungu alikuwa amempatia kazi na kumkatia mpaka kwa vile, anavyovijua vyote, vikiwa havijatimia bado, kwa hiyo ametolewa, mkampata mikononi mwa wapotovu, mkamwua na kumwamba msalabani.
24
Lakini Mungu akamfufua na kuufungua uchungu wa kufa, kwa sababu haikuwezekana, ashikwe kuzimuni.
25
Kwani Dawidi anamsema: Nalimwona Bwana mbele yangu kila, nilipokuwa, kwani yuko kuumeni kwangu, nisitikisike.
26
Kwa hiyo moyo wangu hufurahi, nao ulimi wangu hushangilia; hata mwili wangu utatulia kwa kuwa na kingojeo.
27
Kwani hutaiacha roho yangu, ipotee kuzimuni, wala hutamtoa akuchaye, apate kuoza kaburini.
28
Unanitambulisha njia ziendazo penye uzima, utanijaza furaha zilizopo usoni pako.
29
Waume ndugu zangu, mnipe ruhusa, niseme kwenu waziwazi: Dawidi aliye babu yetu mkuu alikufa, akazikwa, nalo kaburi lake liko kwetu hata siku hii ya leo.
30
Yeye kwa sababu alikuwa mfumbuaji, akajua, ya kuwa Mungu amemwapia kiapo, kwamba atatawalisha kitini pake mmoja aliye mzao wa kiunoni mwake.
31
Hayo aliyaona mbele, yakingali nyuma bado, akayasema na kuuelekea ufufuko wake Kristo, kwani hakuachwa kuzimuni, wala mwili wake haukupata kuoza.
32
Huyo Yesu Mungu amemfufua, nasi sote tu mashahidi wake.
33
Naye alipokwisha kupazwa juu, akae kuumeni kwa Mungu, akapata ruhusa kwa Baba yake kukitimiza kiagio cha Roho Mtakatifu, akaimimina yiyo hiyo, ninyi mnayoiona, tena mnayoisikia.
34
Kwani Dawidi hakupaa mbinguni, lakini anasema mwenyewe:
35
Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu, mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
36
Kwa hiyo wote walio wa mlango wa Israeli watambue kweli: Huyo Yesu, mliyemwamba msalabani ninyi, Mungu amemfanya, awe Bwana na Kristo!
37
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyoni, wakamwambia Petero na mitume wengine: Waume ndugu zetu, tufanyeje?
38
Petero akawajibu: Juteni, kila mmoja abatiziwe Jina lake Yesu Kristo, mwondolewe makosa yenu! Nanyi mkipate kipaji cha Roho Mtakatifu!
39
Kwani kiagio kile ni chenu ninyi na cha watoto wenu nacho chao wote walioko mbali, Bwana Mungu wetu atakaowaita, wamjie.
40
Sharti mwokolewe katika kizazi hiki kipotovu!
41
Basi, waliolipokea neno lake, wakabatizwa; hivyo siku ile waligeuzwa kuwa wanafunzi watu wapata 3000.
42
Wakaongozana na kuyashika mafundisho ya mitume, wakafanya bia ya kumegeana mkate na kuombeana kwa Mungu.
43
Wote wakaingiwa na woga mioyoni mwao, kwani vioja na vielekezo vilivyofanywa na mitume vilikuwa vingi.
44
Wao wote waliomtegemea Bwana walikuwa pamoja, navyo vyote wakavifanyia bia.
45
Wakauza mali zao navyo vyote, walivyokuwa navyo, wakavigawia wote, kila mtu apate, kama alivyokosa.
46
Kwa sababu mioyo yao ilikuwa mmoja tu, walikuwa pamoja kila siku hapo Patakatifu, wakamegeana mkate nyumba kwa nyumba wakipokea vyakula na kushangilia katika mioyo yao iliyowang'aa.
47
Wakamsifu Mungu, wakawapendeza watu wote. Naye Bwana akawaongeza kila siku na kutia papo hapo wenye kuokoka.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28