bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 3
Acts 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 4 →
1
*Petero na Yohana wakapanda kwenda Patakatifu saa tisa, watu walipoombea.
2
Kulikuwa na mtu aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake; naye huchukuliwa, awekwe kila siku karibu ya mlango wa Patakatifu unaoitwa Mzuri, aombe sadaka kwao wanaoingia Patakatifu.
3
Alipomwona Petero na Yohana, wakitaka kupaingia Patakatifu, akataka kupewa sadaka nao.
4
Lakini Petero akamkazia macho pamoja na Yohana, akasema: Tutazame sisi!
5
Alipowatumbulia macho akingoja, watakachompa,
6
Petero akasema: Fedha na dhahabu sinazo, lakini nilicho nacho, nitakupa. Katika Jina la Yesu Kristo wa Nasareti inuka, uende!
7
Kisha akamshika mkono wa kuume, akamwinua. Papo hapo miguu yake na fundo zake zikapata nguvu,
8
akaruka, akasimama, akaenda, akapaingia Patakatifu pamoja nao akizunguka na kurukaruka na kumsifu Mungu.
9
Watu wote walipomwona, anavyozunguka na kumsifu Mungu,
10
wakamtambua, ya kuwa huyu ndiye aliyekaa na kuomba sadaka karibu ya Mlango Mzuri wa Patakatifu. Wote wakashangaa mno na kuyastukia yale yaliyompata.
11
Aliposhikamana na Petero na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika ukumbi unaoitwa wa Salomo kwa kushangaa.
12
Petero alipowaona akawaambia wale watu: Waume Waisiraeli, haya mnayashangaaje? Nasi mnatutumbualiaje macho, kama ni nguvu yetu sisi, au kama ni hivyo, tunavyomcha Mungu, vinavyomwendesha huyu?
13
Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu wa kele, amemtukuza mtoto wake Yesu, ninyi mliyemtoa na kumkana mbele ya Pilato, alipokata shauri, kwamba afunguliwe.
14
Lakini ninyi mkamkana aliyekuwa mtakatifu na mwongofu, mkataka kupewa aliyekuwa mwuaji,
15
mwenye kuwaongoza uzimani mkamwua. Lakini Mungu amemfufua katika wafu, nasi ndio mashahidi.
16
Tena kwa hivyo, huyu alivyolitegemea Jina lake, hilo Jina lake limemtia nguvu huyu, mnayemwona na kumjua. Kweli hivyo, alivyolitegemea kwa kutiwa nguvu nalo, ndivyo vilivyompa huu uzima wote, mnaouona ninyi nyote.*
17
Sasa, ndugu zangu, ninajua, ya kuwa mliyafanya pasipo kujua maana, kama wakubwa wenu nao.
18
Lakini hivyo ndivyo, Mungu alivyoyatimiza, aliyoyatangaza kale kwa vinywa vya wafumbuaji wote kwamba: Kristo wake atateswa.
19
Kwa hiyo juteni na kugeuka, makosa yenu yafutwe, yawatoke!
20
Ndipo, zitakapowafikia nazo siku za kupoea usoni pa Bwana, tena ndipo, atakapopata kumtuma Kristo Yesu, mliyepewa kwanza.
21
Ndiye, aliyempasa kuutwaa ufalme wa mbingu, mpaka siku zifike, vitu vyote vitakaporudishiwa upya, kama Mungu alivyosema hata kale kwa vinywa vya wafumbuaji wake watakatifu.
22
Mose alisema: Miongoni mwa ndugu zenu Bwana Mungu atawainulia mfumbuaji atakayelingana na mimi, nanyi sharti mmsikie yote, atakayowaambia!
23
Lakini itakuwa, kila mtu atakayekataa kumsikia yule mfumbuaji ataangamizwa, atengwe kabisa nao watu wa kwetu.
24
Nao wafumbuaji wote toka kwa Samueli na wale waliofuata, wo wote waliosema, wamepiga mbiu za siku hizo.
25
Ninyi m wana wao wafumbuaji, tena m wana wa Agano, Mungu aliloliagana na baba zenu alipomwambia Aburahamu: Katika uzao wako ndimo, mataifa yote ya nchi yatakamobarikiwa.
26
Ninyi m wa kwanza, Mungu aliowafufulia mtoto wake na kumtuma, awabariki, mgeuke kila mmoja mkiyaepuka mabaya yenu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28