bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 23
Acts 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 24 →
1
Paulo alipokwisha kuwakazia macho hao wakuu wa barazani, akasema: Waume ndugu, mimi mpaka siku hii ya leo nimekuwapo machoni pa Mungu, kwa hiyo moyo umening'aa wote.
2
Mtambikaji mkuu Anania alipowaagiza waliosimama hapo, alipokuwa, wampige kinywani,
3
ndipo, Paulo alipomwambia: Mungu atakupiga wewe, ukuta wenye uzuri wa kupakwa tu! Wewe unakaa kunihukumu, kama yanavyolingana na Maonyo, tena unayabeza Maonyo kwa kuagiza, nipigwe?
4
Nao waliosimama hapo waliposema: Unamtukana mtambikaji mkuu wa Mungu?
5
Paulo akasema: Ndugu zangu, sikumjua, ya kuwa ndiye mtambikaji mkuu, kwani imeandikwa: Mtawala ukoo wako usimwambia maovu!
6
Paulo alipowatambua, ya kuwa fungu ni Masadukeo, fungu ni Mafariseo, akapaza sauti mbele yao wakuu: Waume ndugu, mimi ni Fariseo, mwana wa Fariseo: ninasutwa hivyo, tunavyoungojea ufufuko wa wafu.
7
Aliposema hivi, Mafariseo na Msadukeo wakainukiana, nao wengi wakajitenga.
8
Kwani Masadukeo hukana ya kwamba: Hakuna ufufuko, hakuna malaika, hakuna roho. Lakini Mafariseo huungama kwamba: Yote yapo.
9
Yakawa makelele makubwa; palikuwa na waandishi waliokuwa wa upande wa Mafariseo, wakainuka, wakabishana wakisema: Mtu huyu hatumwoni kiovu cho chote. Kama yuko roho au malaika aliyesema naye, hatutaki kumgombeza Mungu.
10
Lakini matata yalipokaza, mkuu wa kikosi akaogopa, Paulo asiraruliwe nao akaagiza, askari washuke, wampokonye katikati yao, wampeleke bomani.
11
Usiku uliofuata Bwana akamjia na kusimama hapo, alipokuwa, akasema: Tulia! kwani kama ulivyoyashuhudia mambo yangu hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kuyashuhudia hata Roma.
12
Kulipokucha, Wayuda wakakusanyika, wakaapizana, kwamba wasile, wala wasinywe, mpaka wamwue Paulo;
13
nao walioapizana hivyo walikuwa wengi kupita 40.
14
Kisha wakaendea watambikaji wakuu na wazee, wakasema: Tumeapizana kwa kiapo ya kwamba: Tusionje kitu, mpaka tumwue Paulo!
15
Sasa ninyi wakuu nyote, mmweleze mkuu wa kikosi, amshushe kesho kwenu, kwamba mnataka kutambua kwa welekevu, mambo yake yalivyo. Lakini sisi tuko tayari kumwua, akiwa hajawafikia ninyi.
16
Mwana wa umbu lake Paulo alipoisikia njama hiyo, akaja, akaingia bomani, akamjulisha Paulo.
17
Ndipo, Paulo alipoita bwana askari mmoja, akasema: Umpeleke kijana huyu kwa mkuu wa kikosi! Kwani yuko na habari ya kumpasha.
18
Yule akamchukua akampeleka kwa mkuu wa kikosi, akasema: Mfungwa Paulo umeniita, akataka, nimpeleke kijana huyu kwako, yuko na neno la kukuambia.
19
Mkuu wa kikosi akamshika mkono, akaondoka naye kwenda penye njama, akamwuliza: Una habari gani ya kunipasha?
20
Akasema: Wayuda wamepatana kukuomba wewe, umshushe Paulo kesho kwenye wakuu, kwamba wanataka kumwuliza kwa welekevu, mambo yake yalivyo.
21
Basi, wewe usiwaitikie! Kwani watu wao wengi kupita 40 wanamwotea; hao wameapizana kwa kiapo, ya kwamba wasile, wala wasinywe, mpaka wamwue yeye. Sasa wako tayari na kuongoja, uwaitikie wewe.
22
Mkuu wa kikosi akamwaga yule kijana, akamkataza kwamba: Usimwambie mtu, ya kuwa umenieleza haya!
23
Akaita wabwana askari wawili, akasema: Tengenezeni askari 200, waende mpaka Kesaria, na askari wapanda frasi 70 na wenye mikuki 200, wawe tayari saa tatu ya usiku!
24
Tandikeni na nyumbu za kumpandisha Paulo, wampeleke vema mpaka kwa Feliki aliye mtawala nchi!
25
Akamwandikia barua yenye maneno haya:
26
Mimi Klaudio Lisia nakuamkia wewe, mtawala nchi Feliki uliye na nguvu nyingi, salamu!
27
Mtu huyu alikamatwa na Wayuda; nao walipotaka kumwua, nikaenda na kikosi cha askari, nikamwokoa, kwani nalisikia, ya kuwa ni Mroma.
28
Nami kwa hivyo, nilivyotaka kutambua, waliyomsuta, nikamshusha na kumweka barazani kwao wakuu wao.
29
Nikaona, ya kuwa anasutiwa mashindano ya Maonyo yao, lakini hakuna neno linalompasa kuuawa na kufungwa tu.
30
Tena nilipoambiwa, ya kuwa mtu huyu anatunduiliwa, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza hata wenye kumsuta, waseme mbele yako, wanayomsuta.
31
Wale askari wakamchukua Paulo, kama walivyoagizwa, wakampeleka usiku mpaka mji wa Antipatiri.
32
Kesho yake wakawaacha wale wapanda frasi, waondoke pamoja naye, nao wenyewe wakarudi bomani.
33
Wale walipofika Kesaria wakampa mtawala nchi ile barua, wakamsimamisha Paulo mbele yake.
34
Alipokwisha kuisoma hiyo barua, akamwuliza upande wa nchi, aliotoka. Aliposikia, ya kuwa ni mtu wa Kilikia,
35
akasema: Nitakuuliza na kukusikiliza, wewe kukusuta watakapofika; kisha akaagiza, alindwe katika boma la Herode.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28