bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 4
Acts 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 5 →
1
*Walipokuwa wakisema na watu, wakawajia watambikaji na mlinda Patakatifu na Masadukeo.
2
Kwani walikasirika, kwa sababu walifundisha watu na kuwapigia mbiu ya kwamba: Wafu watafufuka kwa hivyo, Yesu alivyofufuka.
3
Kwa hiyo wakawakamata, wakawatia kifungoni, mpaka asubuhi yake, kwani ilikuwa jioni.
4
Lakini waliolisikia lile neno wengi wakalitegemea, waume tu wakawa kama 5000.
5
Kulipokucha, wakakusanyika Yerusalemu wakubwa wao na wazee na waandishi
6
na mtambikaji mkuu Ana na Kayafa na Yohana na Alekisandro nao wote waliokuwa wa ukoo wa mtambikaji mkuu.
7
Kisha wakawasimamisha katikati, wakawauliza: Hilo ninyi mmelifanya kwa nguvu ya nani au kwa jina la nani?
8
Ndipo, Petero alipojaa Roho takatifu, akawaambia: Nyie wakubwa wa watu wa kwetu na wazee,
9
kwa kuwa mtu mwenye kilema amefanyiziwa vizuri, sisi twaulizwaulizwa leo: Huyu amepona kwa nguvu ya nani?
10
Tambueni ninyi nyote na ukoo wote wa Isiraeli: Nguvu ya Jina la Yesu Kristo wa Nasareti, mliyemwamba msalabani ninyi, Mungu aliyemfufua katika wafu, hiyo nguvu yake ndiyo inayomsimamisha huyu mtu machoni penu, yuko mzima!
11
Huyu ndiye lile jiwe lililokataliwa na ninyi waashi, lakini limekuwa jiwe la pembeni.
12
Tena hapana pengine panapopatikana wokovu, wala hapana Jina jingine chini ya mbingu, sisi watu tulilopewa, tuokoke nalo.*
13
Walipomwona Petero na Yohana, walivyosema pasipo woga, tena ilipowaelea, ya kuwa ni watu wasiofundishwa wala Maandiko wala ujuzi wo wote, wakastaajabu, wakawatambua, ya kuwa walikuwa pamoja na Yesu.
14
Lakini walipomtazama yule mtu aliyeponywa, anavyosimama pamoja nao, hawakuwa na neno la kujibu.
15
Wakawaagiza, watoke barazani kwao wakuu kwenda nje, wakala njama wao kwa wao
16
wakisema: Tuwafanyieje watu hawa? Kwani wamefanya kielekezo cha waziwazi kinachotambulikana kwa watu wote wakaao Yerusalemu; nasi hatuwezi kukikana.
17
Lakini kusudi isipate kuenea po pote kwa watu, tuwatishe, wasimwambie tena mtu ye yote jambo lo lote la Jina hilo.
18
Kisha wakawaita, wakawakemea kabisa, wasiseme tena na kufundisha mambo ya Jina la Yesu.
19
Lakini Petero na Yohana wakajibu wakiwaambia: Likateni shauri hilo wenyewe, kama inaongoka mbele ya Mungu, kuwasikia ninyi kuliko Mungu!
20
Kwani sisi hatuwezi kuacha, tusiyaseme, tuliyoyaona nayo tuliyoyasikia.
21
Lakini wakawatisha sana, wakawafungua, kwa sababu hawakuwaonea neno la kuwaumiza, kwa kuwa waliwaogopa watu. Kwani wote walimtukuza Mungu kwa yale yaliyofanyika,
22
kwani yule mtu aliyefanyiwa kielekezo hivyo cha kuponywa, miaka yake ilipita 40.
23
Walipokwisha funguliwa wakaenda kwa watu wao, wakawasimulia yote, watambikaji wakuu na wazee waliyowaambia.
24
Walipoyasikia, ndipo, wote pamoja walipompalizia Mungu sauti na kusema: Bwana, wewe ndiwe uliyezifanya mbingu na nchi na bahari navyo vyote vilivyomo!
25
Uliisemesha Roho takatifu kwa kinywa cha mtoto wako Dawidi: Mbona wamizimu hupiga makelele?
26
Mbona makabila ya watu huwaza mambo yaliyo ya bure? Wafalme wa nchi hushikana mioyo? wakuu nao hula njama wakikaa pamoja, wamkatae Bwana na Kristo wake.
27
Hii ni kweli, kwani walikusanyika mjini humu, wamkamate mtoto wako mtakatifu Yesu, uliyempaka mafuta; akina Herode na Pontio Pilato walipatana na wamizimu na watu wa Isiraeli,
28
wayafanye yote, uliyomtakia kale kwa mkono wako na kwa mapenzi yako, kwamba yatimie papo hapo.
29
Na sasa, Bwana, yatazame matisho yao! Wape watumwa wako waliseme Neno lako waziwazi pasipo woga hata kidogo!
30
Unyoshe mkono, uponye watu na kufanya vielekezo na vioja kwa Jina la mtoto wako mtakatifu Yesu!
31
Walipoomba hivyo, hapo, walipokuwa wamekusanyika, pakatetemeka, wakajazwa wote Roho Mtakatifu, wakalisema Neno la Mungu waziwazi pasipo woga.
32
*Nao wigi wa watu waliokuwa wamemtegemea Bwana, mioyo yao nazo roho zao zilikuwa moja; tena hakuwako hata mmoja aliyezitumia mali zake, kama ni zake mwenyewe, lakini vyote walivitumia bia.
33
Nao mitume wakaushuhudia ufufuko wa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi, magawio makuu ya Mungu yakiwakalia wao wote.
34
Kwa hiyo hakupatikana kwao aliyekosa vitu, alivyopaswa navyo. Kwani wote waliokuwa wenye mashamba au nyumba waliziuza,
35
wakaziweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa, kama alivyokosa.*
36
Kulikuwa na Mlawi aliyetoka Kipuro, jina lake Yosefu, aliyeitwa na mitume Barnaba, maana yake Mwana wa Tulizo,
37
naye alikuwa na shamba, akaliuza, akazileta fedha, akaziweka miguuni pa mitume.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28