bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 11
Acts 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 12 →
1
Mitume na ndugu waliokuwako Yudea wakasikia, ya kuwa hata wamizimu wamelipokea Neno la Mungu.
2
Petero alipopanda kwenda Yerusalemu, waliotahiriwa wakabishana naye wakisema:
3
Umeingia mwa watu wasiotahiriwa, ukala pamoja nao.
4
Petero akaanza kuwaeleza yote, yalivyofuatana, akisema:
5
Mimi nilipokuwa katika mji wa Yope nikimwomba Mungu, nikaingiwa na kituko kwa kuona njozi: chombo kinachofanana na guo kubwa linatelemshwa chini toka mbinguni likishikwa kwa pembe zake nne likaja mpaka hapo, nilipokuwa.
6
Nami nilipochungulia mle nikitazama, nikaona, mna nyama wenye miguu minne wa nchini nao nyama wa mwituni nao watambao nao ndege wa angani;
7
kisha nikasikia sauti ya kuniambia: Inuka, Petero, uchinje, ule!
8
Ndipo, niliposema: Hapana, Bwana, kwani cho chote kilicho chenye mwiko au kisichotakata hakijaingia bado kinywani mwangu.
9
Lakini sauti ikanijibu tena toka mbinguni: Mungu alivyovitakasa, wewe usivizie!
10
Vikafanyika hivyo mara tatu, kisha yote yakavutwa tena na kupazwa mbinguni.
11
Mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba, nilimokuwa, walitumwa kwangu toka Kesaria.
12
Naye Roho akaniambia, niende pamoja nao pasipo mashaka; hata hawa ndugu sita wakafuatana nami, tukaingia nyumbani mwake yule mtu.
13
Huyo akatusimulia, alivyoona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kusema: Tume watu, waende Yope, wamwite Simoni anayeitwa Petero!
14
Ndiye atakayekuambia maneno yatakayokuokoa wewe nao wote wa nyumbani mwako.
15
Nami nilipoanza kusema, Roho Mtakatifu akawaguia, kama alivyotuguia hata sisi hapo kwanza.
16
Ndipo, nilipolikumbuka neno la Bwana, alilolisema: Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatiza katika Roho takatifu.
17
Mungu alipowapa kipaji kilekile, tulichokipata na sisi tuliomtegemea Bwana Yesu Kristo, hapo mimi nilikuwa na nguvu gani, niweza kumzuia Mungu?
18
Walipoyasikia haya wakanyamaza kimya, wakamtukuza Mungu wakisema: Kumbe hata wamizimu Mungu amewapa majuto, nao wapate uzima!
19
Wale waliotawanyika kwa sababu ya maumivu, waliyopatwa nayo, Stefano alipouawa, wakazunguka, wakafika mpaka Ufoniki na Kipuro na Antiokia, wasimwambie mtu hilo Neno pasipo Wayuda peke yao.
20
Lakini wengine wao walikuwa watu wa Kipuro nao wa Kirene. Hao walipofika Antiokia, wakawapigia hata Wagriki mbiu njema ya Bwana Yesu.
21
Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, wakawa wengi waliomgeukia Bwana kwa kumtegemea.
22
Hilo neno lao liliposikilika masikioni pa wateule waliokuwa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba, aende Antiokia.
23
Naye alipofika na kuviona vipaji, Mungu alivyowagawia, akafurahi, akawahimiza wote, wakaze mioyo kushikamana na Bwana.
24
Kwa kuwa mtu mwema aliyejaa Roho takatifu alizidi kumtegemea Mungu; kwa hiyo kikundi kizima cha watu kikapelekwa kwa Bwana.
25
Kisha akatoka kwenda Tarso kumtafuta Sauli;
26
alipomwona akampeleka Antiokia. Kisha wakakaa nao wateule wa hapo hata mwaka mzima, wakafundisha watu wengi; napo hapo Antiokia ndipo, wanafunzi walipoanza kuitwa Wakristo.
27
Ikawa siku zile, wakashuka wafumbuaji toka Yerusalemu kufika Antiokia.
28
Mmoja wao, jina lake Agabo, akainuka kwa kuongozwa na Roho, akaonyesha, kwamba itakuwa njaa kubwa ulimwenguni mote; nayo ikawako siku za Klaudio.
29
Ndipo, wanafunzi walipopatana, kwamba kila mtu kwa hivyo, alivyofanikiwa, atoe mali, zipelekwe za kuwatumikia ndugu waliokaa Yudea.
30
Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28