bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 28
Acts 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
1
Tulipokwisha kuokoka, ndipo, tulipoambiwa, ya kuwa kisiwa kinaitwa Melite.
2
Wenyeji wa huko wakatutunza kwa upendo usiopatikana kila siku: wakawasha moto, wakatupokea mwao sisi sote kwa ajili ya mvua iliyotunyea na kwa ajili ya baridi.
3
Paulo alipodondoa mzigo wa vijiti kuvitia motoni, mkatoka humo nyoka kwa ajili ya moto, akamzingazinga mkono.
4
Wenyeji walipomwona yule mdudu, alivyomng'ang'ania mkononi pake, wakasemezana wao kwa wao: Mtu huyu hakosi kuwa mwuaji, kwani ingawa ameokoka baharini, tena lipizi halimwachi, awepo.
5
Alipomkung'uta yule mdudu motoni, hakuna kiovu tena kilichompata.
6
Lakini wale walimtunduia na kungoja, avimbe au aanguke chini akifa papo hapo. Lakini walipongoja sana na kuona, ya kuwa hapati kibaya cho chote, wakageuka na kusema: Yeye ni mungu!
7
Lakini hapo karibu palikuwa na kiunga cha mkuu wa kisiwa, jina lake Pubulio. Huyu akatupokea mwake siku tatu, akatutunza na kutupendeza.
8
Baba yake Pubulio alipoingiwa na homa na kuhara damu, Paulo akaingia mwake, akamwombea, akambandikia mikono, akamponya.
9
Hayo yalipokwisha kufanyika, nao wengine wa kisiwa kile waliokuwa wenye magonjwa wakamjia, wakaponywa,
10
wakatutukuza kwa matukuzo mengi. Nasi tulipoingia chomboni tena, wakatupakilia navyo vyote vya kutumia njiani.
11
Miezi mitatu ilipopita, tukaondoka tukijipakia chomboni kilichotoka Alekisandria; kilikuwa kimezimaliza siku za kipupwe pale kisiwani; kilikuwa chenye chapa cha mapacha.
12
Tulipofika Sirakuse, tukakaa huko siku tatu.
13
Kutoka huko tukazunguka, tukafika Regio. Tulipongoja siku moja, kukavuma upepo wa kusini, tukafika Puteoli kwa mwendo wa siku mbili.
14
Huko tukakuta ndugu, tukabembelezwa nao, tukae kwao siku saba. Ndivyo, tulivyokwenda kufika Roma.
15
Ndugu wa huko walipovisikia wakaja kukutana na sisi, wakatujia mpaka Apioforo, wengine mpaka Tiretaberne. Paulo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangamka.
16
Tulipoingia Roma, bwana askari akampa mwenzake mkubwa wafungwa, lakini Paulo akapewa ruhusa ya kukaa, alipotaka, pamoja na askari aliyemlinda.
17
Siku tatu zilipopita, akawakusanya wakubwa wa Wayuda. Walipokusanyika, akawaambia: Waume ndugu, mimi sikuwakosea wao wa ukoo wetu wala mazoea ya baba zetu. Nimefungwa huko Yerusalemu, nikatiwa mikononi mwa Waroma.
18
Nao waliponiulizauliza wakataka kunifungua, kwa sababu kwangu hakuna neno linalopasa, niuawe.
19
Lakini Wayuda walipobisha, nikashurutishwa kutaka kuhukumiwa na Kaisari, lakini hapo siko kwamba: Niwasute walio wa taifa langu.
20
Kwa sababu hii nimewaita, niwaone ninyi, tusemeane. Kwani kingojeo cha Waisiraeli ndicho, nilichofungiwa mnyororo huu.
21
Nao wakamwambia: Sisi kwa ajili yako hatukupata barua toka Yudea, wala hakuna ndugu aliyetujia na kutusimulia mambo yako, wala kusema kibaya, ulichokifanya.
22
Lakini twataka kusikia kwako mwenyewe mawazo yako, kwani chama hiki tumekijua, nako kwetu kinatambulika, ya kuwa kinabishiwa po pote.
23
Walipokwisha kuagana naye siku, wengi wakamjia huko, alikofikia, akawaeleza tangu asubuhi mpaka jioni akiushuhudia ufalme wa Mungu; tena akajaribu kuwashinda kwa ajili yake Yesu na kuwafumbulia maonyo ya Mose na maneno ya wafumbuaji wengine wakayaitikia maneno yake, wengine wakakataa kuyategemea.
24
Wengine wakayaitikia maneno yake, wengine wakakataa kuyategemea.
25
Hivyo wakashindwa kupatana wao kwa wao, wakajiendea zao. Ndipo, Paulo aliposema neno kwa kinywa cha mfumbuaji Yesaya:
26
Nenda kwao wa ukoo huu, useme: Kusikia mtasikia, lakini hamtajua maana; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
27
Kwani mioyo yao walio ukoo huu imeshupazwa, wasisikie kwa masikio yao yaliyo mazito, nayo macho yao wameyasinziza, wasije wakaona kwa macho yao, au wakasikia kwa masikio yao, au wakajua maana kwa mioyo yao, wakanigeukia, nikawaponya.
28
Basi, ijulikane kwenu ninyi ya kwamba: Wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwenye wamizimu; hao ndio watakaousikia.
29
Alipovisema hivyo, Wayuda walikwenda wakibishana sana wao kwa wao.
30
Paulo akakaa miaka miwili mzima katika nyumba yake, aliyokuwa ameipanga, akawapokea wote walioingia kwake,
31
akautangaza ufalme wa Mungu, akayafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo pasipo woga na pasipo kuzuiliwa na mtu.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28