bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 15
Acts 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 16 →
1
Kulikuwa na watu waliotelemka toka Yudea, wakaja huko, wakawafundisha ndugu kwamba: Hamwezi kuokoka msipotahiriwa, kama Mose alivyotuzoeza.
2
Ikawa, Paulo na Barnaba wakabishana nao kabisa na kushindana sana. Kisha wakamwagiza Paulo na Barnaba na wenzao wengine, wapande kwenda Yerusalemu kwao mitume na wazee kwa ajili ya mshindano huu.
3
Wakasindikizwa na wateule, wakapita Ufoniki na Samaria, wakaeleza Po pote, wamizimu walivyogeuka; hivyo wakawafurahisha sana ndugu wote.
4
Walipofika Yerusalemu wakapokelewa nao wateule na mitume na wazee, wakayaeleza yote, Mungu aliyoyafanya kwa kuwa nao.
5
Pakainuka waliokuwa wa chama cha Mafariseo, lakini nao walikuwa wenye kumtegemea Bwana, wakasema: Sharti watahiriwe! Sharti waagizwe kuyashika Maonyo ya Mose!
6
Mitume na wazee wakakusanyika, walitazame neno hilo.
7
Mashindano yalipokuwa mengi, Petero akainuka, akawaambia: Waume ndugu, ninyi mnajua, ya kuwa siku zilizopita huku kwenu Mungu alikichagua kinywa changu, wamizimu wakisikie, kinavyowapigia hiyo mbiu njema, waje kuitegemea.
8
Naye Mungu mwenye kuitambua mioyo akawapokea wamizimu alipowapa Roho Mtakatifu, kama alivyotupa na sisi.
9
Tena hakuna, asichowalinganisha na sisi, maana nao amewang'aza mioyo kwa vile, walivyomtegemea.
10
Sasa mwamjaribiaje Mungu mkiwatwisha wanafunzi mzigo, ambao baba zetu hawakuweza kuuchukua, uliotushinda nasi?
11
Lakini tunayategemea, ya kuwa tutaokolewa kwa kugawiwa na Bwana Yesu, sawasawa kama wale nao.
12
Basi, mkutano wote ukanyamaza, wakamsikiliza Barnaba na Paulo, wakivisimulia vielekezo na vioja vyote, Mungu alivyovifanya kwa mikono yao katika wamizimu.
13
Waliponyamaza tena, Yakobo akajibu akisema: Waume ndugu, mnisikilize!
14
Simoni amesimulia, Mungu alivyoanza kuwachagua wamizimu, alipatie Jina lake kundi la watu humo namo.
15
Nayo maneno ya Wafumbuaji huelekeza papo hapo, kama ilivyoandikwa kwamba:
16
Hayo yakiisha, nitarudi, nikijenge tena kibanda cha Dawidi kilichoanguka; hapo palipojenguka nitapajenga tena, nipate kukisimamisha tena,
17
maana watu waliosalia wote wapate kumtafuta Bwana pamoja na wamizimu wote waliotangaziwa Jina langu. Ndivyo, asemavyo Bwana anayeyafanya haya.
18
Yanatambulikana toka kale.
19
Kwa hiyo mimi naona: Wanaotoka kwa wamizimu na kumgeukia Mungu tusiwachukuze mizigo isiyofaa,
20
ila tuwaandikie kwamba: Miiko ni hii tu: Kutambikia mizimu, maana huchafua moyo wa mtu, tena ugoni, tena nyamafu, tena damu.
21
Kwani toka kale hata sasa Mose anao mijini mote wanaoyatangaza maneno yake, tena katika nyumba za kuombea yanasomwa kila siku ya mapumziko.
22
Ndipo, mitume na wazee walipopatana na wateule wote kuchagua wenzao wengineo na kuwatuma kwenda Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Wakamchagua Yuda anayeitwa Barsaba na Sila, waliojua kuongoza ndugu.
23
Wakaandika barua, waipeleke mikononi mwao, ni ya kwamba: Sisi mitume na wazee tunawaamkia kindugu ninyi ndugu zetu huko Antiokia na Ushami na Kilikia mliotoka kwa wamizimu.
24
Tumesikia, ya kuwa wengine watu, tusiowaagiza neno, wamewahangaisha kwa maneno ya kuwatia wasiwasi mioyoni mwenu.
25
Tukakusanyika kwa hivyo, tulivyo na moyo mmoja, tukapatana kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wenzetu akina Barnaba na Paulo, tunawapenda,
26
kwani ni watu waliojitoka wenyewe kwa ajili ya Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
27
Basi, tumemtuma Yuda na Sila, nao watawaelezea kwa vinywa maneno yaya haya.
28
Kwani sisi na Roho Mtakatifu tumepatana, tusiwatwike mzigo kuliko yaleyale yanayofaa,
29
mshike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni. Mkijikataza mambo haya mtafanya vema. Kaeni vema! Salamu.
30
Kisha wakasindikizwa, wakatelemka kwenda Antiokia, wakawakusanya wao wote wa hilo kundi, wakawatolea ile barua.
31
Wale walipoisoma wakafurahi kwa ajili ya matulizo.
32
Hata Yuda na Sila waliokuwa wafumbuaji wenyewe wakawatuliza ndugu na kuwaambia mengi, wakawashupaza.
33
Walipokwisha kukaa kitambo walisindikizwa na ndugu kwa hivyo, walivyopatana, warudi kwao waliowatuma.
34
Lakini Sila alipendezwa kukaa huko.
35
Naye Paulo na Barnaba wakakaa Antiokia wakilifundisha Neno la Bwana na kuipiga hiyo mbiu njema pamoja na wenzao wengi.
36
Siku zilipopita, Paulo akamwambia Barnaba: Turudi tena, tuwakague ndugu mijini mote, tulimolitangaza Neno la Bwana!
37
Lakini Barnaba alitaka kumchukua naye Yohana aliyeitwa Marko.
38
Lakini Paulo alidhani, haifai kumchukua aliyewatoroka huko Pamfilia, asifuatane nao kazini.
39
Kwa hiyo wakabishana kwa ukali, hata wakatengana yeye na mwenziwe; Barnaba akamchukua Marko, akaingia chomboni kwenda Kipuro,
40
naye Paulo akamchukua Sila, akaondoka akiombewa na ndugu, Mungu awaongoze kwa upole.
41
Akaipita nchi ya Ushami na Kilikia, akawashupaza wateule.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28