bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 22
Acts 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 23 →
1
Waume mlio ndugu na baba, sikilizeni, ninayojikania sasa mbele yenu!
2
Waliposikia, ya kuwa anasema nao kwa msemo wao wa Kiebureo, wakakaza kunyamaza.
3
Akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda, nimezaliwa Tarso katika nchi ya Kilikia. Nikalelewa humu mjini, nikakaa miguuni pa Gamalieli na kufundishwa Maonyo ya baba zetu kwa uangalifu wote. Nikajipingia kumfanyia Mungu kazi, kama nanyi nyote leo.
4
Njia hiyo nikaifuata, mpaka nikiua watu; waume na wake nikawafunga na kuwatia kifungoni.
5
Hayo hata mtambikaji mkuu na wazee wote watanishuhudia. Kisha nikapewa barua nao za kwenda kwa ndugu walioko Damasko, nako niwafunge wale waliokuwako, niwalete Yerusalemu, wapatilizwe.
6
Lakini nilipokwenda na kufika karibu ya Damasko, ilipokuwa saa sita ya mchana, mara palitoka mwanga mkubwa mbinguni, ukanimulikia pande zote.
7
Nikaanguka chini, nikasikia sauti iliyoniambia: Sauli, Sauli, unanifukuzaje?
8
Nami nilipojibu: Ndiwe nani, Bwana? akaniambia: Mimi ni Yesu wa Nasareti, ambaye unanifukuza wewe.
9
Nao wenzangu, tuliokuwa pamoja, waliuona mwanga, lakini aliyesema nami hawakumsikia sauti yake.
10
Nilipouliza: Nifanyeje, Bwana? Bwana akanijibu: Inuka, uende Damasko! Ndimo, utakamoambiwa yote, uliyoagizwa kuyafanya.
11
Kwa hivyo, nilivyokuwa sioni kwa kumetuka kwake ule mwanga, nikashikwa mkono na wenzangu, nikaingia Damasko.
12
Kulikuwa na mtu, jina lake Anania, ni mwenye kuyashika Maonyo yote, kama wanavyomshuhudia Wayuda wote wanaokaa huko.
13
Huyo akanijia, akasimama mbele yangu, akaniambia: Ndugu yangu Sauli, uwe mwenye kuona! Nami saa ileile nikapata kuona.
14
Kisha akasema: Mungu wa baba zetu amekuchagua huko kale, upate kuyatambua, ayatakayo, umwone naye Mwongofu wake, uisikie na sauti ya kinywa chake mwenyewe,
15
anavyokuambia: Utakuwa shahidi wangu kwa watu wote ukiwaambia, uliyoyaona nayo uliyoyasikia.
16
Sasa unakawilia nini? Inuka, ubatizwe na kuoshwa, makosa yako yakuondoke, ukilitambikia Jina lake!
17
Niliporudi Yerusalemu nikaja kuombea Patakatifu; hapo nikazimia roho,
18
nikamwona, naye akaniambia; Piga mbio, utoke upesi Yerusalemu! Kwani hawatakupokea, ukinishuhudia mimi.
19
Nam nikasema: Bwana, wao wenyewe wanajua, mimi nilivyowafunga waliokutegemea na kuwapiga mo mote nyumbani mwa kuombea.
20
Napo hapo, damu ya shahidi wako Stefano ilipomwagwa, mimi mwenyewe nilikuwa nimesimama hapohapo kwa kupendezwa, nikayalinda mavazi yao wale waliomvua.
21
Naye akaniambia: Enenda tu! Kwani mimi nitakutuma, uende mbali kwa wamizimu.
22
Ndipo, wale waliomsikiliza mpaka neno hili walipopaza sauti wakisema: Mwondoe huyu nchini! Kwani haimpasi kuwapo.
23
Walipopiga kelele hivyo na kuzirarua nguo zao na kutupa uvumbi juu angani,
24
mkuu wa kikosi akaagiza, aingizwe bomani; akasema, wamwulize kwa mapigo, apate kuijua sababu ya kumpigia makelele kama hayo.
25
Walipomfunga kwa mikanda, apigwe, Paulo akamwambia bwana askari aliyesimama hapo: Je? Mko na ruhusa kupiga mtu aliye Mroma, asipohukumiwa kwanza?
26
Bwana askari alipovisikia hivi akamwendea mkuu wa kikosi, akamjulisha akisema: Wataka kufanya nini? Kwani mtu huyu ni Mroma.
27
Mkuu wa kikosi akamwendea, akamwambia: Niambie, wewe u Mroma? Naye akasema: Ndio.
28
Mkuu wa kikosi alipojibu: Mimi huu Uroma nimeununua kwa fedha nyingi, Paulo akasema: Mimi nimezaliwa nao.
29
Papo hapo wale waliotaka kumwuliza kwa mapigo wakamwacha. Naye mkuu wa kikosi akaogopa alipotambua, ya kuwa ni Mroma, kwani yeye alimfunga.
30
Kesho yake alitaka kuyatambua mashtaka ya Wayuda, kama ni ya kweli; kwa hiyo akamfungua, akaagiza, watambikaji wakuu na baraza yote ya wakuu wakusanyike pamoja, akampeleka Paulo chini kwao, akamsimamisha mbele yao.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28