bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 24
Acts 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 25 →
1
Siku tano zilipopita, mtambikaji mkuu Anania akatelemka pamoja nao wazee wengine na msemaji aliyitwa Tertulo, wakamsuta Paulo mbele ya mtawala nchi.
2
Yule alipoitwa, Tertulo akaanza kumsuta akisema: Kwa nguvu yako, bwana Feliki, tunapata kutengemana sana; na kwa utunzaji wako wewe hili taifa letu limetengenezewa mambo mazuri mengi.
3
Hayo yote twayapokea na kukushukuru sana kila siku na kila mahali.
4
Lakini nisikuchokeshe kwa maneno mengi; nakuomba utusikilize kidogo kwa utu wako.
5
Kwani tumemwona mtu huyu kuwa mwangamizi, akiwaletea kondo Wayuda wote waliopo ulimwenguni po pote, tena ni mkubwa wa chama cha Wanasareti.
6
Alipojaribu kupachafua napo Patakatifu, ndipo, tulipomkamata tukitaka kumhukumu kwa Maonyo yetu.
7
Lakini mkuu wa kikosi Lisia akamwondoa na nguvu nyingi mikononi mwetu, akaagiza, wenye kumsuta waende kwako wewe.
8
Hayo yote, tunayomsuta, utaweza kuyatambua mwenyewe ukimwulizauliza.
9
Wayuda nao wakamwitikia wakisema: Hivyo ndivyo, yalivyo.
10
Mtawala nchi alipomkonyeza Paulo, aseme, akajibu: Ninakujua, ya kuwa wewe ndiwe mwamuzi wa hili taifa letu tangu miaka mingi; kwa hiyo nitajikania haya mambo yangu na kuchangamka.
11
Kwani wewe unaweza kutambua, ya kuwa siku, nilizopanda kwenda Yerusalemu kuombea hapo, hazijapita kumi na mbili.
12
Tena hawakuniona hapo Patakatifu, nikiongea na mtu au nikiwachokoza watu, wainukiane, kama ni nyumbani mwa kuombea au mjini pengine.
13
Tena wanayonisuta sasa, hawawezi kuyatokeza kuwa ya kweli mbele yako.
14
Lakini mbele yako naungama waziwazi: Njia ile, wanayoiita ya chama, ndiyo yangu ya kumtumikia Mungu wa baba zetu, nikayategemea yote yaliyoandikwa penye Maonyo na katika vyuo vya Wafumbuaji.
15
Tena liko jambo, ninalolingojea kwa Mungu, nalo ndilo, wanaloliitikia nao hawa wenyewe, la kwamba: Utakuwapo ufufuko wa waongofu na wa wapotovu.
16
Kwa hiyo nami mwenyewe nakaza kuulinda moyo wangu, uwe umeng'aa mbele ya Mungu, hata mbele ya watu katika mambo yote.
17
Mika ilipopita mingi, nikafika kwao wa taifa langu niwapelekee sadaka ya vipaji.
18
Hapo ndipo, waliponiona, nikieuliwa Patakatifu; hawakuniona, nikikusanya watu au nikipiga kelele.
19
Lakini walioniona ndio Wayuda wengine waliotoka Asia; hao ingewapasa kuwapo hapa, wanisute mbele yako, waliyonionea.
20
Nao hawa na waseme wenyewe, kama wameona upotovu kwangu, niliposimama mbele yao wakuu,
21
lisipokuwa neno lile moja, nililolipazia sauti kabisa nikiinuka katikati yao na kusema: Ufufuko wa wafu ndio, ninaohukumiwa leo mbele yenu!
22
Feliki alipoyasikia haya akawakawilisha, kwani alipata kuelewa na mambo ya njia hiyo. Kwa hiyo akasema: Mkuu wa kikosi Lisia atakapotelemka, nitayatambulisha naye mambo yenu.
23
Akamwagiza bwana askari, Paulo alindwe, lakini asifungwe, wala asiwazuie wenziwe kumtumikia au kumjia.
24
Siku zilipopita, Feliki akaja pamoja na mkewe Dirusila aliyekuwa Myuda, akatuma kumwita Paulo, akamsikiliza, akimwonyesha, kumtegemea Kristo Yesu kulivyo.
25
Lakini alipoeleza mambo ya kupata wongofu na ya kuziepuka tamaa na ya hukumu itakayokuwapo, Feliki akaingiwa na woga, akajibu: Sasa hivi jiendee tu!
26
Hapo, nitakapopata mapumziko, nitakuita tena. Vile vile alingojea kupenyezewa fedha na Paulo, amfungue. Kwa hiyo akamwita mara kwa mara, aongee naye.
27
Lakini miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akampokea Feliki kazi yake. Feliki akataka kuwapendelea Wayuda, kwa hiyo akamwacha Paulo kifungoni.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28