bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 6
Acts 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 7 →
1
Siku zile wanafunzi walipozidi kuwa wengi, Wagriki waliwanung'unikia Waebureo, kwani wanawake wajane wa kwao hawakutumikiwa kama wengine na kugawiwa kila siku vilivyowapasa.
2
Hapo wale kumi na wawili wakawakusanya wingi wa wanafunzi, wakasema: Haifai, sisi tukiliacha Neno la Mungu, tutumikie mezani.
3
Ndugu zetu, mkague watu saba wa kwenu wanaojulikana, ya kuwa wamejaa Roho na werevu wa kweli, tuwaweke, walitumikie jambo hilo!
4
Lakini sisi tuishike kazi yetu ya kuomba na kulitumikia Neno.
5
Neno hili likawapendeza wale wote waliokuwako, wakamchagua Stefano aliyekuwa mwenye kumtegemea Bwana kwa moyo wote na mwenye Roho takatifu na Filipo na Porokoro na Nikanoro na Timoni na Parmena na Nikolao aliyekuwa mfuasi wa Kiyuda wa Antiokia.
6
Hawa ndio, waliowasimamisha mbele ya mitume, wakawabandikia mikono wakiwaombea kwa Mungu.
7
Hivyo Neno la Mungu likaendelea, wanafunzi wakapata kuwa wengi sana Yerusalemu, hata watambikaji wengi wakamtegemea Bwana na kumtii.
8
Naye Stefano alikuwa mwenye nguvu nyingi za kumtegemea Bwana, akafanya vioja na vielekezo vikubwa mbele ya watu.
9
Kwa hiyo wakainuka wengine waliokuwa wa chama kilichoitwa cha Walibertino na watu wa Kirene na wa Alekisandria nao walitoka Kilikia na Asia, wakaulizana na Stefano.
10
Lakini hawakuweza kuyabisha, aliyoyasema kwa werevu uliokuwa wa kweli na kwa Roho.
11
Ndipo, walipoleta watu wengine waliosema: Tumemsikia, alivyosema maneno ya kumbeza Mose na Mungu.
12
Wakawachafua watu na wazee na waandishi, wakamjia, wakamkamata, wakampeleka barazani kwa wakuu.
13
Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema: Mtu huyu haachi kusema maneno ya kupakataa mahali Patakatifu, hata maonyo.
14
Kwani tumesikia, alivyosema: Yesu wa Nasareti atapabomoa mahali hapa na kuzigeuza desturi, Mose alizotupa.
15
Ndipo, wote waliokaa barazani kwa wakuu walipomkazia macho, wakauona uso wake kuwa kama uso wa malaika.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28