bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 8
Acts 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
1
Sauli naye alikuwa amependezwa na kuuawa kwake. Siku ile wateule waliokuwamo Yerusalemu wakashambuliwa na kufukuzwa kabisa; kwa hiyo wote wakatawanyika katika nchi za Yudea na za Samaria; waliosalia ni mitume tu.
2
Ndipo, watu wengine wenye kumcha Mungu walipomzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.
3
Lakini Sauli akawajengua wateule, akaingia nyumba kwa nyumba, akawakokota waume na wanawake, akawatia kifungoni.
4
Wale waliotawanyika wakapita huko na huko wakiipiga mbiu njema ya lile Neno.
5
Filipo akashuka kuuingia mji wa Samaria, akawapigia mbiu ya Kristo;
6
watu wengi wakashikamana na yale yaliyosemwa na Filipo, mioyo yao ikawa mmoja tu kwa hayo, waliyoyasikia na kuviona vielekezo, alivyovifanya.
7
Kwani wengi waliopagawa na pepo wachafu walitokwa nao, wakipiga makelele makubwa, hata wengi waliokuwa wenye kupooza na viwete wakapona.
8
Mjini mle mkawa na furaha nyingi.
9
Kulikuwa na mtu mjini mle, jina lake Simoni, aliyekuwa akiwahangaisha watu wote wa Samaria kwa uganga wake akijisemea mwenyewe: Mimi ni mwenye uwezo.
10
Wote, wadogo hata wakubwa, wakashikamana naye wakisema: Huyu ndio uwezo wa Mungu unaoitwa mkuu.
11
Lakini walishikamana naye, kwa sababu aliwahangaisha siku nyingi kwa uganga wake.
12
Lakini walipomtegemea Filipo aliyewapigia mbiu njema ya ufalme wa Mungu na ya Jina la Yesu Kristo, wakabatizwa, waume na wake.
13
Hata Simoni mwenyewe akamtegemea Mungu, akabatizwa, akashikamana na Filipo; alipoona vielekezo na matendo makuu ya nguvu yaliyofanyizwa naye akahangaika moyoni.
14
Mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia, ya kuwa Wasamaria wamelipokea Neno la Mungu, wakamtuma Petero na Yohana, waende kwao.
15
Nao wakashuka, wakawaombea, wapewe Roho takatifu.
16
Kwani kwao hakuna hata mmoja aliyeshukiwa nayo, walikuwa wamebatiziwa tu Jina la Bwana Yesu.
17
Papo hapo, wale walipowabandikia mikono, walipewa Roho takatifu.
18
Lakini Simoni alipoona, ya kuwa watu hupewa Roho, mitume wakiwabandikia mikono, akawaletea fedha,
19
akasema: Nipeni nami nguvu hii, mtu nitakayembandikia mikono apewe Roho takatifu!
20
Lakini Petero akamwambia: Fedha zako na ziangamie pamoja na wewe, kwa sababu umewaza, ya kuwa gawio lake Mungu linanunulika kwa mali!
21
Wewe jambo hili hugawiwi hata kifungu tu, kwani moyo wako haukunyoka mbele ya Mungu.
22
Sharti ujute na kuuacha huu uovu wako, ukimwomba Bwana, labda utapata kuondolewa mawazo ya moyo wako.
23
Kwani nakuona, unayo yaliyo machungu kama nyongo, tena u mtumwa wa upotovu.
24
Ndipo, Simoni alipojibu akisema: Niombeeni ninyi kwa Bwana mambo hayo, mliyoyasema, yasinipate hata moja!
25
Walipokwisha kulishuhudia Neno la Bwana na kulisema po pote wakarudi kwenda Yerusalemu wakiipiga hiyo mbiu njema katika vijiji vingi vya Wasamaria.
26
*Malaika wa Bwana akamwambia Filipo akisema: Inuka, uende upande wa kusini, uifuate barabara itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza, ileile iliyokwisha kufa.
27
Ndipo, alipoinuka akaenda. Mara akaona mtu wa Etiopia; huyu alikuwa mtunza mali na mtu mwenye nguvu wa Kandake, mfalme wa kike wa Etiopia, alizisimamia mali zake zote. Alikuwa amekwenda Yerusalemu kula sikukuu.
28
Lakini alipokuwa anarudi na kukaa garini mwake alikisoma kitabu cha mfumbuaji Yesaya.
29
Ndipo, Roho alipomwambia Filipo: Haya! Lijongelee gari hili, ulifuatefuate!
30
Filipo akamwendea mbio, akamsikia, alivyokisoma kitabu cha mfumbuaji Yesaya; alipomwuliza: Unayatambua, unayoyasoma?
31
akasema: Nitawezaje, mtu asiponiongoza? akambembeleza Filipo, apande, akae pamoja naye.
32
Nalo fungu la Maandiko, alilolisoma, lilikuwa hili: Kama kondoo alipelekwa kuchinjwa; kama mwana kondoo anavyomnyamazia mwenye kumkata manyoya, vivyo hivyo naye hakukifumbua kinywa chake.
33
Kwa hivyo, alivyonyenyekea, alinyimwa uamuzi mnyofu; yuko nani atakayesimulia, ukoo wake ulivyokuwa? Kwani ameondolewa katika nchi yao walio hai, asikae nchini.
34
Mtunza mali akamwuliza Filipo akisema: Nakuomba, uniambie: Haya mfumbuaji anayasema ya nani? Anajisema mwenyewe au anamsema mwingine?
35
Ndipo, Filipo alipokifumbua kinywa chake, akaanza kwa Maandiko yale yale akimpigia mbiu ya Yesu.
36
Walipoendelea njiani wakafika penye maji kidogo, mtunza mali akasema: Tazama, yako maji, iko nini tena inayozuia, nisibatizwe?
37
Filipo akasema: Ukimtegemea Bwana kwa moyo wako wote, inawezekana. Ndipo, alipojibu akisema: Namtegemea Yesu Kristo kuwa Mwana wake Mungu;
38
kisha akaagiza, gari lisimame, wakashuka wote wawili majini, Filipo na mtunza mali, akambatiza.*
39
Lakini walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana alimpokonya Filipo, mtunza mali asimwone tena. Kisha akaishika njia yake na kufurahi.
40
Lakini Filipo akaonekana Asdodi akiipiga hiyo mbiu njema katika miji yote, aliyoipita, hata akafika Kesaria.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28