bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 17
Acts 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 18 →
1
Wakapita katika Amfipoli na Apolonia, wakafika Tesalonike palipokuwa na nyumba ya kuombea ya Wayuda.
2
Kama Paulo alivyozoea, akaingia humo, akaongea nao maneno ya Maandiko siku tatu za mapumziko.
3
Akawafunulia na kuwaelezea, ya kuwa Kristo alipaswa na kuteswa na kufufuka katika wafu, akawaambia: Yesu, ambaye ninawatangazia habari zake, yuyu huyu ndiye Kristo.
4
Wamoja wao wakashindwa mioyoni, wakashikamana nao akina Paulo na Sila; nao waliotoka kwa Wagriki wenye kumcha Mungu walikuwa wengi mno, hata wanawake wenye cheo hawakuwa wachache.
5
Lakini Wayuda wakaingiwa na wivu, wakajichukulia kikundi cha majitu mabaya wasiokuwa na kazi; hao wakakusanya kundi zima la watu, kisha wakauchafua mji wote, wakaisogeleasogelea nyumba ya Yasoni, wakawatafuta, wawapeleke kwenye kundi lilelile.
6
Wasipowaona wakamburura Yasoni na ndugu wengine, wakaenda nao kwa wakubwa wa mji wakipiga kelele na kusema: Watu hawa waliouchafua ulimwengu wamefika hata hapa,
7
naye Yasoni ndiye aliyewafikiza. Hawa wote huyakanusha maagizo ya Kaisari wakisema: Mfalme ni mwingine, ni Yesu.
8
Wakahangaisha watu wengi, hata wakubwa wa mji wakayasikia.
9
Hao walipokwisha kumtoza Yasoni na wenzake mali zilizowatosha, wakawaacha, waende zao.
10
Ndipo, ndugu walipomsindikiza Paulo na Sila papo hapo na usiku kwenda Beroya. Walipofika huko wakaingia nyumbani mwa kuombea mwa Wayuda.
11
Hao walikuwa wema kuliko wale wa Tesalonike, wakalipokea Neno kwa mioyo iliyolipenda sana, kila siku wakayachunguza Maandiko, waone, kama ndivyo yalivyo kweli.
12
Hivyo wenzao wengi wakaja kumtegemea Bwana, vile vile hata kwa Wagriki wanawake na waume wenye cheo hawakuwa wachache.
13
Lakini Wayuda wa Tesalonike walipotambua, ya kuwa Neno lake Mungu linatangazwa na Paulo hata huko Beroya, wakaja, wakawahangaisha watu nako huko.
14
Papo hapo ndugu wakamsindikiza Paulo, wakamfikisha pwani. Lakini Sila na Timoteo wakakaa huko.
15
Lakini wale waliomsindiza Paulo wakaenda naye mpaka Atene. Walipokwisha kupata maagizo ya kuwapelekea akina Sila na Timoteo, kwamba waje upesi sana kwake, wakaenda zao.
16
*Paulo alipowangoja huko Atene akaumia rohoni mwake akiona, mji ulivyojaa miungu ya kutambikia.
17
Akaongea nao Wayuda na watu wenye kumcha Mungu nyumbani mwa kuombea. Hata sokoni alisema kila siku na wale, aliowakuta hapo.
18
Lakini kulikuwako wenye ujuzi wa chama cha Waepikurio na wa chama cha Wastoiko, wakabishana naye, wengine wakasema Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine tena wakasema: Anaonekana kuwa mtangazaji wa miungu migeni. Kwani alikuwa anawapigia hiyo mbiu njema ya Yesu na ya ufufuko.
19
Ndipo, walipomshika, wakampeleka panapoitwa Areopago, wakamwuliza: Twaweza kutambua, yalivyo hayo mafundisho yako mapya, unayoyasema?
20
Kwani unaingiza maneno mageni masikioni mwetu. Sasa twataka kutambua, hayo yatakapoelekea.
21
Lakini wenyeji wote wa Atene na wageni waliotua humo hakuna, walichokitunukia kuliko kusema au kusikia yaliyo mapya.
22
Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema: Enyi waume wa Atene, po pote ninawaona ninyi, mnavyotambikia miungu.
23
Kwani nilipozunguka na kupatazama pa kuombea penu nikaona pa kuchinjia ng'ombe za tambiko palipoandikwa: Penye Mungu asiyetambulikana. Basi, huyo, mnayemtumikia pasipo kumjua, ndiye, ninayewatangazia.
24
Mungu aliyeuumba ulimwengu navyo vyote vilivyomo hakai katika nyumba za kuombea zilizojengwa na mikono ya watu, kwani yeye ni Bwana wa mbingu na wa nchi.
25
Naye hatumikiwi na mikono ya watu, tena hatumii kitu cho chote, kwani yeye mwenyewe ndiye aliyewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
26
Kwa tendo lake yeye watu wa mataifa yote wametoka kwa mmoja, wakakaa ko kote katika nchi zote zilizoko nchini; akawagawia huko kale siku zao za kuwapo, akawakatia nayo mipaka ya makao yao.
27
Alitaka, wamtafute Mungu, kama wanaweza kumnyatia, mpaka wamwone. Namo miongoni mwetu sisi hamna hata mmoja tu, ambaye anamkalia mbali.
28
Kwani yeye ndiye, tunayekalia, tunayeendea, tunayekuwa naye, kama watunga nyimbo walivyosema hata kwenu kwamba: Uzao wake ndio sisi.
29
Basi, tukiwa uzao wake Mungu, haifai kumfananisha Mungu na maumbo ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe yaliyotengenezwa kwa uwezo na kwa mawazo ya kimtu.
30
Siku za kujikalia tu na kupumbaa Mungu ameziacha tu, zipite; lakini sasa anawaagiza watu wote po pote, wajute.
31
Kwani ameweka siku, atakapompa mtu mmoja, aliyemwonea kazi hiyo, auhukumu ulimwengu wote kwa wongofu; lakini kwanza anawahimiza wote, wamtegemee, maana amemfufua katika wafu.
32
Walipousikia ufufuko wa wafu, wengine wakamfyoza, wengine wakasema: Tunataka kukusikia na siku nyingine, utuelezee jambo hilo.
33
Ndipo, Paulo alipotoka katikati yao.
34
Lakini walikuwako waliogandamana naye, wakaja kumtegemea Bwana. Miongoni mwao alikuwamo mtu wa Areopago, ndiye Dionisio, tena mwanamke, jina lake Damari, na wengine waliokuwa pamoja nao.*
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28