bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 21
Acts 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 22 →
1
Lakini tulipokwisha kuagana nao tukatweka na kukielekeza chombo kwenda Ko kwa tanga moja; tulipofika, kesho yake tukaenda hapo Rodo; toka hapo tukafika Patara.
2
Tukaona chombo cha kuvukia hata Ufoniki, tukajipakia humo, tukatweka.
3
Tulipokuona kule Kipuro tukakuacha kushotoni, tukaendelea mpaka Ushami, tukashukia Tiro; kwani ndiko, chombo kilikoagiziwa kuipakua mizigo yake.
4
Tulipowaona wanafuanzi tukakaa lhuko siku saba. Nao wakamwambia Paulo kwa nguvu ya Roho, asipande kwenda Yerusalemu.
5
Lakini tulipoziishiliza siku zetu tukaondoka kwenda zetu; wakatusindikiza wote pamoja na wanawake na watoto mpaka weuni pa mji; hapo wakapiga magoti pwani, wakatuombea.
6
Tukaagana nao, tukaingia chomboni, lakini wale wakarudi kwao.
7
Nasi tulipokwisha kuimaliza safari ya baharini tukatoka Tiro, tukafika Putolemai, tukawaamkia ndugu, tukakaa kwao siku moja.
8
Kesho yake tukaondoka, tukafika Kesaria, tukaingia nyumbani mwa mpiga mbiu njema Filipo aliyekuwa miongoni mwao wale saba, tukakaa kwake.
9
Mtu huyu alikuwa na wana wa kike wanne, walikuwa wasichana wenye kufumbua.
10
Nasi tulipokaa siku nyingi kwake, pakashuka mfumbuaji toka Yudea, jina lake Agabo.
11
Akatujia, akauchukua mshipi wa Paulo, akajifunga miguuni na mikono, akasema: Ndivyo, asemavyo Roho Mtakatifu: Mwenye mshipi huu Wayuda watamfunga Yerusalemu vivyo hivyo, wamtie mikononi mwa wamizimu.
12
Tulipoyasikia haya sisi na wenyeji wa hapo tukambembeleza, asipande kwenda Yerusalemu.
13
Ndipo, Paulo alipojibu: Huku kulia kwenu na kuniponda moyo kuna maana gani? Kwani mimi nimejielekeza siko kufungwa tu, ila hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya Jina la Bwana Yesu.
14
Alipokataa kutusikia, tukanyamaza tukisema: Bwana ayatakayo na yafanyike!
15
Siku hizi zilipopita, tukatengeneza yote, tukapanda kwenda Yerusalemu.
16
Kulikuwa na wanafunzi Kesaria waliofuatana nasi, wakatupeleka kwa mtu aliyeitwa Mnasoni wa Kipuro aliyekuwa mwanafunzi wa kale, tufikie kwake.
17
Tulipofika Yerusalemu, ndugu wakatupokea kwa furaha.
18
Kesho yake Paulo akaingia mwa Yakobo pamoja nasi, nao wazee wote walikuwamo.
19
Akawaamkia, akawasimulia moja kwa moja mambo yote, Mungu aliyoyafanya kwa wamizimu kwa ile kazi yake, aliyoitumikia.
20
Walipoyasikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia Paulo: Ndugu yetu, unaona, ya kuwa Wayuda walioanza kumtegemea Bwana ni elfu nyingi na nyingi, hao wote hujikaza kuyashika Maonyo.
21
Lakini kwa ajili yako wewe wameambiwa ya kwamba: Unawafundisha Wayuda wote wanaokaa kwa wamizimu, wambeze Mose, ukiwaambia, wasiwatahiri watoto, wala wasiyafuate mambo yaliyo mazoezo tu.
22
Basi, iko nini inayofaa? Sharti kundi hilo zima likusanyike, kwani hawatakosa kusikia, ya kuwa umekuja.
23
Kwa hiyo ufanye, tutakavyokuambia! Tunao waume wanne wenye jambo, waliloliagana na Mungu.
24
Wachukue hao ujieue pamoja nao, uwalipie, wanyolewe vichwa! Hivyo wote watatambua, ya kuwa waliyoambiwa kwa ajili yako ni uwongo tu, ya kuwa wewe mwenyewe unaendelea na kuyashika Maonyo.
25
Lakini kwa ajili ya wamizimu walioanza kumtegemea Bwana tumewaandikia, tulivyopatana ya kwamba, waushike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni.
26
Ndipo, Paulo alipowachukua wale watu, kesho yake akaeuliwa pamoja nao, akapaingia Patakatifu, akatangaza, siku za weuo wao zitakapomalizika, kwamba ni hapo, kila mmoja atakapokwisha kutolewa kipaji cha weuo.
27
Siku zile saba ziliposalia kidogo kutimia, Wayuda walitoka Asia wakamwona Paulo hapo Patakatifu, wakalichanganya kundi lote la watu, wakamkamata kwa mikono yao,
28
wakapiga kelele kwamba: Waume na Isiraeli, tusaidieni! Huyu ndiye yule mtu anayefundisha po pote watu wote, waubeze ukoo wetu nayo Maonyo, hata mahali hapa! Tena ameingiza Wagriki hapa Patakatifu, ndivyo, alivyopapatia uchafu mahali hapa Patakatifu.
29
Kwani kwanza walikuwa wamemwona mjini pamoja na Tirofimo wa Efeso, wakamwazia, ya kuwa Paulo amemwingiza napo Patakatifu.
30
Mji wote ukatukutishwa, watu wote wakapakimbilia hapohapo, wakamkamata Paulo, wakamtoa hapo Patakatifu na kumburura; kisha milango yote ikafungwa papo hapo.
31
Nao walipotaka kumwua, uvumi ulikuwa umemfikia mkuu wa kikosi cha askari, ya kuwa mji wote wa Yerusalemu umevurugika.
32
Mara hiyo akachukua askari na wakubwa wao, akashuka kwao mbiombio. Wale walipomwona mkuu na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
33
Hapo, mkuu alipowafikia, akamshika, akaagiza, afungwe kwa minyororo miwili, akauliza: Nani huyu? Tena amefanya nini?
34
Lakini watu kwa hivyo, walivyokuwa wengi, wengine wakapiga kelele hivyo, wengine hivyo. Asipoweza kuyatambua yaliyo kweli kwa ajili ya makelele akaagiza, apelekwe bomani.
35
Alipofika pa kupandia akachukuliwa na askari, wamkingie ukorofi wa watu;
36
kwani watu wengi mno walimfuata wakipiga kelele kwamba: Mwondoe huyu!
37
Walipotaka kumwingiza bomani, Paulo akamwambia mkuu wa askari: Niko na ruhusa kukuambia neno? Naye aliposema: Unajua Kigriki?
38
Wewe si yule Mmisri aliyefanya kishindo siku hizi akichukua watu 4000 waliokuwa wauaji na kuwapeleka nyikani?
39
Paulo akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda toka mji wa Tarso, ni mwenyeji wa mji huo wa Kilikia usio mdogo; nakuomba, nipe ruhusa ya kusema na watu.
40
Alipompa ruhusa, Paulo akasimama juu hapo pa kupandia, akawapungia watu mkono; nao walipokuwa kimya kabisa, akasema nao Kiebureo, akawaambia:
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28