bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 26
Acts 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 27 →
1
Agripa alipomwambia Paulo: Una ruhusa kujisemea mwenyewe, ndipo, Paulo aliponyosha mkono, akajikania hivyo:
2
Mfalme Agripa, ninashangilia moyoni, kwa kuwa yote, ninayosutwa na Wayuda, nitajikania leo mbele yako wewe,
3
uliyeyatambua sanasana mazoea na mashindano yote ya Kiyuda. Kwa hiyo nakuomba, unisikilize kwa kuvumilia.
4
Mwendo wangu ulivyokuwa hapo mwanzo, nilipokuwa kijana pamoja na vijana wenzangu huko Yerusalemu, Wayuda wote wanavijua.
5
Kwani wamenitambua kale; wakitaka wangenishuhudia, ya kwamba nimekifuata kile chama kinachokaza kuyashika mambo ya tambiko letu, kwani nalikuwa Fariseo.
6
Hata sasa ninasimama hapa, nihukumiwe, kwa sababu nangojea, kile kiagio kitimie, Mungu alichokiagana na baba zetu.
7
Vile vile mashina yetu kumi na mawili hungojea, wakifikie; kwa hivyo wanajihimiza kumtumikia Mungu usiku na mchana. Hicho kingojeo ndicho, ninachosutiwa na Wayuda, mfalme Agripa.
8
Kwa sababu gani huwaza kwenu, ya kuwa neno hilo halitegemeki la kwamba: Mungu anafufua wafu?
9
Kweli nami vyaliniingia moyoni kwamba: Sharti nifanye mdngi ya kulipinga Jina la Yesu wa Nasareti.
10
Hayo niliyafanya huko Yerusalemu; nilipopewa ruhusa na watambikaji wakuu nikawatia watakatifu wengi kifungoni, tena walipouawa, nami nikasaidia.
11
Hata katika nyumba zote za kuombea niliwaumiza mara kwa mara, nikiwashurutisha kumbeza Yesu, nikawaendea na ukorofi kama mwenye wazimu, nikawakimbiza mpaka kwenye miji iliyoko ugenini.
12
Kwa hiyo nikaenda hata Damasko, nilipokwisha kupata maelekezo na maagizo kwa watambikaji wakuu.
13
Ilipokuwa saa sita ya mchana, ndipo, mfalme, nilipoona hapo njiani mwanga uliotoka mbinguni wenye kumetuka kulishinda jua, ukatumulikia pande zote mimi na wenzangu waliokwenda pamoja nami.
14
Tulipoanguka chini sote, nikasikia sauti iliyoniambia kwa msemo wa Kiebureo: Sauli, Sauli, unanifukuzaje? Utashindwa na kupiga mateke penye machomeo.
15
Mimi nilipouliza: Ndiwe nani, Bwana? Bwana akasema: Mimi ni Yesu, ambaye unanifukuza wewe.
16
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako! Kwani hii ndiyo, niliyokutokea; Nikulinganye, utumike kuyashuhudia, uliyoyaona, nayo utakayoonyeshwa nami.
17
Nitakuokoa kwao walio wa kwenu nako kwao wamizimu, maana ndiko, nitakakokutuma,
18
uwafumbue macho yao na kuwaongoza, watoke gizani, waingie mwangani, tena watoke katika nguvu ya Satani, wamfikie Mungu; hivyo watapata kuondolewa makosa na kupewa fungu lao penye watakatifu, wakiwa wakinitegemea.
19
Hapo, mfalme Agripa, sikukataa kuliitikia hilo jambo la mbinguni, nililoliona,
20
ila niliwatumikia kwanza wa Damasko, tena wa Yerusalemu, tena wote walioko katika nchi ya Yudea, kisha hata wamizimu nao, nikiwaambia, wajute wakimgeukia Mungu na kutenda matendo yaliyo ya kujuta kweli.
21
Kwa sababu hiyo Wayuda walinikamata, nilipokuwa hapo Patakatifu, wakajaribu kuniua.
22
Lakini kwa hivyo, nilivyopata msaada kwa Mungu, ninasimama mpaka siku hii ya leo nikiwaeleza wakubwa na wadogo; sisemi mengine, yasipokuwa yale, waliyoyasema Wafumbuaji na Mose kwamba:
23
Yatakayokuwapo ni haya: Kristo sharti ateswe, kisha atakuwa limbuko la ufufuko wa wafu, kisha atawaalika wao wa ukoo huu nao wamizimu, wafike mwangani.
24
Alipojikania hivyo, Festo akapaza sauti akisema: Paulo, una wazimu! Ujuzi wako mwingi unakupapayusha.
25
Paulo akasema: Bwana wangu Festo, sina wazimu, ila natoa maneno yenye kweli na yenye maana.
26
Nawe mfalme, haya unayajua vema; kwa hiyo nasema mbele yako waziwazi. Kwani najua sana, ya kuwa hayo yote hakuna hata moja, usilolitambua, kwa sababu hayo hayakufanyika pembeni.
27
Mfalme Agripa, unawategemea Wafumbuaji? Nimekujua, ya kuwa unawategemea.
28
Agripa akamwambia Paulo: Pamesalia padogo, ungenishinda, nikawa Mkristo.
29
Ndipo, Paulo aliposema: Namwomba Mungu, paliposalia padogo napo paliposalia pakubwa, wote hapa walionisikia leo, si wewe tu, awape kuwa, kama mimi nilivyo, pasipo minyororo hii.
30
Kisha mfalme na mtawala nchi na Berenike nao waliokaa pamoja nao wakainuka,
31
wakajongea pembeni, wakasemezana wao kwa wao: Mtu huyu hakufanya neno linalopasa, auawe au afungwe.
32
Agripa akamwambia Festo: Mtu huyu angeweza kufunguliwa, kama asingalikuwa ametaka kuhukumiwa na Kaisari.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28