bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 10
Deuteronomy 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 11 →
1
Wakati huo Bwana akaniambia: Jichongee mbao mbili za mawe kama zile za kwanza! Kisha panda kwangu huku mlimani! Jitengenezee nalo sanduku la mti!
2
Kisha nitaziandika hizo mbao yale maneno yaliyokuwa yameandikwa katika zile mbao za kwanza, ulizozivunja, kisha uziweke sandukuni.
3
Ndipo, nilipotengeneza sanduku la mti wa mgunga, nikachonga mbao mbili za mawe kama zile za kwanza, kisha nikapanda mlimani nikizishika hizo mbao mbili mkononi mwangu.
4
Akaziandika hizo mbao kuwa kama mwandiko wa kwanza yale maneno kumi, Bwana aliyowaambia ninyi huko mlimani toka motoni siku hiyo, mlipokusanyika; kisha Bwana akanipa.
5
Ndipo, nilipogeuka, nikatelemka mlimani, nikaziweka hizo mbao katika sanduku, nililolitengeneza, zikakaa humo, kama Bwana alivyoniagiza.
6
Kisha wana wa Isiraeli wakaondoka visimani kwa wana wa Yakani, wakaenda Mosera; ndiko, Haroni alikokufa, akazikwa huko, naye mwanawe Elazari akawa mtambikaji mahali pake.
7
Walipoondoka huko wakaenda Gudigoda, tena toka Gudigoda, wakaenda Yotibata, ndiyo nchi yenye vijito vya maji.
8
Siku zile Bwana akalitenga shina la Lawi, walichukue Sanduku la Agano la Bwana, tena wasimame mbele ya Bwana kumtumikia na kubariki watu kwa Jina lake, kama wanavyofanya hata leo.
9
Kwa hiyo lawi asipate kwa ndugu zake fungu la nchi kuwa lake, kwani Bwana ndiye fungu lake mwenyewe, kama Bwana Mungu wako alivyosema.
10
Mimi niliposimama huko mlimani kama siku zile za kwanza siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, Bwana akanisikia hata mara hiyo, Bwana hakutaka kuwaangamiza ninyi,
11
kwa hiyo Bwana akaniambia: Inuka, uende na kuwatangulia watu, waiingie hiyo nchi kuichukua, iwe yao, kwani ndiyo, niliyowaapia baba zao kuwapa.
12
Sasa, Isiraeli, yako mambo gani, Bwana Mungu wako anayokutakia, isipokuwa kumcha Bwana Mungu wako na kuzishika njia zake zote na kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote
13
na kuyashika maagizo ya Bwana na maongozi yake, mimi ninayokuagiza leo, upate kuona mema?
14
Tazama, mbingu nazo mbingu za mbingu nayo nchi pamoja nayo yote yaliyomo ni yake Bwana.
15
lakini Bwana alishikamana na baba zenu tu kwa kuwapenda, akawachagua ninyi mlio wazao wao waliokuwako nyuma yao akiwatoa katika makabila yote, kama inavyoelekea leo.
16
Kwa hiyo itahirini mioyo yenu, tena msizishupaze kosi zenu!
17
kwani Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu, ni Bwana wa mabwana, ni Mungu mkubwa atishaye kwa matendo ya nguvu, hapendelei uso wa mtu, hachukui mapenyezo.
18
Huamulia waliofiwa na wazazi nao wajane, hupenda wageni, awape chakula na nguo.
19
Kwa hiyo nanyi wapendeni wageni, kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
20
Mwogope Bwana Mungu wako, umtumikie, ugandamane naye. Napo utakapoapa litaje Jina lake!
21
Yeye ni shangilio lako na Mungu wako aliyekufanyizia yale matendo makuu yaliyotisha, uliyoyaona kwa macho yako.
22
Baba zako waliposhukia Misri walikuwa watu 70, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34