bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 18
Deuteronomy 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 19 →
1
Watambikaji Walawi, ndio shina lote la Lawi, wasipate fungu la nchi kuwa lao wenyewe kwao Waisiraeli. Ng'ombe za tambiko za Bwana za kuteketezwa nayo yampasayo Bwana kupewa yawe yao; ndiyo, watakayokula.
2
Kweli wasiwe na fungu lililo lao kwao ndugu zao, ila Bwana mwenyewe atakuwa fungu lao, kama alivyowaambia.
3
Lakini hii itakuwa haki yao watambikaji kwao watu watakaochinja ng'ombe ya tambiko, kama ni ng'ombe, au kama ni kondoo: sharti wampe mtambikaji mkono na mashavu mawili na matumbo.
4
Tena malimbuko ya ngano zako nayo ya mvinyo mbichi nayo ya mafuta, nayo malimbuko ya nywele za kondoo, mkiwanyoa, na mmpe.
5
Kwani Bwana Mungu wako amemchagua katika mashina yako yote, asimame na kutumikia katika Jina lake Bwana, yeye na wanawe siku zote.
6
Itakapokuwa, Mlawi atoke malangoni pako pawapo pote kwao Waisiraeli, anapokaa ugenini, aende kwa tunu yote ya roho yake mahali pale, Bwana atakapopachagua,
7
basi, na atumikie katika Jina la Bwana Mungu wake, kama ndugu zake Walawi wote wanaosimama hapo mbele ya Bwana.
8
Watakula sawasawa na kugawiana fungu kwa fungu kuliko yale, atakayoyapata kwa kuuza mali ya baba zake.
9
Utakapoingia katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, usijifundishe kuyafanya matapisho ya hao wamizimu.
10
Kwako asionekane mtu atakayemtumia mwanawe wa kiume au wa kike kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa, wala asionekane mwenye kuagulia ndege na mawingu, wala mpiga bao, wala mlozi,
11
wala mfinga nyoka kwa uganga, wala mwenye kuuliza mizimu, wala mwenye kujua uchawi wote, wala mfanya mashauri na wafu.
12
Kwani kila ayafanyaye hayo humchukiza Bwana, naye Bwana Mungu wako anawafukuza wao mbele yako kwa ajili ya hayo machukizo.
13
Lakini wewe sharti ukae kwa Bwana Mungu wako pasipo kumkosea.
14
Kwani mataifa hayo, utakayoyafukuza, huwasikia waaguliao mawingu na ndege, lakini wewe Bwana Mungu wako hakukupa ruhusa kuwatumia hao.
15
*Miongoni mwa ndugu zako wewe Bwana Mungu wako atakuinulia mfumbuaji atakayelingana na mimi, nanyi sharti mmsikie.
16
Ni kwa ajili yao yote, uliyomwomba Bwana Mungu wako kule Horebu siku hiyo ya mkutano kwamba: Nisiendelee kuisikia sauti ya Bwana Mungu wangu na kuuona huu moto mkubwa, nisife.
17
Ndipo, Bwana aliponiambia: Wamefanya vema waliposema hivyo.
18
Nitawainulia mfumbuaji miongoni mwa ndugu zao atakayelingana na wewe; nitampa maneno yangu kinywani mwake, awaambie yote, nitakayomwagiza.
19
Itakuwa, mtu akikataa kuyasikia maneno yangu, atakayoyasema katika Jina langu, mimi nitamlipisha.*
20
Lakini mfumbuaji atakayejikuza mwenyewe na kusema neno katika Jina langu, nisilomwagiza kulisema, analolisema katika jina la mungu mwingine, huyo mfumbuaji hana budi kufa.
21
Nawe ukiuliza moyoni mwako: Tutajuaje neno kuwa neno, Bwana asilolisema?
22
ni hivi: mfumbuaji akisema neno kwa Jina la Bwana, lakini hilo neno haliji, wala halitimii, basi, hilo ndilo neno, Bwana asilolisema, yule mfumbuaji amelisema kwa kujikuza tu, kwa hiyo usimwogope!
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34