bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 25
Deuteronomy 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 26 →
1
Watu watakapogombana na waende shaurini, waamuliwe, mwamuzi akimtokeza asiyekosa kuwa hakukosa, naye aliyekosa kuwa amekosa.
2
Huyo mkosaji akipaswa na kupigwa, mwamuzi na amlaze chini, wampige mbele yake fimbo zilizoyapasa maovu yake, nazo zihesabiwe.
3
Wakiisha kumpiga 40 wasiendelee! Kwani wakiendelea kumpiga kuzipita hizo, mapigo yatazidi, naye ndugu yako atabezwa machoni pako.
4
Ng'ombe mwenye kupura ngano usimfunge kinywa!
5
Ndugu wakikaa pamoja, mmoja wao akafa pasipo kuacha mwana wa kiume, mkewe yule aliyekufa asiolewe nje na mtu mgeni, ila ndugu yake mumewe sharti amwingilie na kumchukua kuwa mkewe, amsimikie ndugu yake unyumba.
6
Naye mwana wa kwanza, huyu mwanamke atakayemzaa, sharti amwandike kwa jina la ndugu yake aliyekufa, hilo jina lake lisifutwe kwao Waisiraeli.
7
Lakini yule mtu asipopendezwa kumchukua mkewe ndugu yake, huyu mke wa ndugu yake na apande kwenda langoni kwa wazee, awaambie: Ndugu yake mume wangu amekataa kumwinulia ndugu yake jina kwao Waisiraeli, asipotaka kumsimikia unyumba kwa kunichukua.
8
Kisha wazee wa mji huo na wamwite, waseme naye. Atakaposimama na kusema: Sipendezwi kumchukua,
9
yule mkewe ndugu yake na amkaribie machoni pao wazee, amvue kiatu mguuni pake na kumtemea mate usoni, kisha na aseme kwamba: Mtu asiyeijenga nyumba ya ndugu yake na afanyiziwe hivyo!
10
Kwa hiyo na aitwe jina lake kwao Waisiraeli: Nyumba ya mvuliwa kiatu.
11
Watu wawili walio ndugu wakipigana, naye mkewe mmoja wao akaja kumponya mumewe mkononi mwake anayempiga, akaupeleka mkono wake na kumkamata penye soni,
12
sharti umkate huo mkono wake pasipo kumwonea huruma.
13
Mfukoni mwako usiwe na vyuma vya kupimia vya namna mbili, vikubwa na vidogo.
14
Wala nyumbani mwako usiwe na pishi za namna mbili, kubwa na ndogo.
15
Vyuma vyako vya kupimia sharti viwe vizima vilivyo sawasawa, nazo pishi zako ziwe nzima zilizo sawasawa, siku zako zipate kuwa nyingi katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa.
16
Kwani Bwana Mungu wako huwachukia wanaoyafanya hayo yote, wao wote wafanyao mapotovu.
17
Yakumbuke, Waamaleki waliyokufanyizia njiani, mlipotoka Misri!
18
Walikushambulia njiani, wakawauwa wote waliokufuata nyuma kwa kuwa wanyonge, nawe ulikuwa umechoka, ukataka kuzimia roho, lakini wao hawakumwogopa Mungu.
19
Kwa hiyo hapo, Bwana Mungu wako atakapokutulizia adui zako wote watakaokuzunguka pande zote katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe fungu lako mwenyewe, hapo sharti utoweshe ukumbusho wa Waamaleki chini ya mbingu; usivisahau!
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34