bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 30
Deuteronomy 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 31 →
1
Hayo yote yatakapokujia, hayo ya mbaraka nayo ya kiapizo, niliyoyaweka mbele yako, nawe utakapoyaingiza moyoni mwako katika wamizimu wote, Bwana Mungu wako atakapokukumba kwenda kwao,
2
napo utakaporudi kwa Bwana Mungu wako, uisikie sauti yake na kuyafuata yote, mimi ninayokuagiza leo, uyafanye wewe na wanao kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote,
3
ndipo, Bwana Mungu wako atakapoyafungua mafungo yako kwa kukuhurumia, akukutanishe tena na kukutoa katika makabila yote, Bwana Mungu wako alikokutawanya.
4
Ijapo, uwe umekumbwa kwenda hata mapeoni kwa mbingu, huko nako Bwana Mungu wako atakukusanya na kukuchukua huko,
5
Bwana Mungu wako akupeleke katika nchi, baba zako waliyoichukua, iwe yao, uichukue nawe, iwe yako, kisha atakukalisha vema na kukufanya kuwa wengi kuliko baba zako.
6
Naye Bwana Mungu wako atautahiri moyo wako nayo mioyo yao wa uzao wako, mmpende Bwana Mungu wenu kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote, mpate kupona.
7
Kisha Bwana Mungu wako atavitimiza hivyo viapizo vyote, viwapate adui zako na wachukivu wako waliokufukuza.
8
Lakini wewe utaisikia tena sauti ya Bwana, uyafanye maagizo yake yote, mimi ninayokuagiza leo.
9
Ndipo, Bwana Mungu wako atakapokupatia mema mengi ya kuyasaza katika kazi zote za mikono yako na katika mazao ya tumbo lako na katika mazao ya nyama wako wa kufuga na katika mazao ya mashamba yako, kwani Bwana atakufurahia tena, akupatie mema, kama alivyowafurahia baba zako.
10
Hayo utayapata utakapoisikia sauti ya Bwana Mungu wako, uyaangalie magizo na maongozi yake yaliyoandikwa katika kitabu cha Maonyo haya, utakapomrudia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.
11
Kwani hili agizo, mimi ninalokuagiza leo, silo gumu, usiweze kulifanya, wala haliko mbali, usiweze kulifikia:
12
haliko mbinguni, useme: Yuko nani atakayetupandia mbinguni kulichukua na kutuletea, tulisikie, tupate kulifanya?
13
Wala haliko ng'ambo ya bahari, useme: Yuko nani atakayetuvukia bahari kwenda ng'ambo ya huko kulichukua na kutuletea, tulisikie, tupate kulifanya?
14
Kwani neno hilo linakukalia karibu sana, limo kinywani mwako namo moyoni mwako, upate kulifanya.
15
Tazama, nimeweka leo mbele yako maisha na mema, tena kifo na mabaya.
16
Mimi ninakuagiza leo kumpenda Bwana Mungu wako na kuzishika njia zake na kuyaangalia maagizo yake na maongozi yake na maamuzi yake, ndipo, utakapopona, watu wako wawe wengi, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi hiyo, wewe unayokwenda kuichukia, iwe yako.
17
Lakini moyo wako utakapogeuka, usisikie, utadanganyika, utambikie miungu mingine na kuitumikia.
18
Nami ninawatangazia leo hivi: Mtaangamia kabisa, msikae siku nyingi katika hiyo nchi, unayouvukia Yordani, uiingie na kuichukua, iwe yako.
19
Ninawatajia leo hivi mbingu na nchi kuwa mashahidi, ya kuwa nimeweka mbele yako maisha na kifo, mbaraka na kiapizo, ukayachagua maisha, upate kuishi wewe nao wa uzao wako,
20
mkimpenda Bwana Mungu wenu, mwisikie sauti yake na kugandamana naye; kwani humu ndimo, yalimo maisha yako na wingi wa siku zako za kukaa katika hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zako Aburahamu na Isaka na Yakobo kuwapa.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34