bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 20
Deuteronomy 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 21 →
1
Utakapotoka kwenda vitani kupigana na adui zako, ukaona farasi na magari na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope! Kwani Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri kukuleta huku yuko pamoja na wewe.
2
Tena hapo, mapigano yatakapokuwa karibu, mtambikaji na awakaribie ninyi kusema na watu.
3
Awaambie: Sikilizeni, Waisiraeli! Ninyi leo mnakwenda kupigana na adui zenu, lakini kwa hiyo mioyo yenu isilegee, msiwaogope na kutetemeka, wala msiwastuke.
4
Kwani Bwana Mungu wenu atakwenda pamoja nanyi kuwapigania na adui zenu, awaokoe.
5
Kisha wenye amri na waseme na watu na kuwaambia: Kama yuko mtu aliyejenga nyumba mpya, naye hajaieua, bado, na aende kurudi nyumbani kwake, asife katika mapigano, mtu mwingine akiieua.
6
Au kama yuko mtu aliyepanda shamba la mizabibu naye hajalilimbua, na aende kurudi nyumbani kwake, asife katika mapigano, mtu mwingine akalilimbua.
7
Au kama yuko mtu aliyeposa mwanamke, naye hajamwoa, na aende kurudi nyumbani kwake, asife katika mapigano, mwingine akamwoa.
8
Kisha mwenye amri na aendelee kusema na watu na kuwaambia: kama yuko mtu mwoga mwenye moyo uliolegea, na aende kurudi nyumbani kwake, asiiyeyushe mioyo ya ndugu zake kuwa, kama moyo wake ulivyo.
9
Nao wenye amri watakapokwisha kusema na watu, na waweke wakuu wa vikosi kuwatangulia watu.
10
Utakapokaribia mji kupigana nao, kwanza uulize mapatano.
11
Watakapokuitikia kwa kutaka mapatano, wakakufungulia malango, basi, watu wote watakaoonekana humo watakufanyizia kazi za nguvu na kukutumikia hivyo.
12
Lakini watakapokataa kukuitikia mapatano wakitaka kupigana na wewe, basi, na uusonge.
13
Bwana Mungu wako atakapoutia mikononi mwako, sharti uwapige wa kiume wote waliomo kwa ukali wa upanga.
14
Lakini wanawake na watoto na nyama wa kufuga nayo yote yatakayokuwa humo mjini na ujitwalie yote pia kuwa mateka yako ya humo mjini, nawe utaweza kula mateka ya adui zako, Bwana Mungu wako atakayokupa.
15
Hivyo ndivyo, utakavyoifanyizia miji yote iliyoko mbali sana kutoka kwako, isiyo miongoni mwa miji ya wamizimu hawa wa huku.
16
Lakini katika miji ya haya makabila, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe fungu lako mwenyewe, usiponye hata mmoja avutaye pumzi.
17
Ila sharti uwatie mwiko kabisa wa kuwapo hao Wahiti na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza,
18
kusudi wasiwafundishe ninyi kuyafanya hayo matapisho yote, waliyoifanyizia miungu yao, ninyi mkamkosea Bwana Mungu wenu.
19
Utakapokaa siku nyingi kwa kusonga mji na kupigana nao, upate kuuteka, usiiharibu miti yake na kuikata kwa shoka, ila ule matunda yao, kwa hiyo usiikate. Au miti ya shambani ni watu, uiendee kuisonga nayo usoni pako?
20
Hiyo miti tu, utakayoijua, ya kuwa siyo miti izaayo matunda, na uiharibu na kuikata, uitumie ya kuujengea boma mji huo unaopigana na wewe, hata uanguke.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34