bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 22
Deuteronomy 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 23 →
1
Utakapoona, ng'ombe au kondoo wa ndugu yako wakipotea, usijifiche kuwa kama mtu asiyewaona, ila sharti uwarudishe kwake ndugu yako.
2
Kama huyo ndugu yako hakai karibu yako, usimjue, uwaweke nyumbani mwako, wakae kwako, mpaka ndugu yako awatafute; ndipo, utakapowarudisha kwake.
3
Ndivyo ufanye hata utakapomwona punda wake au nguo zake au cho chote, ndugu yako atakachopotelewa nacho; wewe utakapokiona hutaweza kujificha kuwa kama mtu asiyeona.
4
Utakapoona, punda wa ndugu yako au ng'ombe wake wakianguka njiani, usijifiche kuwa kama mtu asiyewaona, ila sharti umsaidie kuwainua.
5
Mwanamke asivae cho chote cha mwanamume, wala mwanamume asivae nguo za kike! Kwani kila atakayefanya mambo kama hayo humchukiza Bwana Mungu wako.
6
Utakapokuta kiota cha ndege njiani, kiko mbele yako katika mti au chini mchangani chenye makinda au chenye mayai, naye mama akiwaatamia makinda au mayai, usimchukue mama pamoja na watoto,
7
ila umwache mama, ajiendee, uchukue watoto tu, upate kuona mema, nazo siku zako ziwe nyingi.
8
Utakapojenga nyumba mpya, sharti juu darini utengeneze kikingio, usifanye nyumbani mwako kuwa mwenye damu ya mtu, mtu akianguka huko.
9
Shamba lako la mizabibu usilipande mbegu za namna mbili, lote pia lisiwe mali ya Patakatifu: mbegu, ulizozipanda, pamoja na mazao ya mizabibu.
10
Ukilima usitumie ng'ombe na punda pamoja.
11
Usivae nguo iliyofumwa kwa kuchanganya nyuzi za manyoya ya kondoo na za pamba pamoja.
12
Jifanyizie vishada penye pembe zote nne za nguo zako za kijifunika!
13
Itakuwa, mtu amwoe mkewe na kuingia kwake, kisha achukizwe naye.
14
Kwa hiyo atamsingizia mambo ya uwongo, ampatie jina baya na kusema: Nimemwoa mwanamke huyu; lakini nilipoingia kwake sikumwona kuwa mwanamwali.
15
Vitakapokuwa hivyo, babake na mamake yule msichana na wamchukue na kumpeleka kwa wazee wa mji huo langoni pake pamoja nayo yanayoweza kuujulisha uwanawali wake.
16
Naye babake yule msichana na awaambie wazee: Nimempa mwanangu mtu huyu kuwa mkewe, kisha akachukizwa naye;
17
akamsingizia mambo ya uwongo kwamba: Sikumwona kuwa mwanamwali. Lakini yatazameni haya yanayoujulisha uwanawali wa mwanangu! Kisha waikunjue hiyo nguo mbele ya wazee wa mji huo.
18
Kwa hiyo wazee wa mji huo na wamchukue yule mwanamume, wamchape.
19
Kisha wamtoze fedha mia, wampe babake msichana, kwa kuwa yule alimpatia msichana wa Kiisiraeli jina baya; kisha awe mkewe, asiweze kumpa ruhusa kwenda zake siku zake zote.
20
Lakini lile neno likiwa la kweli, nayo yanayoujulisha uwanawali wake yasipoonekana,
21
na wampeleke yule msichana hapo pa kuiingilia nyumba ya baba yake, hapo watu wa mji wote wampige mawe, hata afe, kwa kuwa alifanya ujinga mbaya kwao Waisiraeli wa kufanya ugoni nyumbani mwa baba yake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
22
Mtu atakapooneka, ya kuwa amelala na mwanamke aliyeolewa na mwingine, sharti wafe wote wawili, yule mwanamume aliyelala na mwanamke, naye mwanamke. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo kwao Waisiraeli.
23
Mwanamwali akiisha kuposwa na mtu, tena mwingine aliyemkuta mjini akilala naye,
24
sharti mwapeleke wote wawili langoni pa mji huo, mwapige mawe, hata wafe, yule kijana wa kike, kwa kuwa hakupiga kelele mjini, naye yule mwanamume, kwa kuwa amemkorofisha mchumba wa mwenzake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
25
Lakini mwanamume atakapomkuta shambani kijana wa kike aliyekwisha kuposwa, akamkamata kwa nguvu, akalala naye, basi, huyu mwanamume aliyelala naye atakufa peke yake,
26
lakini yule kijana wa kike msimfanyizie neno, kwani yule kijana wa kike hakukosa neno lipasalo, auawe, kwa kuwa jambo hili ni sawasawa, kama mtu aliyemwinukia mwenziwe na kumwua, afe.
27
Kwani alimkuta shambani, naye yule kijana wa kike aliyekwisha kuposwa alipolia, hakuwako aliyemwokoa.
28
Mtu atakapoona mwanamwali asiyeposwa bado, akamshika na kulala naye, basi, wakionwa,
29
yule mwanamume aliyelala naye sharti ampe babake yule kijana wa kike fedha hamsini, kisha sharti awe mkewe, kwa kuwa amemkorofisha, naye hana ruhusa kumwacha siku zake zote.
30
Mtu asimchukue mkewe baba yake, wala asiifunue pembe ya nguo zake!
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34