bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 33
Deuteronomy 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 34 →
1
Hii ndiyo mbaraka, Mose, yule mtu wa Mungu, aliyowabariki wana wa Isiraeli kabla ya kufa kwake,
2
akasema: Bwana alitoka Sinai, akakuchelea kama jua toka Seiri, akautokeza mwanga wake toka mlimani kwa Parani, akaja na kutoka katikati yao maelfu kumi ya watakatifu, kuumeni kwake ukawaka moto uliowatokezea Maonyo.
3
Kweli anayapenda makabila ya watu, watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; nao walipokaa miguuni pako, kila mmoja akapokea neno lake lililompasa.
4
Mose akatuagiza Maonyo, yawe fungu lao mkutano wa Yakobo,
5
akawa mfalme kwake Yeshuruni, vichwa vyao hao watu walipokusanyika kwake pamoja nao wale walio mashina ya Isiraeli.
6
Rubeni na awepo uzimani, asife, ijapo watu wake wahesabike.
7
Nayo hii ni mbaraka ya Yuda, akasema: Bwana, uisikie sauti ya Yuda! Umwingize kwao walio ukoo wake! Kwani mikono yake itakapowapigia vita, nawe msaidie kuwashinda wapingani wake!
8
Naye Lawi akamwambia: Mwanga wako na Kweli yako ni yao watu wako wamchao Mungu, uliowajaribu kule Masa na kuwagombeza kwenye Maji ya Magomvi.
9
Ndio wanaowaambia baba zao na mama zao: Hatukuwaona, nao ndugu zao hawawatazami, wala wana wao hawawajui, kwani huliangalia Neno lako, hulishika Agano lako.
10
Wao na wawafundishe Wayakobo maamuzi yako, nao Waisiraeli Maonyo yako, tena na wavukize mavukizo, yapate kuingia puani mwako, wakitoa ng'ombe nzima za tambiko pako pa kukutambikia.
11
Bwana, zibariki nguvu zao nazo kazi za mikono yao, zikupendeze! Wapingani na wachukivu uwavunje viuno, wasiwainukie tena!
12
Benyamini akamwambia: Mpendwa wa Bwana na akae kwake na kutulia! Bwana humfunika mchana kutwa na kukaa kati ya mabega yake.
13
Naye Yosefu akamwambia: Nchi yako na iwe imebarikiwa naye Bwana, akiipatia kipaji kizuri cha mbinguni, ndio umande, nayo maji mengi yakaayo ndani ya nchi.
14
Na aipatie nacho kipaji kizuri cha mazao, jua linayoyaivisha, nacho kipaji kizuri cha matunda ya kila mwezi!
15
Na aipatie nayo yatokayo juu ya milima iliyo ya zamani, nacho kipaji kizuri cha vilima vilivyo vya kale na kale!
16
Navyo vipaji vizuri vya nchi, navyo vijaavyo ndani yake! Upendeleo wake akaaye porini na ukijie kichwa chake Yosefu, juu ya utosi wake yeye aliyewekwa kwa kutengwa na ndugu zake!
17
Mwanawe wa kwanza ni dume la ng'ombe lenye utukufu, kama pembe za nyati zilivyo, ndivyo, zilivyo nazo pembe zake; atakapozitumia atawakumba makabila ya watu, waanguke chini wote pia walioko huku hata mapeoni kwa nchi, kwani ndivyo, walivyo makumi ya maelfu ya Efuraimu, tena ndivyo, walivyo nayo maelfu ya Manase.
18
Naye Zebuluni akamwambia: Zebuluni, zifurahie safari zako za baharini, nawe Isakari, yafurahie mahema yako!
19
Wataalika makabila ya watu kuja mlimani; ndiko, watakakochinja ng'ombe za tambiko zilizo za kweli, kwani mafuriko ya bahari yatawanyonyesha, mpaka washibe, nazo zile mali nyingi zilizofichika mafukoni zitakuwa zao.
20
Naye Gadi akamwambia: Atukuzwe aliyempatia Gadi nchi iliyo pana! Huota kama jike la simba, apate kurarua mikono na vichwa.
21
Alipoiona nchi ya kwanza, ikawa yake, kwani huko aliwekewa kazi ya mwongozi. Lakini naye akaja kwao waliokuwa vichwa vya watu hawa, akaishindisha haki ya Bwana na kuyatimiza mashauri yake akiwa pamoja nao hao Waisiraeli.
22
Naye Dani akamwambia: Dani ni mwana mchanga wa simba, hushambulia na kutoka Basani.
23
Nafutali akamwambia: Nafutali atashiba yampendezayo, azidishiwe mbaraka ya Bwana; chukua nchi ya baharini na ya kusini, iwe yako!
24
Naye Aseri akamwambia: Aseri ndiye katika hawa wana atakayepata mbaraka zaidi, tena atakuwa mpendwa wao ndugu zake, nao mguu wake atauchovya katika mafuta;
25
makomeo yake yatakuwa ya chuma na ya shaba, nazo nguvu zako ziwe zizo hizo siku zote, utakazokuwapo.
26
Mungu wake Yeshuruni, hakuna wa kufanana naye, ndiye anayepita juu mbinguni, akusaidie, namo mawinguni, auonyeshe utukufu wake.
27
Yeye Mungu wa kale ni kimbilio, chini yako imekunjuliwa mikono iliyo ya kale na kale. Atawafukuza adui mbele yako akikuambia: Angamiza tu!
28
Kwa hiyo Waisiraeli watakaa na kutulia vema, watakuwa pake yao kwenye chemchemi yake Yakobo katika nchi yenye ngano na mvinyo mbichi, nazo mbingu zake zitadondoa umande.
29
Mwenye shangwe ni wewe, Isiraeli! Yuko nani aliyeokolewa na Bwana kama wewe? Yeye ni ngao inayokusaidia, tena ni upanga unaokupatia utukufu. Kwa hiyo adui zako watakunyenyekea, lakini wewe utatembea na kuvikanyaga vilima vyao.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34