bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 2
Deuteronomy 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 3 →
1
Kisha tukageuka na kuondoka huko, turudi nyikani na kushika nja ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu, kama Bwana alivyoniambia, tukazunguka siku nyingi kwenye mlima wa Seiri.
2
Kisha Bwana akaniambia kwamba:
3
Siku, mlizouzunguka mlima huu, ni nyingi, sasa geukeni kwenda upande wa kaskazini!
4
Waagize watu kwamba: Piteni katika mipaka yao ndugu zenu wana wa Esau wanaokaa Seiri! Wao watawaogopa ninyi, lakini jiangalieni sana,
5
msiwapelekee vita! Kwani sitawapa ninyi hata kipande kidogo cha nchi yao, ijapo pawe pa kukanyagia kwa mguu mmoja tu, kwani mlima wa Seiri nilimpa Esau, auchukue, uwe nchi yake.
6
Chakula sharti mjinunulie kwao kwa fedha, mpate kula, nayo maji ya kunywa sharti myanunue kwao kwa fedha.
7
Kwani Bwana Mungu wako amekubariki katika mambo yote, uliyoyafanya kwa mkono wako, anazijua safari zako, ulizozifanya katika nyika hii kubwa; hii miaka arobaini Bwana Mungu wako amekuwa pamoja na wewe, usikose cho chote.
8
Ndipo, tulipoendelea kusafiri na kuondoka kwao ndugu zetu wana wa Esau waliokaa Seiri, tukaziacha njia za huko nyikani na za Elati na za Esioni-Geberi, tukageuka na kushika njia ya kwenda kwenye nyika ya Moabu.
9
Ndipo, Bwana aliponiambia: Usiwasonge Wamoabu, wala msiwapelekee vita mkipigana nao! Kwani sitakupa kipande cha nchi yao, mwichukue, iwe yenu, kwa kuwa naliwapa wana wa Loti nchi ya Ari, waichukue, iwe yao.
10
Kale Waemi walikaa huko, nao walikuwa watu wakubwa na warefu wengi mno kama Waanaki.
11
Nao waliwaziwa kuwa Majitu kama Waanaki, lakini Wamoabu waliwaita Waemi.
12
Huko Seiri kale walikaa Wahori; ndio, wana wa Esau waliowafukuza na kuwaangamiza mbele yao, kisha wakakaa mahali pao, kama Waisiraeli walivyofanya katika nchi, waliyoichukua, iwe yao, Bwana aliyowapa.
13
Sasa inukeni, mkivuke kijito cha Zeredi! Ndipo, tulipokivuka hicho kijito cha Zeredi.
14
Nazo siku, tulizosafiri toka Kadesi-Barnea mpaka tulipokivuka kijito cha Zeredi, zilikuwa miaka 38; ndipo, kile kizazi chote cha wapiga vita kilipokuwa kimeishilizwa makambini, kama Bwana alivyowaapia.
15
Nao mkono wa Bwana ulikuwa ukiwapingia, upate kuwaangamiza makambini, mpaka waishilizwe kabisa.
16
Ikawa, wale wapiga vita walipokwisha kuishilizwa wote na kuondolewa kwa wenzao wa ukoo kwa hivyo, walivyokufa,
17
Bwana akaniambia kwamba:
18
Leo hivi wewe upite mpaka wa Moabu na kupita Ari.
19
Kisha utafika karibu kwao wana wa Amoni; usiwasonge, wala usiwapelekee vita! Kwani sitakupa kipande cha nchi ya wana wa Amoni, ukichukue, kiwe chako, kwani nchi hiyo naliwapa wana wa Loti, waichukue, iwe yao.
20
Nchi hii nayo iliwaziwa kuwa ya Majitu; kale Majitu walikaa huko kweli, nao Waamoni waliwaita Wazamuzumi.
21
Nao walikuwa watu wakubwa na warefu wengi mno kama Waanaki, lakini Bwana aliwaangamiza mbele yao; ndipo, walipoichukua nchi yao, iwe yao, wakakaa mahali pao.
22
Ni vivyo hivyo, alivyowafanyizia wana wa Esau wanaokaa Seiri, maana mbele yao waliwaangamiza Wahori, wapate kuichukua nchi yao na kukaa huko mahali pao mpaka siku hii ya leo.
23
Nao Waawi waliokaa vijijini mpaka Gaza waliangamizwa na Wakafutori waliotoka Kafutori, kisha wao walikaa mahali pao.
24
Nanyi inukeni na kuondoka huku, mkivuke kijito cha Arnoni! Tazama Mwamori Sihoni, mfalme wa Hesiboni, nimemtia mikononi mwako pamoa na nchi yake. Haya! Anza kuichukua ukimpelekea vita, upigane naye!
25
Leo hivi nitaanza kuyatisha makabila yote chini ya mbingu, wakustukie kwa kukuogopa; watakapousikia uvumi wako watakutetemekea na kujipinda kwa machungu.
26
Ndipo, nilipotuma wajumbe toka nyikani kwa Kedemoti kwake Sihoni, mfalme wa Hesiboni, kumwambia maneno haya ya mapatano kwamba:
27
Ninataka kupita katika nchi yako na kwenda njiani tu, nisiondoke njiani kwenda wala kuumeni wala kushotoni.
28
Chakula utaniuzia kwa fedha, nipate kula, nayo maji utanipa kwa fedha, nipate kunywa ninataka kupita tu kwa miguu yangu.
29
Hivyo ndivyo, walivyonifanyizia nao wana wa Esau wanaokaa Seiri, nao Wamoabu wanaokaa Ari; fanya hivyo nawe, mpaka nitakapouvuka Yordani, niingie nchi, Bwana Mungu wetu aliyotupa.
30
Lakini Sihoni, mfalme wa Hesiboni, hakutaka kutupa ruhusa ya kupita kwake, kwa kuwa Bwana Mungu wako alimpa mawazo magumu rohoni na kuushupaza moyo wake, apate kumtia mikononi mwako, kama inavyoelekea sasa.
31
Ndipo, Bwana aliponiambia: Tazama, nimeanza kumtoa Sihoni na nchi yake mbele yako. Nawe anza kuichukua nchi yake, iwe yako!
32
Sihoni alipotoka asubuhi, yeye pamoja na watu wake wote, wapigane nasi kule Yasa,
33
Bwana Mungu wetu akamtoa mbele yetu, tukampiga, yeye na wanawe na watu wake wote,
34
tukaiteka miji yake yote siku hizo, tukawatia mwiko wa kuwapo wote pia waliokuwamo mijini, wanawaume na wanawake na watoto, hatukusaza hata mmoja aliyeweza kukimbia.
35
Ni nyama tu wa kufuga na nyara za miji, tuliyoiteka, ndizo tulizojichukulia.
36
Toka Aroeri ulioko ukingoni kwenye kijito cha Arnoni, katika miji iliyoko kule kwenye kijito mpaka Gileadi haukuwako mji wenye boma refu la kutushinda, yote pia Bwana Mungu wetu aliitoa mbele yetu.
37
Nchi ya wana wa Amoni tu hukuikaribia, ile nchi yote iliyoko kando ya kijito cha Yakobo pamoja na miji ya milimani; kwani hiyo yote Bwana Mungu wetu alitukataza kuichukua.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34