bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 23
Deuteronomy 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 24 →
1
Katika mkutano wa Bwana asiingie mume aliyekomeshwa kuzaa kwa kupondwa au kwa kukatwa.
2
Katika mkutano wa Bwana asiingie mwana wa ugoni wa ndugu na ndugu; ijapo awe wa kizazi chake cha kumi, asiingie katika mkutano wa Bwana.
3
Mwamoni wala Mmoabu asiingie katika mkutano wa Bwana, ijapo awe wa kizazi chao cha kumi, kale na kale na wasiingie katika mkutano wa Bwana.
4
Kwa kuwa hapo, mlipotoka Misri, hawakuwaendea na kuwapelekea ninyi wala chakula wala maji, tena walimkodisha Bileamu, mwanawe Beori, na kumtoa Petori ulioko Mesopotamia, aje, akuapize.
5
Lakini Bwana Mungu wako akakataa kumsikia Bileamu, akakugeuzia kiapizo chake kuwa mbaraka kwa hivyo, Bwana Mungu wako alivyokupenda.
6
Nawe usiwatafutie utengemano wala mema yo yote siku zako zote kale na kale!
7
Lakini Mwedomu usichukizwe naye; kwani ni ndugu yako. Wala Mmisri usichukizwe naye, kwani ulikuwa mgeni katika nchi yake.
8
Wana wao watakaozaliwa wa kizazi cha tatu wataweza kuingia katika mkutano wa Bwana.
9
Utakapotoka makambini kuwaendea adui zako, jiangalie, usifanye kibaya cho chote!
10
Atakapokuwako kwako mtu asiye mwenye kutakata kwa jambo lililompata na usiku, sharti atoke kwenda nje ya makambi, asiingie ndani ya makambi.
11
Itakapokuwa saa ya jioni, ajiogeshe majini, kisha jua litakapokuchwa, aweza kuingia ndani ya makambi.
12
Tena huko nje ya makambi uwe na mahali pa kuendea chooni.
13
Namo katika vyombo vyako uwe na muo; napo utakapokwenda chooni huko nje, kwanza ufukue nao kishimo, upate kukaa, kisha uyafunike yaliyokutoka.
14
Kwani Bwana Mungu wako hutembea katikati ya malango yako, akuponye na kuwatia adui zako mikononi mwako. Kwa hiyo makambi yako sharti yawe matakatifu, asione kwako cho chote kisichofaa, akarudi nyuma na kukuacha.
15
Mtumwa aliyekukimbilia, ajiponye mikononi mwa bwana wake, usimrudishe kwake yule bwana wake.
16
Na akae kwako mahali, atakapojichagulia po pote penye malango yako patakapokuwa pema machoni pake, nawe usimsumbue.
17
Katika wana wa kike wa Kiisiraeli wasiwe wagoni wa Patakatifu, wala katika wana wa kiume wa Kiisiraeli wasiwe wagoni wa Patakatifu.
18
Wala usiingize Nyumbani mwa Bwana Mungu wako mshahara wa ugoni wala fedha za kuuza mbwa, ijapo ziwe za kiapo cho chote, kwani Bwana Mungu wako huzikataa zote mbili kwa kuchukizwa nazo.
19
Usimkopeshe ndugu yako, ujipatie faida ya fedha au faida ya chakula au faida ya cho chote, watu wanachokikopeshea faida.
20
Asiye wa Kiisiraeli na umkopeshe, ujipatie faida, lakini ndugu yako usimkopeshe, ujipatie faida, kusudi Bwana Mungu wako akubarikie kazi zote, mikono yako itakazozifanya katika hiyo nchi, utakayoiingia kuichukua, iwe yako.
21
Utakapoapa kiapo cha kumpa Bwana Mungu wako cho chote usikawie kukitimiza, kwani Bwana Mungu wako atakitafuta kwako, nawe usipompa utakuwa kama mwenye kujikosesha.
22
Lakini utakapoacha kuapa hivyo hukosi.
23
Lakini yaliyokwisha kutoka midomoni mwako sharti uyaangalie na kuyafanya, kama ulivyomwapia Bwana Mungu wako kwa kuyapenda mwenyewe uliyoyasema kwa kinywa chako.
24
Utakapoingia mizabibuni kwa mwenzako utaweza kula zabibu, kama roho yako itakavyopenda, hata ushibe, lakini usitie nyingine chomboni.
25
Utakapoingia penye ngano za mwenzako zilizoiva utaweza kukonyoa masuke kwa mkono wako, lakini usiyakatekate mabua ya mwenzako kwa mundu.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34