bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 21
Deuteronomy 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 22 →
1
Atakapoonekana mtu aliyeuawa katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako, naye akiwa analala porini, yule aliyemwua asijulikane,
2
basi, wazee wako na waamuzi wako na watoke, wazipime njia za kwenda katika miji inayomzunguka yule mtu aliyeuawa.
3
Wazee wa mji huo utakaokuwa karibu zaidi ya yule mtu aliyeuawa sharti wachukue mori ya ng'ombe asiyefanyishwa kazi bado, wala asiyevuta bado gari au jembe.
4
Huyo mori wazee na wamtelemshe penye mto usiokupwa, pasipolimwa wala pasipopandwa, kisha wamvunje huyo mori shingo huko mtoni.
5
Kisha watambikaji Walawi na waje huko, kwani Bwana Mungu wako aliwachagua kumtumikia na kubariki katika Jina lake Bwana, magomvi yote na mapigano yote yamalizwe kwa kusema kwao.
6
Kisha wazee wote wa mji huo ulio karibu zaidi ya yule mtu aliyeuawa na wainawe mikono yao juu ya huyo mori aliyevunjwa shingo huko mtoni
7
na kusema kwa kupaza sauti: Mikono yetu haikuimwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona, ilipomwagwa.
8
Bwana, wapoze walio ukoo wako wa Isiraeli, uliowakomboa, usiwalipishe damu ya mtu asiyekora manza iliyomwagwa katikati yao walio ukoo wako wa Isiraeli! Ndipo, watakapopata upozi kwa ajili ya hiyo damu.
9
Hivyo ndivyo, utakavyoondoa katikati yako damu ya mtu asiyekora manza, utakapoyafanya haya yaongokayo machoni pake Bwana.
10
Utakapotoka kwenda kupigana na adui zako, naye Bwana Mungu wako atakapowatia mikononi mwako, uwachukue kuwa mateka.
11
Nawe ukiona katika hayo mateka mwanamke mwenye mwili mzuri wa kupendezwa naye, basi, utamchukua kuwa mkeo.
12
Kwa hiyo umwingize nyumbani mwako, ajinyoe nywele za kichwani pake, ajikate nazo kucha za vidoleni pake,
13
azivue nazo nguo, alizokuwa amezivaa alipotekwa, akae nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake mwezi mzima, kisha utaingia kwake, uwe mumewe, naye awe mkeo.
14
Lakini itakapokuwa, usipendezwe tena naye, utampa ruhusa, ajiendee, atakakopenda, lakini usimwuze kwa fedha, wala usimkorofishe, kwa kuwa ulimtumia kuwa mkeo.
15
Itakuwa, mtu awe na wake wawili, naye mmoja atapendezwa naye, lakini wa pili atachukizwa naye, wakamzalia watoto, yule apendezwaye naye naye yule achukizwaye naye, naye mwana wa kwanza ni wake yule achukizwaye naye.
16
Baadaye siku zitakapotimia, awagawanyie wanawe mali zake, wazichukue, ziwe urithi wao, hataweza kumfanya mwanawe yule apendezwaye naye kuwa mwana wa kwanza mahali pake mwanawe wa kwanza aliyezaliwa naye yule achukizwaye naye,
17
ila hana budi kumtokeza kuwa wa kwanza huyo mwana aliye wake mkewe achukizwaye naye, amgawie mafungu mawili ya mali zake zote zinazoonekana kwake, kwani huyo ni wa kwanza, nguvu zake ziliyemzaa; kwa hiyo haki ya kuzaliwa wa kwanza ni yake yeye.
18
Itakuwa, mtu awe na mwana mtundu na mkatavu asiyesikia wala sauti ya baba yake wala sauti ya mama yake, asisikie, ijapo wamchape,
19
basi, baba yake na mama yake na wamkamate, wampeleke kwao wazee wa mji wao langoni pake,
20
wawaambie wazee: Huyu mwana wetu ni mtundu na mkatavu, hazisikii sauti zetu, ni mlafi na mnywaji.
21
Kisha watu wote wa huo mji wa kwao na wamtupie mawe, afe. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako, kwani Waisiraeli wote watakapovisikia wataogopa.
22
Itakuwa, mtu aliyekora manza za kufa auawe, watu wakimtundika mtini.
23
Lakini mzoga wake usikae hapo mtini usiku kucha, ila sharti umzike siku iyo hiyo, kwani aliyetundikwa ameapizwa na Mungu; huko ni kwamba: usiipatie uchafu nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe fungu lako mwenyewe.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34