bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 13
Deuteronomy 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 14 →
1
Atakapoinuka katikati yako mfumbuaji au mwota ndoto na kukutolea kielekezo au kioja,
2
nacho hicho kielekezo au kioja, alichokuambia, kitakapotimia, ndipo, atakapokuambia: Twende, tufuate miungu mingine, msiyoijua, tuitumikie!
3
Lakini usiyasikie maneno ya mfumbuaji huyo au ya mwota ndoto huyo! Kwani Bwana Mungu wenu atawajaribu tu, ajue, kama ninyi mnampenda Bwana Mungu wenu kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote.
4
Mfuateni Bwana Mungu wenu na kumcha, myashike maagizo yake na kuisikia sauti yake, mmtumikie na kugandamana naye!
5
Lakini yule mfumbuaji au yule mwota ndoto sharti auawe, kwa kuwa amesema, mmwache Bwana Mungu wenu aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri na kuwakomboa nyumbani, mlimokuwa watumwa; naye yule alitaka kukudanganya, uondoke katika hiyo njia, Bwana Mungu wako aliyokuagiza kuishika. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako!
6
Itakuwa, ndugu yako aliyezaliwa na mama yako au mwanao wa kiume au wa kike au mkeo anayekaa kfuani pako au mwenzako, unayempenda, kama unavyojipenda mwenyewe, akuhimize penye njama kwamba: Twende, tutumikie miungu mingine, usiyoijua wewe, wasiyoijua nao baba zako!
7
Nayo ndiyo iliyomo miongoni mwa miungu ya makabila yanayoaa na kuwazunguka ninyi pande zote, wengine wao wanakukalia karibu, wengine mbali toka mwanzo wa nchi hata mwisho wake.
8
Basi itakapokuwa hivyo, usimwitikie, wala usimsikie, jicho lako lisimwonee machungu, usimhurumie, wala usimfiche,
9
ila mwue kabisa! Mkono wako sharti uwe wa kwanza wa kumua, kisha mikono yao watu wote na ifuate.
10
Sharti umpige mawe, hata afe! Kwani alijaribu kukudanganya, umwache Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani ulimokuwa mtumwa.
11
Nao Waisiraeli wote watakapovisikia wataogopa, wasiendelee kufanya kwako mabaya kama nayo.
12
Itakuwa, upate habari ya mmojawapo katika miji yako, Bwana Mungu wako atakayokupa ya kukaa humo, kwamba:
13
Wako watu wasiofaa waliotoka katikati yako, waliowadanganya wenyeji wa miji yao kwamba: Twende, tutumikie miungu mingine, msiyoijua!
14
Basi, utakapovisikia, sharti utafute na kuchunguza na kuuliza vema; kisha utakapoona, ya kama neno hili ni la kweli, ikaelekea, ya kama tapisho hilo limefanyika kweli katikati yako,
15
huna budi kuwapiga wenyeji wa mji huo kwa ukali wa upanga na kuutia huo mji pamoja nayo yote yaliyomo mwiko wa kuwapo, nao nyama wao wa kufuga sharti uwaue kwa ukali wa upanga.
16
Kisha na uyakusanye mateka yote katikati ya uwanja wake, uuteketeze huo mji kwa moto pamoja na amteka yake yote kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana Mungu wako ya kuteketezwa yote nzima, uwe chungu ya majivu kale na kale, usijengwe tena.
17
Katika vile vyote vilivyotiwa mwiko wa kuwapo kisioneke cho chote kitakachogandamana na mkono wako, Bwana ayatulize tena makali yake yaliyowaka moto, akuonee machungu, akuhurumie na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako.
18
haya yatakuwa, utakapoisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyaangalia maagizo yake yote, mimi ninayokuagiza leo, uyafanye yanyokayo machoni pake Bwana Mungu wako.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34