bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 5
Deuteronomy 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 6 →
1
Mose akawapazia sauti Waisiraeli wote, akawaambia: Sikieni, Waisiraeli, maongozi na maamuzi, mimi ninayoyasema leo masikioni mwenu, mjifundishe na kuyaangalia, mpate kuyafanya!
2
Bwana Mungu wetu alifanya Agano na sisi kule Horebu;
3
Agano hilo Bwana hakulifanya na baba zetu, ila na sisi wenyewe tuliopo leo hapa sote wenye uzima.
4
Huko mlimani Bwana alisema nasi uso kwa uso toka motoni.
5
Siku hiyo mimi nilisimama katikati ya Bwana nanyi, niwatangazie Neno la Bwana, kwani mliuogopa ule moto, kwa hiyo hamkupanda mlimani; naye alisema:
6
Mimi ndimi Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa.
7
Usiwe na miungu mingine ila mimi!
8
Usijifanyie kinyago, wala mfano wo wote wa vitu vilivyoko mbinguni juu, wala vilivyoko nchini chini, wala vilivyomo majini chini ya nchi!
9
Usivitambikie, wala usivitumikie! Kwani mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; manza za baba nitazipatilizia wana, nikifikishe kizazi cha tatu na cha nne, kwao wanichukiao.
10
Lakini nitawafanyizia mema, nikifikishe hata kizazi cha maelfu, kwao wanipendao na kuyashika maagizo yangu.
11
Usilitaje Jina la Bwana Mungu wako bure! Kwani Bwana hatamwachilia alitajaye Jina lake bure.
12
Ishike siku ya mapumziko kuitakasa, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza!
13
Siku sita sharti ufanye kazi, uyamalize mambo yako yote!
14
Lakini siku ya saba ndiyo ya kumpumzikia Bwana Mungu wako. Hapo usifanye kazi yo yote, wala wewe, wala mwanao wa kiume, wala wa kike, wala mtumishi wako wa kiume, wala wa kike, wala ng'ombe wako wala punda wako wala nyama wako ye yote wa kufuga, wala mgeni wako aliomo malangoni mwako, mtumishi wako wa kiume na wa kike apate kupumzika kama wewe!
15
Sharti ukumbuke, ya kama ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, naye Bwana Mungu wako akakutoa huko kwa kutoa nguvu za kiganja chake na kwa kuukunjua mkono wake; kwa hiyo Bwana Mungu wako alikuagiza kuifanya siku ya mapumziko.
16
Mheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, siku zako zipate kuwa nyingi, nawe upate kuona mema katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!
17
Usiue!
18
Usizini!
19
Usiibe!
20
Usimshuhudie mwenzio uwongo!
21
Usimtamani mke wa mwenzio! Wala usiitamani nyumba ya mwenzio, wala shamba lake, wala mtumishi wake wa kiume, wala wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote, mwenzio alicho nacho!
22
Maneno haya Bwana aliwaambia wao wote wa mkutano wenu kule mlimani kwa sauti kuu toka motoni mle winguni mwenye weusi, hakuongeza neno, kisha akayaandika katika mbao mbili za mawe, akanipa mimi.
23
Ikawa, mlipoisikia sauti toka gizani, nao mlima ulipowaka moto, mkanikaribia ninyi mliokuwa vichwa vya mashina yenu na wazee wenu,
24
mkasema: Tazama, Bwana Mungu wetu ametuonyesha utukufu na ukuu wake, tukaisikia nayo sauti yake toka motoni, siku hii ya leo tumeona, ya kuwa Bwana anasema na mtu, naye hafi.
25
Sasa mbona tufe, moto huu mkubwa ukitula? Tukiendelea kuisikia tena sauti ya Bwana Mungu wetu hatuna budi kufa.
26
Kwani yuko wapi mwingine mwenye mwili, ndiye aisikie kama sisi sauti ya Mungu Mwenye uzima, akisema toka motoni, kisha awepo mwenye uzima?
27
Nenda wewe, uyasikilize yote, Bwana Mungu wetu atakayoyasema, kisha wewe tuambie yote, Bwama Mungu wetu aliyoyasema! Nasi tutakapoyasikia tutayafanya.
28
Bwana alipozisikia sauti za maneno yenu, mliyoniambia, yeye Bwana akaniambia: Nimezisikia sauti za maneno ya watu hawa, waliyokuambia, hayo yote waliyoyasema ni mema.
29
Laiti wangekuwa siku zote wenye mioyo inayoniogopa hivyo, wayaangalie maagizo yangu yote, wao na wana wao wapate kuona mema kale na kale!
30
Nenda, uwaambie: Rudini tu mahemani mwenu!
31
Lakini wewe uje hapa kusimama kwangu, nikuambie maagizo na maongozi na maamuzi yote, utakayowafundisha, wayafanye katika nchi hiyo, mimi nitakayowapa, waichukue, iwe yao.
32
Kwa hiyo angalieni, mfanye, kama Bwana Mungu wenu alivyowaagiza ninyi, msiondoke kwake kwenda wala kuumeni wala kushotoni!
33
Ila njia zote, Bwana Mungu wenu alizowaagiza ninyi, zishikeni na kuzifuata, mkae uzimani na kuona mema, nazo siku zenu ziwe nyingi katika nchi, mnayokwenda kuichukua, iwe yenu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34