bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 7
Deuteronomy 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 8 →
1
Bwana Mungu wako atakapokuingiza katika nchi hiyo, utakayoiingia kuichukua, iwe yako, ndpo, atakapong'oa huko mbele yako mataifa mengi, Wahiti na Wagirgasi na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi, ndio mataifa saba yaliyo yenye watu wengi na yenye nguvu kuliko wewe.
2
Bwana Mungu wako atakapowatoa mbele yako, uwapige, sharti uwatie mwiko kabisa wa kuwapo, usifanye agano nao, wala usiwahurumie.
3
Wala usioane nao: mwanao wa kike usimpe mwana wa kiume wa kwao, wala mwana wa kike wa kwao usimpe mwanao wa kiume.
4
Kwani ataugeuza moyo wa mwanao, aache kunifuata, watumikie miungu mingine; ndipo, makali ya Bwana yatakapokuwakia, akuangamize upesi.
5
Ila mwafanyizie hivyo: pao pa kutambikia sharti mpabomoe, nazo nguzo zao za mawe za kutambikia mzivunje, nayo miti yao ya Ashera mwikate, navyo vinyago vyao vya kuchongwa mviteketeze kwa moto.
6
Kwani wewe ndiwe kabila takatifu la Bwana Mungu wako; wewe Bwana Mungu wako alikuchagua katika makabila yote yaliyoko huku nchini, uwe kabila lake mwenyewe.
7
Bwana hakushikamana nanyi na kuwachagua, kwa kuwa m wengi kuliko makabila mengine, kwani mlikuwa wachache kuliko makabila yote,
8
ila kwa kuwa Bwana aliwapenda ninyi, akataka kukitimiza kiapo, alichowaapia baba zenu, kwa hiyo Bwana aliwatoa ninyi kwa mkono wake wenye nguvu, akawakomboa mkononi mwa Farao, mfalme wa Misri, na kuwatoa nyumbani, mlimokuwa watumwa.
9
Kwa hiyo jua, ya kuwa Bwana Mungu wako ni Mungu kweli, ni Mungu mwelekevu anayeyatimiza maagano na magawio kwao wampendao na kuyashika maagizo yake, akifikishe hata kizazi cha maelfu.
10
Lakini wao wamchukiao huwalipisha waziwazi na kuwaangamiza, hakawii kumlipisha waziwazi amchukiaye.
11
Kwa hiyo yaangalieni maagizo na maongozi na maamuzi, mimi ninayokuagiza leo kuyafanya.
12
Itakuwa, mtakapoyasikia haya maamuzi na kuyaangalia, myafanye, naye Bwana Mungu wako atakutimilizia maagano na magawio, aliyowaapia baba zako.
13
Ndipo, atakapokupenda, akubariki na kukufanya kuwa wengi, ayabariki nayo mazao ya tumbo lako nayo mazao ya shamba lako, ngano zako na mvinyo zako mbichi na mafuta yako na ndama wako na wana kondoo wako, watakaozaliwa katika nchi hiyo, Bwana aliyowaapia baba zako kukupa.
14
Utakuwa umebarikiwa kuliko makabila yote, hatakuwa kwako mtu, wala mume, wala mke asiyezaa, nao nyama wenu wa kufuga watakuwa vivyo hivyo.
15
Nao ugonjwa wote Bwana atauondoa kwako, hata hayo maradhi mabaya ya Misri, unayoyajua, atayazuia kwako, atayafikisha tu kwao wote wakuchukiao.
16
Nayo makabila yote, Bwana Mungu wako atakayokupa, uyale, usiyaonee huruma kabisa, wala usiitumikie miungu yao, kwani hii itakuwa tanzi la kukunasa.
17
Napo, utakaposema moyoni mwako: Mataifa haya ni mengi ya kunishinda, nitawezaje kuyafukuza?
18
Usiwaogope, ila yakumbuke sana, Bwana Mungu wako aliyomfanyizia Farao nao Wamisri wote.
19
Yakumbuke hayo majaribu makuu, macho yako yaliyoyaona, navyo vielekezo na vioja, nacho kiganja chake chenye nguvu, nao mkono, Bwana Mungu wako alioukunjua alipokutoa. Hivyo ndivyo, Bwana Mungu wako atakavyoyafanyizia makabila yote, wewe unayoyaogopa.
20
Tena Bwana Mungu wako atatuma mavu kwao, waangamie nao watakaosalia kwa kujificha, usiwaone.
21
Usiwastuke! Kwani Bwana Mungu wako yuko katikati yako, naye ni Mungu mkubwa anayeogopesha.
22
Yeye Bwana Mungu wako atayang'oa hayo mataifa mbele yako moja kwa moja, kwani hutaweza kuwamaliza upesi, nyama wa porini wasizidi kuwa wengi kwako.
23
Bwana Mungu wako atawatoa mbele yako na kuwahangaisha mahangaiko makubwa, hata waishe kuangamizwa.
24
Nao wafalme wao atawatia mikononi mwako, nawe sharti uyatoweshe majina yao chini ya mbingu; hakuna atakayeweza kusimama mbele yako, mpaka uwaangamize.
25
Vinyago vya miungu yao vya kuchongwa sharti mviteketeze kwa moto, usitamani kuzichukua fedha na dhahabu vilizotiwa, usinaswe nazo, kwani zinamchukiza Bwana Mungu wako.
26
Wala usiingize nyumbani mwako machukizo kama hayo, usitiwe nawe mwiko wa kuwapo kama wao, ila na yakuchukize kabisa na kukutapisha kwa kuwa yenye mwiko.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34