bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 3
Deuteronomy 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 4 →
1
Kisha tukageuka, tukapanda na kushika njia ya Basani. Naye Ogi, mfalme wa Basani, akatoka, atujie yeye pamoja na watu wake wote, wapigane nasi kule Edirei.
2
Lakini Bwana akaniambia: Usimwogope! Kwani nimemtia mikononi mwako pamoja na watu wake wote na nchi yake. Nawe umfanyizie, kama ulivyomfanyizia Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni.
3
Kisha Bwana Mungu wetu akamtia mikononi mwetu huyo Ogi, mfalme wa Basani, pamoja na watu wake wote, tukampiga, hatukusaza kwake hata mmoja aliyeweza kukimbia.
4
Tukaiteka miji yake yote siku hizo, haukuwako mji kwao, tusiouchukua: miji 60 nacho hicho kipande kizima cha Argobu, ndio ufalme wote wa Ogiwa Basani.
5
Miji hiyo yote ilikuwa yenye maboma magumu na marefu na malango na makomeo; tena tukapata miji mingi sana iliyokuwa wazi.
6
Tukawatia mwiko wa kuwapo, kama tulivyomfanyizia Sihoni, mfalme wa Hesiboni, tulipowatia mwiko wa kuwapo wote pia waliokuwamo mijini, wanawaume na wanawake na watoto.
7
Lakini nyama wa kufuga wote na nyara za miji tukajichukulia.
8
Ndivyo, tulivyozichukua siku hizo nchi za wafalme wawili wa Waamori waliokaa ng'ambo ya huku ya Yordani toka kijito cha Arnoni mpaka milimani kwa Hermoni.
9
Wasidoni waliita milima ya Hermoni Sirioni, nao Waamori waliiita Seniri.
10
Nasi tukaichukua miji yote ya nchi ya tambarare na nchi yote ya Gileadi na ya Basani mpaka Salka na Edirei, iliyokuwa miji ya ufalme wa Ogi kule Basani.
11
Yeye ogi, mfalme wa Basani, alikuwa amesalia peke yake kwa masao ya Majitu; mkikitazama kitanda chake, ni kitanda cha chuma, nacho kingaliko katika mji wa Raba wa wana wa Amoni, urefu wake ni mikono tisa, nao upana wake ni mikoni minne, mkipima kwa mikono wa mtu.
12
Siku hizo tukaichukua nchi hiyo, iwe yetu toka Aroeri ulioko kwenye kijito cha Arnoni. Nusu ya milima ya Gileadi pamoja na miji yake ikawapa Warubeni na Wagadi.
13
Kipande cha Gileadi kilichosalia na Basani yote iliyokuwa ufalme wa Ogi nikawapa wao wa nusu ya shina la Manase, ni kipande chote cha Argobu pamoja na Basani yote inayoitwa nchi ya Majitu.
14
Yairi, mwana wa Manase, alikichukua kile kipande chote cha Argobu hata mpakani kwa Wagesuri na Wamakati, akaziita hizo nchi za Basani kwa jina lake Mahema ya Yairi; ndivyo, zinavyoitwa hata leo.
15
Makiri nikampa Gileadi.
16
Warubeni na Wagadi nikawapa kipande cha Gileadi mpaka kijito cha Arnoni, mpaka uwe mtoni katikati; tena mpaka ukafika kijito cha Yakobo ulio mpaka wa wana wa Amoni.
17
Tena nyika inayopakana na Yordani toka Kinereti hata kwenye bahari ya nyikani, ndio Bahari ya Chumvi chini ya matelemko ya Pisiga upande wa maawioni kwa jua.
18
Siku hizo nikawagiza ninyi kwamba: Bwana Mungu wenu amewapa nchi hii, mwichukue, iwe yenu; kwa hiyo wa kwenu wote walio wenye nguvu na washike mata ya vita, mvuke mbele ya ndugu zenu hao wana wa Isiraeli.
19
Wanawake na watoto wenu na makundi yenu tu na wakae katika miji yenu, kwani najua, ya kuwa mnayo makundi mengi.
20
Hapo, Bwana atakapowapatia ndugu zenu kutulia kama ninyi, nao watakapokwisha kuichukua nchi, Bwana Mungu wenu atakayowapa ng'ambo ya huko ya Yordani, ndipo, mtakaporudi kila mtu kwenye nchi yake, aliyoichukua, iwe yake, niliyowapa ninyi.
21
Naye Yosua nikamwagiza siku hizo kwamba: Macho yako yameyaona yote, Bwama Mungu wetu aliyowafanyizia hao wafalme wawili; hivyo ndivyo, Bwana atakavyozifanyizia nchi zote za kifalme, utakazoziingia wewe.
22
Msiwaogope! Kwani Bwana Mungu wenu ndiye atakayewapigia vita.
23
Siku hizo nikambembeleza Bwana kwamba:
24
Bwana Mungu wangu, wewe umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukuu wako na nguvu za mkono wako; kwani yuko Mungu gani mbinguni na duniani anayeweza kufanya matendo, kama hayo ya uwezo wako mwingi?
25
Nipe ruhusa, nivuke, niione nchi hiyo njema iliyoko ng'ambo ya Yordani, hiyo milima mizuri, nayo ya Libanoni.
26
Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, kwa hiyo Bwana hakunisika, akaniambia: Acha tu! Usiseme tena na mimi kwa ajili ya shauri hili!
27
Panda juu mlimani kwa Pisiga, uyainue macho yako na kuyaelekeza upande wa baharini na wa kaskazini na wa kusini na wa maawioni kwa jua, uitazame hiyo nchi kwa macho yako. Kwani hutauvuka mto huu wa Yordani.
28
Mwagizie Yosua mambo yako! Mtie nguvu na kumshikiza moyo! Kwani yeye ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, naye ndiye atakayewagawia nchi hiyo, utakayoiona, iwe yao.
29
Kisha tukakaa bondeni na kuelekea Beti-Peori.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34