bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 8
Deuteronomy 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 9 →
1
Maagizo yote, mimi ninayokuagiza leo, sharti myaangalie, myafanye, mpate kupona na kuwa wengi na kuiingia hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zenu, mwichukue, iwe yenu.
2
Zikumbuke njia zote, Bwana Mungu wako alizokuendesha nyikani hii miaka 40, akunyenyekeze na kukujaribu, ayajue yaliyomo moyoni mwako, kama utayaangalia maagizo yake, au kama utayakataa.
3
Akakunyenyekeza na kukutia njaa, lakini kisha akakulisha Mana, usizozijua wewe, wala baba zako hawakuzijua, akajulisha, ya kama mtu hataishi kwa chakula tu, ila kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Bwana.
4
Nguo zako hazikuchakaa mwilini pako, wala miguu yako haikuvimba hii miaka 40.
5
Hapo ujue moyoni mwako, ya kuwa Bwana Mungu wako anakuchapa, kama mtu anavyomchapa mwanawe.
6
Kwa hiyo yaangalie maagizo ya Bwana Mungu wako, upate kuzishika njia zake na kumcha.
7
Kwani Bwana Mungu wako ndiye atakayekuingiza katika nchi hiyo njema iliyo nchi yenye vijito na visima na viziwa vya maji yatokeayo mabondeni na vilimani.
8
Ni nchi yenye ngano na mawele na mizabibu na mikuyu na mikomamanga, ni nchi yenye michekele iletayo mafuta, nazo asali ziko.
9
Ni nchi, utakakokula chakula na kushiba sana, kwani hutakosa cho chote; ni nchi yenye mawe ya chuma, nazo shaba utazichimbua ndani ya milima yake.
10
Kwa hiyo utakapokula na kushiba sharti umtukuze Bwana Mungu wako kwa ajili ya nchi hiyo njema, aliyokupa.
11
Jiangalie, usimsahau Bwana Mungu wako, ukiacha kuyaangalia maagizo yake na maamuzi yake na maongozi yake, mimi ninayokuagiza leo.
12
Hapo, utakapokula na kushiba, tena utakapojenga nyumba nzuri na kukaa humo,
13
tena ng'ombe na mbuzi na kondoo wako watakapokuwa wengi, nazo fedha na dhahabu zako zitakapokuwa nyingi, nazo mali zako zote zitakapokuwa nyingi,
14
jiangalie, moyo wako usijikuze, ukamsahau Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa!
15
Naye ndiye aliyekuongoza katika ile nyika kubwa inayoogopesha sana kwa nyoka za moto na kwa nge walioko na kwa kiu iliyoko nyingi, kwa kuwa hakuna maji; lakini yeye alikutolea maji katika mwamba mgumu sana.
16
Akakulisha nyikani Mana, baba zako wasizozijua, akunyenyekeze na kukujaribu, apate kukufanyizia mema, yawe ya mwisho ya kukupa.
17
kama sivyo, ungalisema moyoni mwako: Nguvu zangu na uwezo wa mikono yangu ndizo zilizonipatia mali hizi.
18
Mkumbuke Bwana Mungu wako, kwani yeye ndiye anayekupa nguvu za kujipatia mali, alishikize Agano lake, alilowaapia baba zako, kama inavyoelekea leo.
19
Lakini itakapokuwa, umsahau Bwana Mungu wako na kufuata miungu mingine, uitumikie na kuitambikia, ninawashuhudia leo, ya kuwa mtaangamia kabisa.
20
Kama Bwana alivyoyaangamiza yale mataifa mbele yenu, ndivyo, mtakavyoangamia nanyi, kwa kuwa hamkuisikiliza sauti ya Bwana Mungu wenu.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34