bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 14
Deuteronomy 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 15 →
1
Ninyi m watoto wake Bwana Mungu wenu; kwa hiyo msijichanje chale, wala msizinyoe nyushi katikati ya macho yenu kwa ajili ya mfu!
2
Kwani ninyi m watu watakatifu wa Bwana Mungu wako, maana Bwana akikuchagua kuwa kabila lililo lake mwenyewe kuliko makabila yote yakaayo huku nchini.
3
Usile cho chote kinachotapisha!
4
Hawa ndio nyama, mtakaowala: ng'ombe, kondoo na mbuzi,
5
kulungu na paa na funo na mbarapi na kuro na pofu na swala.
6
Nyama wote wenye kwato zilizopasuka na kutengeka kabisa kuwa kwato mbili, kama ni wenye kucheua, ndio, mtakaowala miongoni mwa nyama.
7
Lakini nao hao msiwale miongoni mwao wanaocheua namo miongoni mwao walio wenye kwato zilizopasuka na kutengeka: ngamia na sungura na pelele. Kweli wanacheua, lakini hawapasui kwato, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
8
Naye nguruwe, kweli anayapasua makwato, lakini hacheui; kwa hiyo ni mwiko kwenu. Nyama zao hao msizile, nayo mizoga yao msiiguse.
9
Katika nyama wote waliomo majini mtakula hawa: wote wenye mapezi na magamba mtawala;
10
lakini wote wasio wenye mapezi na magamba msiwale! ni mwiko kwenu.
11
Kila ndege mwenye kutakata mtakula.
12
Lakini wao, mtakaoacha kula nyama zao, ni hawa: kozi na pungu na furukombe,
13
na tumbuzi na mwewe na ngusu na ndugu zake,
14
na makunguru yote na ndugu zao,
15
na mbuni na kinega na dudumizi na kipanga na ndugu zake,
16
na mumbi na bundi na yangeyange,
17
na korwa na tai na shakwe,
18
na korongo na kitwitwi na ndugu zake na hudihuda na popo.
19
Wadudu wote wenye mabawa wanaotambaa ni mwiko kwenu, hawaliwi.
20
Ndege wote wenye kutakata mtakula.
21
Msile kibudu cho chote! Mgeni aliomo malangoni mwako utampa, ale, au utakiuza kwa mtu wa kimizimu. Kwani ninyi m watu watakatifu wa Bwana Mungu wenu. Kitoto cha mbuzi usikipike katika maziwa ya mama yake.
22
Mwaka kwa mwaka sharti utoe fungu la kumi la mapato yote ya mbegu zako zitakazotoka shambani.
23
Hili fungu la kumi ulile mbele ya Bwana Mungu wako mahali pale, atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, nalo hilo fungu la kumi ulitolee ngano zako na mvinyo zako mbichi na mafuta yako, tena wana wa kwanza wa ng'ombe nao wa mbuzi na kondoo wako, upate kujifunza kumcha Bwana Mungu wako siku zote.
24
Kama safari ya kutoka kwako kwenda huko itakuwa ndefu zaidi, usiweze kuyapeleka hayo matoleo, kwa kuwa ni mbali zaidi kutoka kwako kwenda mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, basi, hapo Bwana Mungu wako atakapokubariki,
25
yale matoleo yageuze kuwa fedha, kisha hizo fedha zifunge mkononi mwako, upate kwenda nazo mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua.
26
Ndipo, utakapoweza kujipatia kwa hizo fedha yote, roho yako itakayotunukia, ng'ombe na mbuzi na kondoo na mvinyo na vileo nayo mengine yote, roho yako itakayoyapenda, ujipatie, kisha utakula hapo mbele ya Bwana Mungu wako, mfurahiwe pamoja wewe nao waliomo nyumbani mwako.
27
Naye Mlawi atakayekuwapo malangoni pako usimwache, kwani hana fungu la nchi kwako lililo lake mwenyewe.
28
Miaka mitatu itakapopita, mafungu yote ya kumi utakayoyatolea mapato yako ya mwaka huo, uyaweke malangoni pako.
29
Kisha Walawi, kwa kuwa kwako hawana fungu lao la nchi lililo lao wenyewe, na waje pamoja na wageni, nao wliofiwa na wazazi, nao wajane waliomo malangoni mwako, na waje, wale, washibe! Hivyo ndivyo, Bwana Mungu wako atakavyokubarikia kazi zote za mikono yako, utakazozifanya.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34