bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 16
Deuteronomy 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 17 →
1
Uangalie mwezi wa Abibu, ule sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wako! Kwani ulikuwa mwezi wa Abibu, Bwana Mungu wako alipokutoa huko Misri na usiku.
2
Ndipo umchinjie Bwana Mungu wako kondoo ya Pasaka, ndio ng'ombe na mbuzi na kondoo, mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake.
3
Sikukuu hiyo usile cho chote kilichochachwa, ila siku zake saba sharti ule mikate isiyochachwa kuwa mikate ya matesoni, kwa kuwa ulitoka upesiupesi na kiwogawoga katika nchi ya Misri, upate kuikumbuka siku hiyo ya kutoka katika nchi ya Misri siku zote za maisha yako.
4
Siku hizo saba isionekane chachu katika mikate yako, wala nyama za yule kondoo, utakayemchinja siku ya kwanza jioni, zisilale usiku huo hata asubuhi.
5
Huwezi kuichinja kondoo ya Pasaka malangoni pako miongoni mwa miji, Bwana Mungu wako atakayokupa.
6
Ila mahali pale tu, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, ndipo, utakapoichinja kondoo ya Pasaka jioni, jua likiisha kuchwa, ndio saa zilezile zilizokuwa, ulipotoka Misri.
7
Napo mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua, ndipo, utakapoipika na kuila palepale; kisha asubuhi yake na ugeuke nyuma kwenda hemani kwako.
8
Siku sita sharti ule mikate isiyochachwa, nayo siku ya saba na mkutanie kumheshimu Bwana Mungu wenu; hapo msifanye kazi yo yote.
9
Jihesabie majuma saba! Watu wakianza kukata ngano kwa miundu, ndipo uanzie kuyahesabu hayo majuma saba.
10
Kisha na ule sikukuu ya Majuma ya Bwana Mungu wako, mkono wako ukimtolea vipaji kwa furaha ya moyo ya kuvifurahia hivyo, Bwwana Mungu wako alivyokubariki.
11
Ndipo, mtakapofurahi mbele ya Bwana mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, wewe na mwanao wa kiume na wa kike na mtumishi wako wa kiume na wa kike, naye Mlawi aliopo malangoni pako, nao wageni, nao waliofiwa na wazazi, nao wajane walioko kwako.
12
Nawe ukumbuke, ya kama ulikuwa mtumwa kule Misri! Kwa hiyo angalia, uyafanye haya maongozi!
13
Sikukuu ya Vibanda utaila siku saba utakapokwisha kuyakusanya yatokayo purioni pako na kamulioni pako.
14
Hiyo sikukuu yako mtaifurahia, wewe na mwanao wa kiume na wa kike na mtumishi wako wa kike na wa kiume, naye Mlawi, nao wageni, nao waliofiwa na wazazi nao wajane waliopo malangoni pako.
15
Siku saba utaila hiyo sikukuu ya Bwana Mungu wako mahali pale, Bwana atakapopachagua. Kwani Bwana Mungu wako atakubarikia mapato yako yote, nazo kazi zote za mikono yako, kwa hiyo utaweza kuwa mwenye furaha.
16
Kila mwaka mara tatu watu wako wote walio wa kiume sharti watokee mbele ya Bwana Mungu wako mahali pale, atakapopachagua: penye sikukuu ya Mikate isiyochachwa na penye sikukuu ya Majuma na penye sikukuu ya Vibanda, lakini wasitokee mbele ya Bwana mikono mitupu!
17
Kila mtu ashike mkononi mwake vipaji vya kuishuuru mbaraka, Bwana Mungu wako aliyokupatia.
18
Jiwekee waamuzi na wenye amri malangoni pako pote, Bwana Mungu wako atakapokupa wewe kuwa pao mashina yako, wawaamue watu maamuzi yaongokayo.
19
Usipotoe mashauri, wala usipendelee uso wa mtu, wala usitwae mapenyezo, kwani mapenyezo huyapofusha nayo macho yao werevu wa kweli, tena huyapotoa maneno ya waongofu.
20
Jihimize kuyafuata yaongokayo kweli, upate kukaa uzimani na kuichukua hiyo nchi, iwe yako, Bwana Mungu wako atakayokupa.
21
Usijipandie miti yo yote ya Ashera kandokando ya mahali pa kumtambikia Bwana Mungu wako, utakapojitengenezea.
22
Wala usijisimamishie nguzo za mawe za kutambikia, kwani Bwana Mungu wako anazichukia.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34