bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 26
Deuteronomy 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 27 →
1
Utakapoingia katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe fungu lako, utakapoichukua na kukaa huko,
2
sharti uchukue malimbuko ya mazao yote ya hiyo nchi, utakayoyatoa katika hiyo nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa. Kisha uyaweke kikapuni, uende mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake.
3
Utakapofika umwendee mtambikaji atakayekuwapo siku hizo, umwambie: Leo hivi ninamshuhudia Bwana Mungu wako, ya kama nimeingia katika hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zetu kutupa sisi.
4
Ndipo, mtambikaji atakapokichukua hicho kikapu mkononi mwako, akiweke mbele ya hapo pa kumtambikia Bwana Mungu wako.
5
Kisha uanze kusema mbele ya Bwana Mungu wako kwamba: Baba yangu alikuwa Mshami mwenye kutangatanga, akashuka Misri, akakaa huko ugenini pamoja na watu wachache, akapata kuwa huko taifa kubwa yenye nguvu na watu wengi.
6
Lakini Wamisri wakatufanyizia mabaya, wakatutesa na kutufanyisha kazi ngumu za utumwa.
7
Ndipo, tulipomlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akazisikia sauti zetu, akayaona mateso yetu na masumbuko yetu na masongano yetu,
8
Bwana akatutoa katika nchi ya Misri kwa kutoa nguvu za kiganja chake na kwa kuukunjua mkono wake na kwa mambo makuu yaliyostusha na kwa vielekezo na kwa vioja,
9
akatuingiza mahali hapa, akatupa nchi hii, nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali.
10
Sasa tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya nchi hii, wewe Bwana uliyonipa. Kisha yaweke mbele ya Bwana Mungu wako na kumwangukia Bwana Mungu wako.
11
Ndivyo, utakavyoyafurahia mema yote, Bwana Mungu wako aliyokupa wewe na mlango wako, uyafurahie wewe pamoja na Mlawi na mgeni atakayekaa kwako.
12
Katika mwaka wa tatu, ndio mwaka wa kutolea mafungu ya kumi, utakapokwisha kuyatoa mafungu ya kumi yote ya mapato yako, umpe Mlawi na mgeni na mwana aliyefiwa na wazazi na mjane, wayale malangoni pako, hata washibe.
13
Kisha useme mbele ya Bwana Mungu wako: Nimeyaondoa nyumbani mwangu yaliyo matakatifu, nikampa Mlawi na mgeni na mwana aliyefiwa na wazazi na mjane, nikayafanya maagizo yako yote sawasawa, kama ulivyoniagiza, sikupita agizo lako lo lote, wala sikusahau mojawapo.
14
Nilipolala tanga sikuyala hata kidogo, wala nilipokuwa mwenye uchafu sikuyaondoa hata kidogo, wala sikutoa mengine kumpa mwenzangu aliyefiwa, ila nimeisikia sauti ya Bwana Mungu wangu, nikayafanya yote, kama ulivyoniagiza.
15
Chungulia toka mbinguni penye Kao lako takatifu, uwabariki walio ukoo wako wa Isiraeli nayo nchi hii, uliyotupa, kama ulivyowaapia baba zetu. Nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali.
16
Leo hivi Bwana Mungu wako anakuagiza kufanya maongozi haya na maamuzi haya, uyaangalie, upate kuyafanya kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.
17
Nawe umesema leo, ya kama unamtaka Bwana, awe Mungu wako, ya kama unataka kuzishika njia zake na kuyaangalia maongozi yake na maagizo yake na maamuzi yake na kuisikia sauti yake.
18
Naye Bwana amekuambia leo, ya kama anakutaka, uwe ukoo wake ulio wake mwenyewe, kama alivyokuagia, tena ya kama anakutaka, uyaangalie maagizo yake yote;
19
tena ya kama anataka kukufanya kuwa mkuu kuliko mataifa yote, aliowafanya, upate matukuzo na jina la utukufu kuliko wao, ni kwamba: upate kuwa ukoo mtakatifu wa Bwana Mungu wako, kama alivyosema.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34