bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 24
Deuteronomy 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 25 →
1
Mtu akichukua mwanamke na kumwoa, naye halafu asipompendeza machoni pake, kwa kuwa ameona kwake neno lisilofaa, na amwandikie cheti cha kuachana na kumpa mkononi mwake, kisha na amtume kwenda zake na kutoka nyumbani mwake.
2
Atakapokwisha kutoka nyumbani mwake, na aende zake kuwa mke wa mtu mwingine.
3
Naye huyu mumewe wa pili atakapochukizwa naye, na amwandikie naye cheti cha kuachana na kumpa mkononi mwake, kisha naye na amtume kwenda zake na kutoka nyumbani mwake. Hata itakapokuwa, huyu mumewe wa pili aliyemchukua kuwa mkewe afe,
4
bwana wake wa kwanza aliyemtuma kwenda kwao hana ruhusa kumchukua kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa uchafu, kwani haya humchukiza Bwana. Kwa hiyo usiikoseshe hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe fungu lako.
5
Mtu akichukua mwanamke mpya asitoke kwenda vitani, wala asifanyishwe kazi yo yote nyingine, sharti mwaka mmoja aachwe tu kukaa nyumbani mwake, amfurahishe mkewe, aliyemchukua.
6
Mtu usimtoze mawe ya kusagia, wala hilo la juu tu kuwa rehani, kwani hivyo ungemtoza yule mtu roho kuwa rehani.
7
Atakapoonekana mtu atakayemwiba mwingine kwao wana wa Isiraeli, amtumie kuwa mtumwa au amwuze, mwizi huyu hana budi kuuawa; ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
8
Jiangalie, utakapopatwa na pigo la ukoma! Yaangalie sana na kuyafanya yote sawasawa, kama watambikaji Walawi watakavyowafunza ninyi! Kama nilivyowaagiza wao, yaangalieni, myafanye vivyo hivyo!
9
Yakumbuke, Bwana Mungu wako aliyomfanyizia Miriamu njiani, mlipotoka Misri.
10
Utakapomkopesha mwenzako cho chote, alichokukopa, usiingie nyumbani mwake kumtoza roho yake,
11
ila usimame nje, yule mtu uliyemkopesha wewe akutolee rehani yake huko nje.
12
Naye kama ni mtu mnyonge, usilale na rehani yake,
13
ila umrudishie rehani yake, jua litakapokuchwa, apate kulala na nguo yake ya kujifunika, akubariki. Hii itakupatia wongofu machoni pake Bwana Mungu wako.
14
Usimkorofishe mtu wa kazi aliye mkiwa na mkosefu wa mali, kama ni wa ndugu zako au mmojawapo wa wageni watakaokaa katika nchi yako malangoni pako,
15
ila umpe mshahara wake siku iyo hiyo, jua lisije kuchwa, akiwa hajapata, kwani ni mkiwa, huutaka sana wa kujitunza, asimlilie Bwana kwa ajili yako, ukawa mwenye kujikosesha.
16
Baba asiuawe kwa ajili ya mwana, wala mwana asiuawe kwa ajili ya baba, ila kila mtu auawe kwa ajili ya kosa lake mwenyewe.
17
Usipotoe shauri la mgeni wala la mwana aliyefiwa na wazazi, wala mjane usimtoze nguo yake kuwa rehani!
18
Nawe kumbuka, ya kama ulikuwa mtumwa huko Misri, Bwana Mungu wako akakukomboa na kukutoa huko. Kwa sababu hii mimi ninakuagiza kuyafanya haya.
19
Utakapoyavuna mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda mmoja shambani, usirudi kuuchukua, ila uache, uwe wa mgeni au wa mwana aliyefiwa na wazazi au wa mjane, Bwana Mungu wako akubarikie kazi zote za mikono yako.
20
Utakapoupukutisha mchekele wako usiurudie tena kuyapukutisha nayo matawi yake, matunda yao na yawe ya mgeni au ya mwana aliyefiwa na wazazi au ya mjane.
21
Utakapochuma mizabibuni kwako, usiirudie mizabibu kuiokoteza. Na iwe ya mgeni au ya mwana aliyefiwa na wazazi au ya mjane.
22
Nawe kumbuka, ya kama ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri! Kwa sababu hii mimi ninakuagiza kuyafanya haya.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34