bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 31
Deuteronomy 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 32 →
1
Mose akaenda, akawaambia Waisiraeli wote maneno haya,
2
akawaambia: Mimi leo ni mwenye miaka 120, siwezi tena kuingia na kutoka, naye Bwana aliniambia: Hutauvuka huu Yordani.
3
Bwana Mungu wako atakutangulia mwenyewe, ukivuka; naye ndiye atakayeyaangamiza mataifa hayo mbele yako, upate kuzichukua nchi zao. Naye Yosua ndiye atakayekuvukisha, kama Bwana alivyosema.
4
Naye Bwana atawafanyizia, kama alivyowafanyizia Sihoni na Ogi, wale wafalme wa Waamori, na wenyeji wa nchi zao, aliowaangamiza.
5
Bwana atawatoa mbele yenu, mwafanyizie na kulifuata agizo, nililowaagiza ninyi.
6
Jipeni mioyo, mpate nguvu, msiwaogope, wala msiwastuke! Kwani Bwana Mungu wako atakwenda pamoja na wewe, hataondoka kwako, wala hatakuacha.
7
Kisha Mose akamwita Yosua, akamwambia machoni pao Waisiraeli wote: Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utaingia na watu hawa katika nchi hiyo, Bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, kisha utawagawia mafungu yao ya nchi.
8
Naye Bwana mwenyewe atakutangulia, awe pamoja na wewe; hataondoka kwako, wala hatakuacha; usiogope, wala usiingiwe na vituko!
9
Mose akayaandika Maonyo haya, akawapa watambikaji, wana wa Lawi waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana, na wazee wote wa Waisiraeli.
10
Kisha Mose akawaagiza kwamba: Kila miaka saba itakapopita, mwaka wa kuachilia madeni utakapotimia, penye sikukuu ya Vibanda,
11
Waisiraeli wote watakapokuja kumtokea Bwana Mungu wako mahali pale, atakapopachagua, ndipo, utakapoyasoma Maonyo haya masikioni pao Waisiraeli wote.
12
Hapo uwakutanishe watu wote, waume na wake na wana na wageni watakaokuwako malangoni pako, wayasikie, wapate kujifunza, wamwogope Bwana Mungu wenu, wayaangalie na kuyafanya maneno yote ya Maonyo haya.
13
Nao wana wao wasioyajua na wayasikie, wapate kujifunza, wamwogope Bwana Mungu wenu siku zote, mtakazokuwako katika hiyo nchi, mnayoivukia Yordani, mpate kuichukua, iwe yenu.
14
Bwana akamwambia Mose: Tazama, siku zako zimetimia, upate kufa! Mwite Yosua, mwende kusimama Hemani mwa Mkutano, nipate kumwagiza kazi. Ndipo, Mose na Yosua walipokwenda kusimama Hemani mwa Mkutano.
15
Bwana akatokea mle Hemani katika wingu lililokuwa kama nguzo, nalo hilo wingu lililokuwa kama nguzo likasimama hapo pa kuliingilia Hema.
16
Bwana akamwambia Mose: Tazama, unakwenda kulala na baba zako. Kisha watu wataondoka kwenda kufanya ugoni wa kufuata miungu migeni ya nchi hiyo, watakayoiingia, lakini mimi wataniacha na kulivunja Agano, nililolifanya nao.
17
Siku hiyo makali yangu yatawawakia, nami nitawaacha na kuuficha uso wangu, wasiuone; kisha wataliwa na kupatwa na mabaya mengi ya kuwasonga. Siku hiyo watasema: Kumbe haya mabaya hayakutupata, kwa kuwa Mungu wetu hayumo katikati yetu?
18
Lakini mimi nitauficha uso wangu kabisa siku hiyo kwa ajili ya mabaya yote, waliyoyafanya walipoigeukia hiyo miungu mingine.
19
Sasa jiandikieni wimbo huu, mwafundishe wana wa Isiraeli na kuutia vinywani mwao, kusudi wimbo huu uwe shahidi wangu kwao wana wa Isiraeli!
20
Kwani nitawaingiza katika hiyo nchi, niliyowaapia baba zao, ichuruzikayo maziwa na asali. Lakini watakapokula na kushiba na kunenepa, ndipo, watakapogeukia miungu mingine, waitumikie na kunibeza mimi na kulivunja Agano langu.
21
Kisha hapo, mabaya mengi ya kuwasonga yatakapowapata, wimbo huu na uwajibu na kuwashuhudia, kwani hautasahauliwa vinywani mwao walio uzao wako. Kwani ninayajua mawazo yao, wanayoyatunga leo, kwa kuwa sijawaingiza bado katika hiyo nchi, niliyowaapia.
22
Siku iyo hiyo Mose akauandika wimbo huo, akawafundisha wana wa Isiraeli kuuimba.
23
Naye Yosua, mwana wa Nuni, Bwana akamwagiza kwamba: Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utawaingiza wana wa Isiraeli katika hiyo nchi, niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja na wewe.
24
Mose alipokwisha kuyaandika maneno ya Maonyo haya katika kitabu na kuyamaliza yote,
25
Mose akawaagiza Walawi waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana kwamba:
26
Kichukueni kitabu cha Maonyo haya, mkiweke kando ndani ya Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, kiwe humo ndani shahidi wako!
27
Kwani ninaujua ukatavu wako na ugumu wa ukosi wako; tazameni, siku hizi za leo, ninapokuwa bado mwenye uzima pamoja nanyi, mmekuwa wenye kumkataa Bwana. Tena itakuwaje, nitakapokwisha kufa?
28
Wakusanyeni mbele yangu wazee wote wa mashina yenu na wakuu wenu, niyaseme masikioni pao hayo maneno ya kuwatajia mbingu na nchi kuwa mashahidi.
29
Kwani ninajua, ya kama hapo, nitakapokwisha kufa, mtafanya mabaya sana mkiondoka katika njia, niliyowaagiza; kwa hiyo ubaya utawapata siku za mwisho, kwani mtayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bana, mmkasirishe kwa kazi za mikono yenu.
30
Kisha Mose akayasema maneno ya wimbo huu masikioni pao wa mkutano wote wa Waisiraeli na kuyamaliza yote.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34