bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 17
Deuteronomy 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 18 →
1
Bwana Mungu wako usimchinjie ng'ombe wala kondoo mwenye kilema au kibaya cho chote! Kwani hayo humchukiza Bwana Mungu wako.
2
Itakuwa, malangoni mwako miongoni mwa miji, Bwana Mungu wako atakayokupa, aonekane mtu mume au mke anayefanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wako kwa kupitana na Agano lake
3
akienda kutumikia miungu mingine na kuitambikia, kama ni jua au mwezi au vikosi vyote vya mbinguni, nisivyokuagiza.
4
Nawe utakapopashwa habari hizi au utakapovisikia tu, sharti utafute vema; kisha utakapoona, ya kuwa neno hilo ni kweli, ikaelekea, ya kama hilo tapisho limefanyika kweli kwao Waisiraeli,
5
huna budi kumtoa malangoni pako huyo mtu mume au mke aliyelifanya hilo neno baya, kisha sharti mmpige mawe huyo mtu mume au mke, hata afe.
6
Kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu mtu apaswaye na kufa ataweza kuuawa, lakini kwa ushahidi wa mtu mmoja mtu asiuawe!
7
Mikono yao mashahidi sharti iwe ya kwanza ya kumwua, kisha mikono yao watu wote na ifuate; hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
8
Itakapokuwa, shauri liwe gumu zaidi la kukushinda, kama wanastakiana manza za damu au unyang'anyi au mapigano au magomvi ya malangoni pako, basi, utainuka, upande kwenda mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua.
9
Utakapofika kwa watambikaji Walawi na kwa mwamuzi atakayekuwako siku hizo uwaulize, nao watakukatia shauri hilo.
10
Nawe sharti uyafanye, watakayokuambia na kukuonyesha njia mahali pale, Bwana atakapopachagua, nawe uangalie, uyafanye yote kuwa sawasawa, kama walivyokufunza.
11
Sharti uyafuate hayo maonyo, watakayokufunza, nayo maamuzi, watakayokuambia, uyafanye hayo maneno, watakayokuonyesha, usiyaache kabisa kwenda kuumeni wala kushotoni.
12
Itakapokuwa, mtu ajikuze, akatae kumsikia mtambikaji anayesimama huko na kumtumikia Bwana Mungu wako au mwamuzi, huyo mtu hana budi kufa; ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo kwao Waisiraeli.
13
Ndipo, watu wote watakaovisikia watakapoogopa, wasijikuze tena.
14
Utakapoingia katika nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako, ukae huko, ndipo, utakaposema: Na nijiwekee mfalme, kama mataifa yote yanayokaa na kunizunguka pande zote yalivyo na wafalme.
15
Napo hapo na umweke yule kuwa mfalme wako, Bwana Mungu wako atakayemchagua katikati ya ndugu zako; yeye ndiye, utakayemweka kuwa mfalme; mtu mgeni asiye ndugu yako hutaweza kumweka kuwa mkuu wako.
16
Lakini angalia, asijitunzie farasi wengi, asiwarudishe watu hawa huko Misri kwa kuwa na farasi wengi, kwani Bwana aliwaambia: Msirudi tena huko na kuishika njia hii!
17
Wala asijipatie wanawake wengi, moyo wake usirudi nyuma! Wala asijiwekee fedha nyingi sana!
18
Lakini hapo, atakapokaa katika kiti chake cha kifalme, sharti ajiandikie mwandiko wa pili wa haya Maonyo katika kitabu na kukifuata kile cha watambikaji Walawi.
19
Hicho kitabu sharti awe nacho, akisome siku zote za maisha yake, kusudi ajifundishe kumcha Bwana Mungu wake na kuyaangalia maneno yote ya haya Maonyo nayo ya haya maongozi, ayafanye.
20
Asijikweze moyoni mwake kuwa mkuu kuliko ndugu zake, wala asiliache hili agizo kwenda wala kuumeni wala kushotoni, siku zake za kuwa mfalme yeye na wanawe katikati ya Waisiraeli zipate kuwa nyingi.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34