bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 27
Deuteronomy 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 28 →
1
Mose pamoja na wazee wa Waisiraeli wakawaagiza watu kwamba: Yaangalieni maagizo yote, mimi ninayowaagiza leo!
2
Siku hiyo, mtakapouvuka Yordani kwenda katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, ujisimikie mawe makubwa na kuyapaka chokaa!
3
Kisha uyaandike maneno yote ya Maonyo haya utakapokwisha kuvuka, kusudi upate kuingia katika nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa. Nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali, kama Bwana Mungu wa baba zako alivyokuambia.
4
Hapo mtakapouvuka Yordani yasimikeni mlimani kwa Ebali mawe haya, ninayowaagiza leo, kisha myapake chokaa!
5
Kisha umjengee huko Bwana Mungu wako mahali pa kumtambikia, napo pajengwe kwa mawe yasiyochongwa kwa chuma cho chote.
6
Hapo pa kumtambikia Bwana Mungu wako sharti upajenge kwa mawe yaliyo mazima, kisha umtolee Bwana Mungu wako juu yake ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
7
Uchinje nazo ng'ombe za tambiko za shukrani, upate kula huko na kumfurahia Bwana Mungu wako.
8
Nayo yale mawe uyaandike maneno yote ya haya Maonyo na kuyachora vema!
9
Kisha Mose na watambikaji Walawi wakawaambia Waisiraeli wote kwamba: Nyamaza kimya, Isiraeli, upate kusikia! Leo hivi umepata kuwa ukoo wake Bwana Mungu wako.
10
Kwa hiyo isikie sauti ya Bwana Mungu wako, uyafanye maagizo yake na maongozi yake, mimi ninayokuagiza leo!
11
Siku hiyo Mose akawaagiza watu kwamba:
12
Hawa na waende kusimama mlimani kwa Gerizimu na kuwabariki hawa watu, mtakapokwisha kuuvuka Yordani: Simeoni na Lawi na Yuda na Isakari na Yosefu na Benyamini.
13
Nao hao na waende kusimama mlimani kwa Ebali na kuapiza: Rubeni na Gadi na Aseri na Zebuluni na Dani na Nafutali.
14
Kisha Walawi na waanze kusema na kuwaambia watu wote wa Waisiraeli kwa kupaza sauti:
15
Na awe ameapizwa mtu atakayefanya kinyago cha kuchonga au cha kuyeyusha na kuvisimamisha na kufichaficha! Kwani Bwana huchukizwa navyo, navyo ni kazi za mikono ya fundi. Nao watu wote na waitikie: Amin!
16
Na awe ameapizwa atakayembeza baba yake na mama yake! Nao watu wote na waitikie: Amin!
17
Na awe ameapizwa atakayeusogeza mpaka wa mwenzake! Nao watu wote na waitikie: Amin!
18
Na awe ameapizwa atakayempoteza kipofu njiani! Nao watu wote na waitikie: Amin!
19
Na awe ameapizwa atakayepotoa shauri la mgeni au la mwana aliyefiwa na wazazi au la mjane! Nao watu wote na waitikie: Amin!
20
Na awe ameapizwa atakayelala na mkewe baba yake! Kwani huko atazifunua nguo za baba yake. Nao watu wote na waitikie: Amin!
21
Na awe ameapizwa atakayelala na nyama wo wote! Nao watu wote na waitikie: Amin!
22
Na awe ameapizwa atakayelala na umbu lake aliye binti baba yake au binti mama yake! Nao watu wote na waitikie: Amin!
23
Na awe ameapizwa atakayelala na mkwewe! Nao watu wote na waitikie: Amin!
24
Na awe ameapizwa atakayempiga mwenzake mahali panapojificha! Nao watu wote na waititike: Amin!
25
Na awe ameapizwa atakayechukua mapenyezo, ampige mtu na kuimwaga damu yake asiyekosa! Nao watu wote na waitikie: Amin!
26
Na awe ameapizwa asiyeyasimamisha maneno ya Maonyo haya na kuyafanya! Nao watu wote na waitikie: Amin!
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34