bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 6
Deuteronomy 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 7 →
1
Nayo haya ndiyo maagizo na maongozi na maamuzi, Bwana Mungu wenu aliyoniagiza, niwafundishe ninyi, mpate kuyafanya katika nchi, mnayoivukia kuichukua, iwe yenu.
2
Sharti umwogope Bwana Mungu wako, uyaangalie maongozi na maagizo yake yote, ninayokuagiza, wewe na wanao na wana wa wanao siku zote za maisha yako, kusudi siku zako zipate kuwa nyingi.
3
Isiraeli, yasikie na kuyaangalia, uyafanye, kusudi uone mema, nanyi mpate kuwa wengi sana, kama Bwana Mungu wa baba zako alivyokuagia kukupa nchi ichuruzikayo maziwa na asali.
4
*Sikia, Isiraeli: Bwana Mungu wetu ni Bwana peke yake.
5
Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu yako yote.
6
Maneno haya, ninayokuagiza leo, sharti yawe moyoni mwako.
7
Jikaze kuwafundisha watoto wako na kuyasema nao ukikaa nyumbani mwako, ukienda safari zako, ukitaka kulala, hata ukiamka!
8
Yafunge mkononi pako kuwa kielekezo, yawe napo pajini pako katikati ya macho yako!
9
Yaandike vizingitini namo milangoni nyumbani mwako!
10
Hapo Bwana Mungu wako atakapokuingiza katika hiyo nchi, aliyowaapia baba zako Aburahamu na Isaka na Yakobo, kwamba akupe wewe miji mikubwa mizuri, usiyoijenga,
11
na nyumba zijaazo mema yote, usizozijaza, na visima vilivyochimbuliwa, usivyovichimbua, na mizabibu na michekele, usiyoipanda, basi, hapo utakapoila na kushiba,
12
jiangalie, usimsahau Bwana aliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa!
13
Mwogope Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye! Hapo utakapoapa litaje Jina lake!*
14
Msifuate miungu mingine miongoni mwa miungu ya makabila yanayowazunguka!
15
Kwani Bwana Mungu wako anayekaa katikati yako ni Mungu mwenye wivu; angalia, makali yake Bwana Mungu wako yasikuwakie, akakuangamiza, utoweke juu ya nchi.
16
Msimjaribu Bwana Mungu wenu, kama mlivyomjaribu kule Masa.
17
Yaangalieni sana maagizo ya Bwana Mungu wenu na mashuhuda yake na maongozi yake, aliyoyaagiza!
18
Yafanye yaongokayo nayo yafaayo machoni pake Bwana, kusudi uone mema, upate kuingia katika hiyo nchi njema, Bwana aliyowaapia baba zako, uichukue, iwe yako.
19
Naye na akupe kuwakimbiza adui zako wote mbele yako, kama Bwana alivyosema.
20
Mwanao atakapokuuliza siku zijazo kesho kwamba: Nini maana yao haya mashuhuda na maongozi na maamuzi, Bwana Mungu wetu aliyowaagiza ninyi?
21
ndipo umwambie mwanao: Sisi tulikuwa watumwa wa Farao kule Misri, lakini Bwana akatutoa Misri kwa mkono wake wenye nguvu,
22
Bwana alipofanya machoni petu kule Misri vielekezo na vioja vikubwa vilivyomwogopesha Farao na mlango wake wote.
23
Ndivyo, alivyotutoa huko na kutuleta huku, atupe nchi hii, aliyowaapia baba zenu.
24
Ndipo, Bwana alipotuagiza kuyafanya haya maongozi yote kwa kumcha Bwana Mungu wetu, tuone mema siku zote za maisha yetu, kama inavyoelekea leo.
25
Nao wongofu wetu ndio huu wa kujiangalia, tuyafanye haya maagizo yote mbele ya Bwana Mungu wetu, kama alivyotuagiza.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34