bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 19
Deuteronomy 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 20 →
1
Bwana Mungu wako atakapokwisha kuyang'oa hayo mataifa walio wenye hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako, ukae mijini mwao namo nyumbani mwao,
2
ndipo ujitengee miji mitatu katikati ya hiyo nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako.
3
Utakapojitengenezea njia za kwenda huko uanze kuigawanya mipaka ya hiyo nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe yako mwenyewe, uitoe mafungu matatu, mwuaji apate pa kukimbilia.
4
Nalo shauri lake mwuaji atakayekimbilia kwako, apate kupona, liwe hivyo: Itakuwa, mtu ampige mwenzake pasipo kuvijua, pasipo kuwa mchukivu wake tangu zamani.
5
Itakuwa, kama mtu akienda na mwenzake mwituni kukata kuni, napo hapo, mkono wake ulipolipandisha shoka kukata mti, chuma kikachomoka katika kipini, kikampata mwenzake, naye akafa, basi, hapo na akimbilie miji hiyo mmojawapo, apate kupona.
6
Naye mwenye kuilipiza hiyo damu asimkimbize huyo mwuaji kwa ajili ya moto huo unaowaka moyoni mwake, amkamate, kwa kuwa njia ni ndefu, ampige, azimie roho, naye yule hakukora manza za kuuawa, kwani hakuwa mchukivu wake tangu zamani.
7
Kwa sababu hii mimi ninakuagiza kwamba: Jitengee miji mitatu!
8
Tena itakuwa, Bwana Mungu wako aipanue mipaka yako, kama alivyowaapia baba zako, ya kuwa atawapa.
9
Hivi vitakuwa, ukiyaangalia na kuyafanya haya maagizo yote, mimi ninayokuagiza leo, umpende Bwana Mungu wako, uzishike njia zake siku zote; basi, hapo, hivyo vitakapotimia, sharti hiyo miji mitatu uiongeze kwa kujitengea mji mitatu mingine,
10
ni kwamba: katikati ya hiyo nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, iwe fungu lako, isimwagwe damu ya mtu asiyekora manza za kufa, hiyo damu ikakukalia wewe.
11
Lakini mtu akiwa mchukivu wa mwenzake, akamvizia na kumnyatianyatia, mwisho akampata, ampige na kuizimiza roho yake, afe kabisa; napo, atakapokimbilia miji hiyo mmojawapo,
12
wazee wa mji wake na watume watu, wamchukue kule na kumtia mikononi mwake mlipiza hiyo damu, afe.
13
Jicho lako lisimwonee machungu, upate kuondoa kwao Waisiraeli damu ya mtu asiyekora manza za kufa. Ndipo, utakapoona mema.
14
Usimsogezee mwenzako mipaka, wakale waliyoikata penye fungu lako, utakalolichukua, liwe lako katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako.
15
Mtu mmoja asimwondokee mwingine katika shauri la manza zo zote, wala la ukosaji wo wote uliomkosesha mtu kosa lo lote, watu wanalolikosa, ila shauri litawezekana tu kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.
16
Shahidi mkorofi atakapomwinukia mwenzake kumsingizia upotovu,
17
Nao watu wawili wanaobishana na waende kusimama mbele ya Bwana na mbele ya watambikaji na mbele ya waamuzi watakaokuwapo siku hizo,
18
nao waamuzi na watafute vema sana iliyo kweli. Nao watakapoona, ya kama yule shahidi ni shahidi wa uwongo, naye alitaka kumkorofisha ndugu yake kwa uwongo,
19
basi, na mmfanyie yaleyale, aliyoyawazia kumfanyizia ndugu yake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
20
Wao wengine wasiokuwapo watakapovisikia wataogopa, wasiendelee kufanya mambo mabaya kama hayo katikati yako.
21
Jicho lako lisiwaonee machungu, ila uwatoze roho kwa roho, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34