bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Ezekiel 10
Ezekiel 10
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 11 →
1
Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya makerubi kulikuwa kitu kinachofanana na jiwe la rangi ya samawi, umbo lake kama kiti cha kifalme.
2
Mungu akamwambia yule mutu aliyevaa nguo ya kitani: Kwenda katikati ya magurudumu yanayokuwa chini ya makerubi, ujaze mikono yako na makaa ya moto unaokuwa katikati yao na kuyasambaza juu ya muji. Nikamwona akienda.
3
Wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa nyumba ya Yawe, yule mutu alipoingia ndani; wingu likafunika kiwanja cha ndani.
4
Utukufu wa Yawe ukapanda juu tokea wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na kiwanja kilijaa mwangaza wa utukufu wa Yawe.
5
Shindo la mabawa ya makerubi iliweza kusikilika hata kwenye kiwanja cha inje, kama sauti ya Yawe wa majeshi anaposema.
6
Yawe alipomwamuru yule mutu aliyevaa nguo ya kitani atwae moto toka katikati ya magurudumu yaliyokuwa chini ya makerubi, yule mutu alikwenda na kusimama pembeni ya gurudumu moja.
7
Kerubi mumoja akanyoosha mukono wake kwa kutwaa moto uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa sehemu yake na kuutia katika mikono ya yule mutu aliyevaa nguo ya kitani; naye alipoupokea, akajiendea.
8
Makerubi hao walionekana kuwa na kitu kama mukono wa mutu chini ya mabawa yao.
9
Niliangalia, nikaona kulikuwa magurudumu mane, gurudumu moja pembeni ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama jiwe la zabarajadi.
10
Yote mane yalionekana kuwa ya namna moja, na kila gurudumu lilionekana kama liko ndani ya gurudumu lingine.
11
Yaliweza kwenda pande zote bila kugeuka; kule gurudumu la kwanza lilielekea, yote yalifuata.
12
Miili ya hao makerubi, migongo yao, mikono na mabawa yao, pamoja na magurudumu, vyote vilijaa macho pande zote.
13
Niliambiwa kwamba magurudumu yale yanaitwa “Magurudumu Yanayozunguka”.
14
Kila kerubi alikuwa na nyuso ine: uso wa kwanza ulikuwa wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa ine ulikuwa wa tai.
15
Makerubi wakanyanyuka juu. Hawa ndio vile viumbe niliowaona karibu na muto Kebari.
16
Makerubi wale walipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda pembeni yao. Walipokunjua mabawa yao kusudi wapande juu, magurudumu nayo yalikwenda pamoja nao.
17
Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopanda juu, magurudumu nayo yalipanda pamoja nao. Maana roho wa hao viumbe ilikuwa katika magurudumu hayo.
18
Kisha utukufu wa Yawe ulitoka kwenye kizingiti cha nyumba, ukaenda na kusimama juu ya wale makerubi.
19
Makerubi wakakunjua mabawa yao, wakapanda juu, mimi nikiwa ninawaona na yale magurudumu yalikuwa pembeni yao. Wakasimama mbele ya mulango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Yawe, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
20
Hawa walikuwa wale viumbe niliowaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na muto Kebari, nami nikatambua kwamba ni makerubi.
21
Kila mumoja wao alikuwa na nyuso ine na mabawa mane na chini ya kila bawa kulikuwa kitu kinachokuwa kama mukono wa mutu.
22
Vilevile nilizitambua nyuso zao: zilikuwa zilezile nilizokuwa nimeziona kule kwenye muto Kebari. Kila kiumbe kilikwenda mbele, moja kwa moja.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48