bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Ezekiel 27
Ezekiel 27
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 28 →
1
Neno la Yawe lilinifikia kusema hivi:
2
Sasa ewe mwanadamu, imba wimbo huu wa maombolezo juu ya muji wa Tiro.
3
Muji wenye kuwa karibu ya bahari, unaofanya biashara na mataifa ya visanga vingi. Umwambie: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ewe Tiro, wewe umejivuna kuwa muzuri kwelikweli!
4
Mipaka yako imeenea kwelikweli! Umejengwa kama mashua nzuri.
5
Waliokujenga walitumia miti ya misunobari ya kutoka Seniri kwa kupasua mbao zako zote; walitwaa mierezi kutoka Lebanoni kwa kukutengenezea mulingoti.
6
Walitwaa miti ya mialo toka Basani wakakuchongea makasia; walikutengenezea mbao za kuikalia kwa miti ya misunobari ya kisanga cha Kipuro, na kuipamba kwa pembe ya tembo.
7
Kitani kilichopindwa vizuri kutoka Misri kilikuwa kwa kupamba tanga lako na kwa ajili ya bendera yako. Chandarua chako kilitengenezwa na nguo ya rangi ya samawi na nyekundu-nyeusi kutoka visanga vya Elisa.
8
Watu wa miji Sidona na Arwadi walikuwa wapiga makasia wako. Wenye hekima wako walikuwa ndani wakifanya kazi ya kuongoza.
9
Wazee wa Gebali na wafundi wao walikuwa wakiziba nyufa zako. Wachuuzi wa bahari waliokuwa wakipitia kwako walifanya biashara nawe.
10
Watu kutoka Persia, Ludi na Puti walijiunga katika kundi lako la waaskari; walilundika ngao zao na kofia zao kwenye kambi zao za kiaskari. Waaskari hao walikupatia utukufu.
11
Watu wa Arwadi pamoja na waaskari wako walilinda kuta zako pande zote, nao watu wa Gamadi walilinda minara yako. Walitundika ngao zao kwenye kuta zako pande zote, na hivyo wakaukamilisha uzuri wako.
12
Watu wa Tarsisi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mwingi na wa kila namna. Walitoa feza, chuma, bati, na risasi kwa kupata biashara yako.
13
Watu wa Yavani, Tubali na Meseki, walifanya biashara nawe, wakakupatia watumwa na vifaa vya shaba wapate vitu vyako.
14
Uliuzisha biashara yako huko Beti-Togarma kwa kujipatia farasi wa kubeba mizigo na farasi wa vita, ngamia na nyumbu.
15
Watu wa Dedani walifanya biashara nawe. Inchi nyingi za kandokando ya bahari zilikuwa masoko yako makubwa. Watu wake walikuletea pembe za tembo na miti mizuri inayoitwa ebene kwa kununua vitu kwako.
16
Watu wa Edomu walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa vitu vyako. Kwa kupata vitu vyako walikupa akiki, vitambaa vya rangi nyekundu-nyeusi, vitambaa vilivyopindwa vizuri, kitani safi, matumbawe na yakuti.
17
Hata watu wa inchi ya Yuda na ya Israeli walifanya biashara nawe; walikupa ngano, mizeituni, tini za kwanzakwanza, asali, mafuta na marasi kwa kununua vitu kwako.
18
Watu wa Damasiki walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa vitu vyako; walikupa divai kutoka muji wa Helboni na manyoya meupe ya kondoo.
19
Wedani na Yavani walisafirisha vitu vyako toka muji wa Uzali; hata chuma kilichofuliwa, mudalasini na muchaichai kwa kununua vitu kwako.
20
Watu wa Dedani walifanya biashara nawe kwa kukupatia matandiko ya farasi.
21
Waarabu na wakubwa wote wa inchi ya Kedari walikuwa wachuuzi wako wakubwa katika biashara ya wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.
22
Wachuuzi wa Seba na wa Rama walifanya biashara nawe; walikuletea viungo vya chakula, mawe ya bei kali na zahabu kwa kujipatia vitu vyako safi.
23
Wakaaji wa miji ya Harani, Kane na Edeni na wachuuzi wa Asuria na Kilmadi walifanya biashara nawe.
24
Hao walifanya nawe biashara ya nguo za bei kali, nguo za rangi nyekundu nyeusi zilizopindwa vizuri, nguo za rangi mbalimbali na kamba ngumu zilizosokotwa.
25
Mashua makubwa za Tarsisi ndizo zilikusafirishia vitu vyako. Basi wewe ulikuwa umejaa vitu kama vile mashua katikati ya bahari.
26
Wavuta makasia wako walikupeleka mbali katika bahari. Upepo mukali wa mashariki umekuvunjavunja ukiwa mbali katikati ya bahari.
27
Mali yako, biashara yako, na vitu vyako, waongozi wako wote katika chombo, wafundi wako wa mashua na wachuuzi wako, waaskari wako wote wanaokuwa kwako, pamoja na wasafiri wanaokuwa kwako, vyote vitaangamia ndani ya bahari, siku ile ya kuangamizwa kwako.
28
Kilio cha waongozi wako kitakaposikilika, inchi za kandokando ya bahari zitatetemeka.
29
Halafu wavuta makasia wote wataziacha mashua zao. Waongozi wote wa mashua watakaa inchi kavu.
30
Wataomboleza kwa uchungu wa moyo juu yako, na kulia kwa uchungu mukubwa; watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao na kugaagaa kwenye majivu.
31
Watajinyoa vichwa kwa ajili yako na kuvaa gunia. Watalia kwa uchungu wa moyo juu yako.
32
Wataimba wimbo wa maombolezo juu yako; Nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro katikati ya bahari?
33
Vitu vyako vilipofika katika inchi za ngambo, ulitimiza mahitaji ya watu wengi! Kwa wingi wa utajiri wa vitu vyako uliwatajirisha wafalme wa dunia.
34
Lakini sasa umevunjikia ndani ya bahari; umeangamia katika vilindi vya maji. Biashara yako na watu wote waliokuwa ndani yako vimezama pamoja nawe.
35
Wakaaji wote wa visanga wameshangaa sana juu yako; wafalme wao wameogopa sana, nyuso zimekunjamana kwa huzuni.
36
Wachuuzi wa mataifa watakuzomea! Umekuwa kitu cha kuogopesha, na umetoweka kwa milele!
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48