bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Ezekiel 35
Ezekiel 35
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 36 →
1
Neno la Yawe lilinifikia kusema hivi:
2
Wewe mwanadamu! Ugeukie upande wa mulima Seiri, utoe unabii juu ya wakaaji wake.
3
Uwaambie kwamba: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Mimi ninapingana nawe, ee mulima Seiri. Ninanyoosha mukono wangu juu yako na kukufanya ukuwe jangwa na ukiwa.
4
Ninaifanya miji yako kuwa mabomoko nawe utakuwa jangwa. Halafu utatambua kwamba mimi ni Yawe.
5
Ulikuwa adui wa siku zote wa Waisraeli, ukasababisha watu wake wauawe kwa upanga, wakati wa musiba wao, wakati wa azabu yao ya mwisho.
6
Kwa hiyo, kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– kifo kinakungoja na hautaweza kukiepuka. Uko na makosa ya mauaji, basi mauaji nayo yatakuandama.
7
Nitaufanya mulima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote atakayepitia huko nitamwangamiza.
8
Nitajaza milima yako watu waliouawa; na katika vilima vyako na mabonde yako na mitelemuko yako yote kutakuwa watu waliouawa kwa upanga.
9
Nitakufanya kuwa jangwa milele, na miji yako haitakaliwa tena. Halafu utatambua kwamba mimi ni Yawe.
10
Wewe ulisema kwamba mataifa hayo mawili, ni kusema inchi ya Yuda na ya Israeli, ni mali yako na kwamba utazirizi! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Yawe.
11
Kwa hiyo, kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– nitakutendea kadiri ya hasira na wivu wako, kulingana na chuki yako kwao. Nitakapokuazibu utatambua mimi ni nani!
12
Wewe utajua kwamba mimi mwenyewe Yawe nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa juu ya milima ya Waisraeli, ukisema: Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Imetolewa kusudi tupate kuinyanganya!
13
Nimesikia jinsi unavyojivuna na kusema maneno mengi juu yangu.
14
Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitakapokufanya wewe Edomu kuwa jangwa, dunia yote itafurahi
15
kama wewe ulivyofanya wakati inchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mulima Seiri, pamoja na inchi yote ya Edomu. Halafu watu watatambua kwamba mimi ni Yawe.
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 36 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48