bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 1
Matthew 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
1
Chuo cha uzao wake Yesu Kristo, mwana wa Dawidi, mwana wa Aburahamu, ni hiki:
2
Aburahamu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na nduguze,
3
Yuda na Tamari wakamzaa Peresi na Zera, Peresi akamzaa Hesiromu, Hesiromu akamzaa Ramu,
4
Ramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nasoni, Nasoni akamzaa Salmoni.
5
Salmoni na Rahabu wakamzaa Boazi, Boazi na Ruti wakamzaa Obedi, Obedi akamzaa Isai,
6
Isai akamzaa mfalme Dawidi.
7
Dawidi na mkewe Uria wakamzaa Salomo,
8
Salomo akamzaa Rehabeamu, Rehabeamu akamzaa Abia, Abia akamzaa Asafu, Asafu akamzaa Yosafati, Yosafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia,
9
Uzia akamzaa Yotamu, Yotamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hizikia,
10
Hizikia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia,
11
Yosia akamzaa Yekonia na nduguze siku zile, walipohamishwa kwenda Babeli.
12
Walipokwisha kuhamishwa kwenda Babeli, Yekonia akamzaa Saltieli, Saltieli akamzaa Zerubabeli,
13
Zerubabeli akamzaa Abihudi, Abihudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azoro,
14
Azoro akamzaa Sadoko, Sadoko akamzaa Ahimu, Ahimu akamzaa Elihudi,
15
Elihudi akamzaa Elazari, Elazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo,
16
Yakobo akamzaa Yosefu, mumewe Maria aliyekuwa mama yake Yesu aitwaye Kristo.
17
Basi, vizazi vyote tangu Aburahamu mpaka Dawidi ni vizazi 14; tangu Dawidi mpaka kuhamishwa kwenda Babeli ni vizazi 14, tena tangu kuhamishwa kwenda Babeli mpaka Kristo ni vizazi 14.
18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria, mama yake, alionekana ana mimba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu hapo, alipokuwa ameposwa na Yosefu, nao walikuwa hawajakaribiana.
19
Yosefu, mchumba wake, alikuwa mwongofu, tena hakutaka kumwumbua, kwa hiyo alitaka kumwacha tu, watu wasijue.
20
Alipokuwa akiyafikiri haya, mara malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akisema: Yosefu, mwana wa Dawidi, usiogope kumwoa Maria, Mchumba wako, kwani kitakachozaliwa naye ni cha Roho Mtakatifu.
21
Atazaa mtoto mwanamume, naye utamwita jina lake Yesu. Kwani yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika makosa yao.
22
Haya yote yalifanyika, lipate kutimia lililonenwa na Bwana kwa mfumbuaji:
23
Tazama, mwanamwali atapata mimba, atazaa mtoto mwanamume, nalo jina lake watamwita Imanueli, ni kwamba: Mungu yuko nasi.*
24
Yosefu alipoamka katika usingizi akatenda, kama malaika wa Bwana alivyomwagiza. Akamwoa mchumba wake,
25
lakini hakumkaribia, mpaka alipomzaa mwanawe wa kwanza. Akamwita jina lake YESU.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28