bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 13
Matthew 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
1
Siku ile Yesu alitoka nyumbani, akaenda kukaa kandokando ya bahari.
2
Wakamkutanyikia makundi mengi ya watu, kwa hiyo akaingia chomboni, akakaa humo, watu wote wakisimama pwani.
3
Akawaambia maneno mengi kwa mifano akisema: Tazameni, mpanzi alitoka kumiaga mbegu.
4
Ikawa alipozimiaga, nyingine zikaangukia njiani; ndege wakaja, wakazila.
5
Nyingine zikaangukia penye miamba pasipo na udongo mwingi. Kuota zikaota upesi kwa kuwa na udongo kidogo;
6
lakini jua lilipokuwa kali, zikanyauka, kwa kuwa hazina mizizi.
7
Nyingine zikaangukia penye miiba; nayo miiba ilipoota ikazisonga.
8
Lakini nyingine zikaangukia penye mchanga mzuri, zikazaa, nyingine punje mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.
9
Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
10
Wanafunzi wake wakamjia, wakamwambia: Sababu gani unasema nao kwa mifano?
11
Naye akajibu akisema: Ninyi mmepewa kuyatambua mafumbo ya ufalme wa mbingu,
12
lakini wale hawakupewa. Kwani ye yote aliye na mali atapewa, ziwe nyingi zaidi; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
13
Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano, kwamba wakitazama wasione, wakisikiliza wasisikie na kujua maana.
14
Hivyo ufumbuo wa Yesaya unatimizwa kwao unaosema: Kusikia mtasikia, lakini hamtajua maana; kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
15
Kwani mioyo yao walio ukoo huu imeshupazwa, hata kwa masikio yao yaliyo mazito hawasikii; nayo macho yao wameyasinziza, wasije wakaona kwa macho, au wakasikia kwa masikio, au wakajua maana kwa mioyo, wakanigeukia, nikawaponya.
16
Lakini yenye shangwe ni macho yenu, kwani huona, nayo masikio yenu, kwani husikia.
17
Kweli nawaambiani: Wengi waliokuwa wafumbuaji na waongofu waliyatunukia, wayaone, mnayoyaona ninyi, lakini hawakuyaona; waliyatunukia wayasikie, mnayoyasikia ninyi, lakini hawakuyasikia.
18
Basi, ninyi usikieni mfano wa mpanzi!
19
Kila anayelisikia Neno la ufalme asipolijua maana, huja yule Mbaya na kulinyakua lililomiagwa moyoni mwake. Hizo ndizo zilizomiagwa njiani.
20
Lakini zilizomiagwa penye miamba ni kama mtu anayelisikia Neno na kulipokea papo hapo kwa furaha.
21
Lakini hana mizizi moyoni mwake, ila analishika kwa kitambo kidogo tu. Yanapotukia maumivu au mafukuzo kwa ajili ya Neno, mara hujikwaa.
22
Lakini zilizomiagwa penye miiba ni kama mtu anayelisikia Neno, lakini masumbuko ya dunia hii na udanganyifu wa mali hulisonga Neno, lisizae matunda.
23
Lakini zilizomiagwa penye mchanga mzuri ni kama mtu anayelisikia Neno na kulijua maana. Ndiye mwenye kuzaa, mwingine huleta punje mia, mwingine sitini, mwingine thelathini.
24
*Akawatolea mfano mwingine akisema: Ufalme wa mbingu umefanana na mtu aliyemiaga mbegu nzuri katika shamba lake.
25
Lakini watu walipolala, akaja mchukivu wake, akamiaga mbegu za nyasi katikati ya ngano, akaenda zake.
26
Halafu majani ya ngano yalipoota na kuchanua, zikaonekana nazo nyasi.
27
Watumwa wa mwenye shamba wakaja wakamwuliza: Bwana, hukumiaga mbegu nzuri katika shamba lako? Basi, nyasi limezipata wapi?
28
Alipowaambia: Mtu aliye mchukivu amevifanya hivyo, watumwa wakamwambia: Unataka, twende, tuzing'oe na kuzikusanya?
29
Akasema: Hapana, msije, mkazing'oa nazo ngano mkiwa mnakusanya nyasi.
30
Acheni, zikue zote mbili pamoja, mpaka mavuno yatakapokuwa! Siku za kuvuna nitawaambia wavunaji: Kusanyeni kwanza nyasi, mzifunge matitatita, mziteketeze! Lakini ngano zitieni chanjani kwangu!*
31
*Akawatolea mfano mwingine akisema: Ufalme wa mbingu umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukipanda katika shamba lake.
32
Nacho ni kidogo kuliko mbegu zote. Lakini kinapokua ni mkubwa kuliko miboga yote inayopandwa, huwa mti mzima, hata ndege wa angani huja na kutua katika matawi yake.
33
Akawaambia mfano mwingine: Ufalme wa mbingu umefanana na chachu, mwanamke akiitwaa akaichanganya na pishi tatu za unga, mpaka ukachachwa wote.
34
Haya yote aliwaambia makundi ya watu kwa mifano, pasipo mfano hakuwaambia neno,
35
kusudi litimie lililosemwa na mfumbuaji, akisema: Nitakifumbua kinywa changu, kiseme mifano. Nitatangaza mambo yaliyofichika tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa.*
36
Kisha Yesu akawaaga makundi ya watu, akaingia nyumbani. Ndipo, wanafunzi wake walipomjia wakisema: Tuelezee mfano wa nyasi za shambani!
37
Akajibu akisema: Mwenye kumiaga mbegu nzuri ni Mwana wa mtu.
38
Nalo shamba ndio ulimwengu. Nazo mbegu nzuri ndio wana wa ufalme. Lakini nyasi ndio wana wa yule Mbaya.
39
Naye mchukivu aliyezimiaga ndiye Msengenyaji. Nayo mavuno ndio mwisho wa dunia. Nao wavunaji ndio malaika.
40
Kama nyasi zinavyokusanywa na kuteketezwa motoni, ndivyo, itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii:
41
Mwana wa mtu atawatuma malaika zake, nao watakusanya na kuyatoa katika ufalme wake makwazo yote nao waliofanya maovu,
42
wawatupe shimoni mwa moto; ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
43
Ndipo, waongofu watakapoangaza kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
44
*Ufalme wa mbingu umefanana na fedha zilizofukiwa shambani. Mtu alipoziona akazifukia, akaenda kwa furaha yake, akaviuza vyote, alivyokuwa navyo, akalinunua shamba lile.
45
Tena ufalme wa mbingu umefanana na mchuuzi aliyetafuta ushanga wa lulu nzuri.
46
Naye alipoona lulu moja yenye bei kubwa akaenda, akaviuza vyote alivyokuwa navyo, akainunua.*
47
Tena ufalme wa mbingu umefanana na wavu uliotupwa baharini, ukakusanya samaki wa kila mtindo.
48
Hata ulipojaa, wakauvuta pwani, wakakaa, wakawachagua samaki, walio wazuri wakawaweka vyomboni, lakini walio wabaya wakawatupa.
49
Hivyo ndivyo, itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii: Malaika watatokea, watawatenga wabaya kati ya waongofu,
50
wawatupe shimoni mwa moto. Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
51
Mmeijua maana ya hayo yote? Walipomwambia: Ndio,
52
akawaambia: Kwa sababu hii kila mwandishi aliyefundishiwa ufalme wa mbingu amefanana na mtu mwenye nyumba anayetoa mawekoni mwake mambo mapya na ya kale.
53
Ikawa, Yesu alipokwisha kuisema mifano hiyo akatoka, akaenda zake.
54
Alipofika kwao, alikokulia, akawafundisha katika nyumba yao ya kuombea, nao wakashangaa wakisema: Huyu amepata wapi werevu huu ulio wa kweli na nguvu hizi?
55
Huyu si mwana wa seremala? Mama yake si yeye anayeitwa Maria? Nao ndugu zake sio akina Yakobo na Yosefu na Simoni na Yuda?
56
Nao maumbu zake hawako wote kwetu? Basi, huyu amepata wapi haya yote? Wakajikwaa kwake.
57
Yesu akawaambia: Mfumbuaji habezwi, isipokuwa kwao, alikokulia, namo nyumbani mwake.
58
Kwa hiyo hakufanya kule ya nguvu mengi, kwa sababu walikataa kumtegemea.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28