bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 19
Matthew 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 20 →
1
Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, akaondoka Galilea, akaja mipakani kwa Yudea ng'ambo ya Yordani.
2
Wakamfuata makundi mengi ya watu akawaponya huko.
3
Nao Mafariseo wakamjia, wakamjaribu wakimwuliza: Iko ruhusa, mtu amwache mkewe kwa sababu yo yote?
4
Naye akajibu akisema: Hamkusoma, ya kuwa Muumbaji hapo mwanzo aliwaumba mume na mke, akasema:
5
Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake, agandamiane na mkewe, nao hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6
Kwa hiyo sio wawili tena, ila wamekuwa mwili mmoja tu. Basi, Mungu alichokiunga, mtu asikiungue!
7
Wakawambia: Mose aliagiziaje tena kuwapa watu cheti cha kuachana, kisha kuwaacha?
8
Akawaambia: kwa ajili ya ugumu wa mioyo yenu Mose aliwapa ruhusa ya kuwaacha wake zenu. Lakini tokea hapo mwanzo havikuwapo hivyo.
9
Nami nawaambiani: Mtu akimwacha mkewe, isipokuwa kwa ajili ya ugoni, akaoa mwingine, anazini; naye anayeoa mke aliyeachwa anazini.
10
Wanafunzi wakamwambia: Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11
Naye akawaambia: Sio wote wanaoweza kuitambua maana yake neno hili, ni wale tu waliofunuliwa.
12
Kwani katika watu wasiozaa, wako waliozaliwa hivyo tangu tumboni mwa mama zao. Tena wako wengine waliokomeshwa na watu, wasizae. Tena wako wengine waliojikomesha wenyewe, wasizae kwa ajili ya ufalme wa mbingu. Anayeweza kuitambua maana na aitambue!
13
Hapo ndipo, alipoletewa vitoto, awabandikie mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi waliwatisha.
14
Ndipo, Yesu aliposema: Waacheni vitoto, msiwazuie kuja kwangu! Kwani walio hivyo ufalme wa mbingu ni wao
15
Akawabandikia mikono; kisha akaondoka pale, akaenda zake.
16
Hapo ndipo mmoja alipomjia na kusema: Mfunzi mwema, nifanye jambo jema gani, niupate uzima wa kale na kale?
17
Naye akamwambia: Unaniulizaje jambo lililo jema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia uzimani yashike maagizo!
18
Alipomwuliza: Yapi? Yesu akasema: Ni haya: Usiue! Usizini! Usiibe! Usisingizie!
19
Mheshimu baba na mama! nalo hilo: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
20
Yule kijana akamwambia: Hayo yote nimeyashika; ninalolisaza la kulifanya ni nini tena?
21
Yesu akamwambia: Ukitaka kuyatimiza yote nenda, uviuze, ulivyo navyo, uvigawie maskini! Hivyo utakuwa na kilimbiko mbinguni. Kisha uje, unifuate!
22
Lakini yule kijana alipolisikia neno hili akaenda zake na kusikitika, kwani alikuwa mwenye mali nyingi.
23
Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake: Kweli nawaambiani: Ni vigumu, mwenye mali aingie katika ufalme wa mbingu.
24
Tena nawaambiani: Masumbuko ya ngamia ya kupenya tunduni mwa sindano ni madogo kuliko yake mwenye mali ya kuingia ufalme wa Mungu.
25
Wanafunzi walipoyasikia wakastuka sana, wakasema: Ikiwa hivyo, yuko nani awezaye kuokoka?
26
Yesu akawachungua, akawaambia: Kwa watu neno hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.
27
Hapo Petero akamjibu akimwambia: Tazama, sisi tumeviacha vyote, tukakufuata wewe; basi, tutapata nini?
28
Ndipo, Yesu alipowaambia: Kweli nawaambiani: Siku, ulimwengu utakapopata kuwa mpya, Mwana wa mtu atakapokaa katika kiti cha utukufu wake, hapo ndipo nanyi mlionifuata mimi mtakapokaa katika viti vya kifalme kumi na viwili, myahukumu hayo mashina kumi na mawili ya Isiraeli.
29
Ndipo, kila mtu aliyeacha nyumba au kaka au dada au baba au mama au wana au mashamba kwa ajili ya Jina langu atakapoyapata tena na kuongezwa mara nyingi, kisha ataurithi nao uzima wa kale na kale.
30
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, nao walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28